Othman una kazi kweli, kama mnapoteza muda kufuatilia tunaosoma mkataba badala ya kuwafuatilia akina Balali wasituibie pesa zetu BOT?
Kutoka gazeti la Mwananchi.
Serikali yaonya wanaosambaza mkataba wa serikali wa Buzwagi
Na Ramadhan Semtawa
SIKU chache baada ya wapinzani kuugawa mkataba wa uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi kwa wananchi, serikali imeonya watakaokutwa nao watachukuliwa hatua kama watu wanaohatarisha Usalama wa Taifa.
Taarifa kutoka serikalini zilizofikia Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, zilisema mkataba huo ni siri kati ya serikali na Kampuni ya Barrick.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, serikali imekuwa kimya ikisubiri kuona watu watakaosambaza mkataba huo na watakaokukutwa nao, kwamba watachukuliwa kama waliokiuka Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970.
"Sheria ya Usalama wa Taifa inaeleza bayana, ingawa serikali ipo kwa ajili ya wananchi lakini si kila kitu ni kinachofanywa na serikali wanapaswa kuambiwa," zilisema taarifa kutoka ndani ya serikali.
Taarifa hizo za serikali zilifafanua kwamba, kusambaza mkataba huo kunaweza kuleta madhara kwa nchi na viongozi wa serikali ambao watakuwa wanahusika katika utiaji saini mkataba huo.
Onyo hilo la serikali limekuja wakati tayari, Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi, amekuwa katika wakati mgumu hasa anapojitokeza hadharani hasa katika mikutano na wananchi ambao huwa wanamwona kama asiyefaa.
Hata hivyo, alipoulizwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Casimila Kyuki ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, hakukanusha wala kuthibitisha badala yake, alisema kwa kifupi tu kwamba sheria ziko wazi na zinaeleza kila kitu kuhusu mikataba ya serikali.
Alipoulizwa vipi kuhusu kifungu cha 18 (d) cha Katiba cha Jamhuri ya Muungano kinachohusu haki ya kila mtu kupata taarifa ikiwemo zinahusu taifa, alijibu, "Msimamo wangu ni kwamba sheria ziko wazi, kumbuka uhuru unaishia pale unapoanza uhuru wa mwingine na kumbuka siyo kila taarifa za serikali zinapaswa kutolewa hadharani."
"Kwa mfano, huwezi kudai taarifa za namna gani jeshi la polisi linapambana na majambazi au uhalifu, serikali ipo kwa ajili ya wananchi na ndiyo maana inafanya mambo kwa ajili ya wananchi, lakini si taarifa zote zinatolewa," alisisitiza Kyuki ambaye pia ni Mwandishi Mkuu wa Sheria za Serikali.
Kyuki akikataa kuingia kwa undani, taarifa hizo kutoka serikalini zinaeleza hatua ya kusambazwa kwa mkataba huo inaweza kusababisha machafuko katika jamii na kuiathiri Kampuni ya Barrick.