Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Kuhusu data: Zitto "ambishia" Rais Magufuli

Si wakati wa Kutishana unajua ukiwa na hoja hakuna atakayekutisha. Muhimu TRA na Gavana watolee ufafanuzi. MH Rais kutumia nafasi yake kupiga vijembe watu sio vizuri awaachie mawaziri, idara huzika wizara na nk, Yeye ni Mtu mkubwa sana kimadaraka apunguze vijembe vijembe akizoea hata kuwa tofauti na Gwajima kila mtu atakuwa na hamu ya kusikliza vijembe badala ya mambo ya maana tunayotaka kutoka kwake.
100% correctly..!
 
Ila swali la msingi ni kwa nini Zitto hakamatwi kwa uchochezi?

Naomba nisaidiwe hapo, huyu jamaa hajawahi kulala Polisi na wala hana hata kesi moja mahakamani.

Hiki ni kitengo.
Hata Slaa ni kitengo aliewasaliti Dakika za Mwisho

Hata Lissu ni kitengo kwa kupigwa risasi 38 kutokea upande wa kushoto lakin zikamapata Tano tu Tena Mguu a Kulia na Dereva hakupata walau mchubuko
 
kwa data zitto yuko vizuri kuliko jpm. kiukweli juzi jpm alipotosha kuhusu kodi na pesa za miradi ya maendeleo kama reli..n
Unataka niamin bei ya sukar ilikuwa 5000/- 2015 kisa amesema JPM!??
 
Zito hujui kuwa bajeti ya serikali mapato yake hutokana na makusanyo ya ndani na mapato ya Nje?

Kosa la rais kutekeleza kwa pesa za kukopa si kuvunja Sheria. Uchumi wa Nchi yetu bado haujafikia hatua ya kujitosheleza kulipia bajeti yote.
Kauli ya Mhe rais kuhusu kuongezeka kwa makusanyo ya ndani ni kweli acha kupotosha takwimu za serikali.
Naamini sasa umebaki unalia kama debe tupu huku ukidhani utaendelea kuwadanganya watanzania hutaweza
Tatizo LA mpenda sifa ni uongo mwingi na ZZK hapendi uongo. Mwambieni huyo muuza sura aache mipasho na mihemuko awe mkweli, ili awe mpenzi was Mungu!
 
Sisi tumeshachoka na haya mambo yenu tunasubiri 2020 tuu tumpige risasi kwenye sanduku la kura....imetosha kuongozwa na baba jesca...na kama ikitokea nchi inasajiri wananchi ntakwenda huko

Huna hiyo jeuri..hayo ni maneno ya mtu aliyelewa shisha.
 
Anaandika kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe

Taarifa yetu kuhusu ' kupikwa ' Kwa takwimu za Pato la Taifa tutaitoa mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Act Wazalendo kitakachoketi 28/10/2017. Sheria ya Takwimu aliyotaja Rais kutaka itumike kuziba watu midomo haizuii tafsiri za Takwimu zinazotolewa na Serikali.

Tunatumia takwimu za Serikali kuonyesha kuwa Serikali inadanganya Kwa kutokusema ukweli wote wa uhalisia wa uchumi na kuporomoka Kwa mapato. Ni sawa na mtu anayesema Glasi ni ' half empty or half full ' kwani anasema kitu kile kile.

Kwa mfano, Rais anaposema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa Kwa kutumia ongezeko la kodi anakuwa anadanganya Wananchi na anafanya hivyo akijua anadanganya. Rais anajua kuwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa TZS 6.5trn katika miaka yake miwili ya urais. ( Deni la Nje limeongezeka Kwa US$1.5bn ( TZS 4.5trn) kati ya July 2016-July 2017. Deni la ndani limeongezeka Kwa TZS 2trn katika kipindi hicho.

Soma . http://www.bot.go.tz/Publications/MonthlyEconomicReviews/MER August 2017 Final.pdf ).

Pia Rais anajua kuwa Serikali inatumia, bila kufuata sheria, Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo Benki Kuu kulipia baadhi ya Miradi yake. Kukiuka sheria za Fedha ni kosa la jinai na wakati mwengine kosa la kikatiba kwani Katiba imeweka utaratibu wa masuala ya Fedha za Umma.

Kodi inayokusanywa na TRA inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu. Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi Kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma.

Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA
Ni vyema tukasubiri taarifa ya Kamati Kuu ya ACT WAzalendo ya tarehe 28/10/2017!
 
Tunakoelekea ni kutokuamika kwa taarifa za kitakwimu zinazotolewa na NBS.
 
Zitto hayo yote inakuuma coz hujapewa kitengo serikalini kama ulidhani kuwa kimya ili uteuliwe UDC au URC umechemka utasubiri sana ww pambana na hali yako sio kuanza kuongea pumba uchumi umeshuka nyumbani kwako na sio serikalini
 
Vyama vya upinzani wanatumiaa luzuku vibaya!!nafikiri vinyimwe luzuku kwa sababu huwezi kuitisha kamati kuu ili tu mjibizane na rais !!this serious!!
 
Sisi tumeshachoka na haya mambo yenu tunasubiri 2020 tuu tumpige risasi kwenye sanduku la kura....imetosha kuongozwa na baba jesca...na kama ikitokea nchi inasajiri wananchi ntakwenda huko

Eti mmpige kwa kura !!!au yeye awapige mfe kifo cha mende!!!maana sijui kama mtakuwa na ajenda yoyote ile!!nendeni Kenya ndiko kuliko na democracy!! Hahahahhaaaaaa!!kule Kenya DREVA ya naibu jaji Mkuu kapigwa lisasi na watu waiyojulikana!!hiyo ndiyo democracy Kenya hahahahaaaa
 
Back
Top Bottom