Kuhusu kuondoa Ukomo wa Rais John Magufuli

Kuhusu kuondoa Ukomo wa Rais John Magufuli

Kwanza sijaelewa mantiki ya kuondoa term limit

Kuna ambao wanasema ili akamilishe miradi yake

Najiuliza kwani yeye ndiye mkandarasi?

Yeye si msimamizi : anaweza kuitoa au kuiacha iendelee
 
Shida hapa siyo Rais JPM kuongezewa muda, ni wabunge, Madiwani mizigo ambao hawana uwezo wakushinda nafasi zao bali kwa upepo wa JPM. Acheni uzembe wa kufikiri pambaneni watumikieni wananchi kila mmoja atavuna alichopanda.

Sawa, Maoni yako ni yapi ?
 
Baraka Obama is a smart president ametawala 8 years. Msishabikie kitu kama hiki kuongeza ukomo wa Rais nikufukua makaburi tutakayo yakuta tusiseme hatukuambiwa. Yes we need Magufuli but we need to grow new leadership. Nayeye awe mshauri.
Hata kwa ushauri hafai. Ametutenga sana kiitikadi, kikanda na kikabila. Ana utawala wa KIDIKTETA ambao siyo mzuri kuacha mwingine akaufuata
 
Ukitaka kujua nia ya magufuli kuhusu kuongeza muda wa utawala,tazama kwanza watu anaoambatana nao ndio utajua;Museven,Kagame,Nkurunziza,Kabila.

Wewe maoni yako ni yapi ?
 
Yes we need to grow new talents, suali la msingi, imechukua miaka mingapi kumpata Mtu kama JPM ?
Watu wazuri tunao tena wazuri kuliko JPM. Wapo ndani ya CCM na wapo na upinzani, hata wewe mwenyewe Mk54 waonekana ni bora kuliko JPM kwa namna unavyowasilisha mada zako jukwaani . Tunachojitaji ni Rais anaye heshimu KATIBA alyoiapa.
 
Hata kwa ushauri hafai. Ametutenga sana kiitikadi, kikanda na kikabila. Ana utawala wa KIDIKTETA ambao siyo mzuri kuacha mwingine akaufuata

Fafanua Kikanda na Udikteta with facts and evidence support
 
Mheshimiwa Magufuli hana ukomo wa Uraisi,mpaka mbadilishe usemi wa kuwaita Maraisi waliopita kuwa ni Maraisi wastaafu,waitwe Maraisi waliomaliza muda wao kutokana na sheria iliyomo kwenye Katiba, sio wastaafu.
 
Watu wazuri tunao tena wazuri kuliko JPM. Wapo ndani ya CCM na wapo na upinzani, hata wewe mwenyewe Mk54 waonekana ni bora kuliko JPM kwa namna unavyowasilisha mada zako jukwaani . Tunachojitaji ni Rais anaye heshimu KATIBA alyoiapa.

Nina weza kuwa bora but Sio Mzalendo. Angalia aliyofanya JPM na pima kulinganisha na his predecessors
 
Fafanua Kikanda na Udikteta with facts and evidence support
Hili liko wazi na inakuwa, siwezi kupiteza muda. Kuna threads nyingi sana humu zinazoongelea Hilo.
 
Rais alishasema muda wake ukiisha anaondoka, hataongeza hata siku moja.

Kauli hubadilika. Refer kauli za Kagame. Nimeeleaza hapo Juu Kwenye siasa hakuna Bahati Mbaya Yaani HAKUNAGA;

Nashauri ujifunze ku pay attention [emoji3544]
 
Back
Top Bottom