Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
Kuna watanzania wanasema wanadanganywa? Wapi nioneshe
 
Ila swali la msingi ni kwa nini Zitto hakamatwi kwa uchochezi?

Naomba nisaidiwe hapo, huyu jamaa hajawahi kulala Polisi na wala hana hata kesi moja mahakamani.

Hiki ni kitengo.
Mkuu kwa hili naweza tofautiana na ww kidogo japo nipo neutral! Unakumbuka ile kamati ya bunge aliyoitwa aliwajibu nadhani majibu yale hadi leo bado kichwa kinawauma! Sasa kumkamata mtu wa namna hii lazima nawe uwe na hoja na si vioja! Hebu tuvute subira hii move mkuu atakubali matokeo kwa kukaa kimya au atajibu mashambulizi. Ila sisi waungwana huwa twasema 'anaekubali mapungufu ni jasiri'! 'Bwana yule' anaweza hii?
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
umejibu bila hata kusoma vizuri. unakimbilia wapi? Zito kasema kukopa sio dhambi, na kwa akili yako unafikiria kweli Zito hajui mfumo wa bajeti wa Serikali?
 
Asili ya watu wa kigoma;
  1. Wabishi sana (anaweza kuamua kubadili jina la migebuka na kuita mikongo) na akakubishia
  2. Ni wepesi kurubuniwa
  3. Si wa kuwaamini sana
ZZK ni moja ya watu wanafiki sana, nadhani sasa tusubiri mkono wa serikali uhusike naye, maana anachokitafuta anakijua mwenyewe, hakuna aliyebaki salama kubishana na UWT!

Pole sana ZZK, maana wanachama wanazidi kukukimbia na kibaya hata huko KGM huna lako, 2020 wananchi hawakupi kura, sasa sijui utafanyejej ewe mnafiki
Hebu jaribu kupangua hoja yake walau 1 tu sio hii mipasho
 
Maneno ya mkosaji. 2020 ni Zaidi ya 75% MAGUFULI TENA. Iringa, Mbeya, Arusha, Arumeru, Dar yote itakuwa mali ya CCM, kama unanielewa ninachomaanisha. Kiama chenu kinakuja na mtaishia kulia lia tu na ole mjifanye mnaleta fyokofyoko za kuandamana, sisi huwa hatujaribiwi.
Mtatia huruma kwakweli
Fikiri vzr Kabla hujaandika hii
Sanduku la Kura litakalosimamiwa na KAILIMA kweli unaamini ataondoka? hivi unajuwa kwanini dab haondolewi Dar
 
Kwanini mkuu wa KAYA aanze kuwatisha wanaotoa data? Bila shaka kuna ukweli juu ya hili
 
Anaandika kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe

Taarifa yetu kuhusu ' kupikwa ' Kwa takwimu za Pato la Taifa tutaitoa mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Act Wazalendo kitakachoketi 28/10/2017. Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali.

Tunatumia takwimu za Serikali kuonyesha kuwa Serikali inadanganya Kwa kutokusema ukweli wote wa uhalisia wa uchumi na kuporomoka Kwa mapato. Ni sawa na mtu anayesema Glasi ni ' half empty or half full ' kwani anasema kitu kile kile.

Kwa mfano, Rais anaposema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa Kwa kutumia ongezeko la kodi anakuwa anadanganya Wananchi na anafanya hivyo akijua anadanganya. Rais anajua kuwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa TZS 6.5trn katika miaka yake miwili ya urais. ( Deni la Nje limeongezeka Kwa US$1.5bn ( TZS 4.5trn) kati ya July 2016-July 2017. Deni la ndani limeongezeka Kwa TZS 2trn katika kipindi hicho.

Soma . http://www.bot.go.tz/Publications/MonthlyEconomicReviews/MER August 2017 Final.pdf ).

Pia Rais anajua kuwa Serikali inatumia, bila kufuata sheria, Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo Benki Kuu kulipia baadhi ya Miradi yake. Kukiuka sheria za Fedha ni kosa la jinai na wakati mwengine kosa la kikatiba kwani Katiba imeweka utaratibu wa masuala ya Fedha za Umma.

Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu. Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi Kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma.

Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA
Hii ishu iwekwe uwanjani ili kukata mzizi wa fitina ikibainika mtu kadanganya atolewe madarakani na miaka miwili atumikie taifa ili heshima irudi maana imekua tunafanyana mazombi sasa
 
Ni kwanini ccm mna tabia ya kujibu hoja bila kuweka data? Zitto kaja na data anazoziamini ambazo zinapinga data zilizotolewa na serikali, ni kwanini basi badala ya kutaja mlolongo wa miradi msiseme juu ya madeni ya nje na ndani mmeyalipa kwa kiwango gani kutokana na makusanyo yenu?
Kama kweli kwa uhalisia wa ukusanyaji mnaotamba kuwa nao lipeni madeni ya walimu na pensheni za wastaafu basi kwa kasi hiyohiyo ya ukusanyaji!
Hiyo miradi si ipo kibajeti au kuna ya dharura?
Zitto might be right kama majibu ndiyo yale ya jana!
Ccm wengi kichwani patupu
 
Hamjiulizi zile pesa tulizozuiwa kuchukua kwenye mifuko yetu zinaenda wapi.?? Nayo yanaitwa mapato
 
Jiandaeni kwa kuitwa kwa press conference nyingine Nyumba nyeupe kwa ajili ya kumjibu Zito
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza


Rais alisema miradi yote ya maendeleo ya ujenzi wa reli, ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara na mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme inatumia makusanyo ya pesa za ndani, na zipo za kutosha.
 
Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali.
Hivi Mh Rais anataka watu wazibwe midomo?
Hii sheria ipo?, ni kweli ni kwa ajili ya kuziba watu midomo.
Kama ilitungwa na Bunge na kuna makosa ambayo yanaangukia kwenye sheria hiyo, kwa nini isitumike?
Hivi ikitumika itakuwa ni kwa ajili ya kuwaziba watu midomo?
 
Back
Top Bottom