Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Kwa namna Mambo yanavyoenda, viongozi wa CHADEMA wanazidi kukosa njia sahihi za kushughulika na maswala badala yake wanaendelea kuzidisha uanaharakati hata pale harakati zisipohitajika
Kwa watu makini wanafahamu kabisa jambo bora hutokana na fikra tulivu zisizo na purukushani wala marumbano
Kwa mazingira yaliyopo, hoja kuu ya CHADEMA wanataka katiba mpya ili wapate tume huru ya uchaguzi! (Japo yapo mengi lakini hili limeteka mijadala ya viongozi wao)
Sote tunafahamu kuwa katiba ndio msingi wa ujenzi wa Taifa bora! Fundi anapojenga msingi wa nyumba huku anapresha za hapa na pale kutoka kwa Boss wake, familia na njaa tumboni mwake hawezi kujenga msingi uliobora kubeba nyumba imara
CHADEMA wanatakiwa kutumia nafasi hii ya kudai katiba mpya bila vitisho kwa serikali ili waweze kupata faida ya kuwaunganisha wananchi wote bila kujali makundi yao ili wawe kitu kimoja
Mazingira ya Sasa sio yaliyokuwepo miezi kadhaa nyuma. Sasa hivi nchi ina utulivu na watu bado wanampima Rais aliyepo madarakani
Haiwezekani kwa miezi mitatu tu afute yale yooote yaliyoharibiwa na kiongozi aliyekuwepo! Angekuwa amejiuzulu au amepinduliwa hapo labda! Lakini kumbukeni aliyekuwepo amefariki! Anayeingia lazima atajaribu kulinda heshima ya marehemu kwa muda hata Kama alikuwa hakubaliana nae
CHADEMA wasitake kukurupuka katika hili halafu wakatuletea katiba mbovu kuliko iliyopo
Wanachotakiwa kufahamu, wananchi wote sio wanachama wa chama chao na wanapigania kitu kinachohusu wananchi wote. Jukumu lao kubwa ilitakiwa iwe kushawishi kwanza hasa hasa kidiplomasia kuliko kushurutisha
Baadhi ya wananchi wanaweza kuwaona CHADEMA kana kwamba wanapigania hiyo katiba zaidi kwa maslahi yao wenyewe kuliko maslahi ya nchi