Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
629
Othman una kazi kweli, kama mnapoteza muda kufuatilia tunaosoma mkataba badala ya kuwafuatilia akina Balali wasituibie pesa zetu BOT?

Kutoka gazeti la Mwananchi.

Serikali yaonya wanaosambaza mkataba wa serikali wa Buzwagi

Na Ramadhan Semtawa

SIKU chache baada ya wapinzani kuugawa mkataba wa uchimbaji madini katika mgodi wa Buzwagi kwa wananchi, serikali imeonya watakaokutwa nao watachukuliwa hatua kama watu wanaohatarisha Usalama wa Taifa.

Taarifa kutoka serikalini zilizofikia Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, zilisema mkataba huo ni siri kati ya serikali na Kampuni ya Barrick.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, serikali imekuwa kimya ikisubiri kuona watu watakaosambaza mkataba huo na watakaokukutwa nao, kwamba watachukuliwa kama waliokiuka Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970.

"Sheria ya Usalama wa Taifa inaeleza bayana, ingawa serikali ipo kwa ajili ya wananchi lakini si kila kitu ni kinachofanywa na serikali wanapaswa kuambiwa," zilisema taarifa kutoka ndani ya serikali.

Taarifa hizo za serikali zilifafanua kwamba, kusambaza mkataba huo kunaweza kuleta madhara kwa nchi na viongozi wa serikali ambao watakuwa wanahusika katika utiaji saini mkataba huo.

Onyo hilo la serikali limekuja wakati tayari, Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi, amekuwa katika wakati mgumu hasa anapojitokeza hadharani hasa katika mikutano na wananchi ambao huwa wanamwona kama asiyefaa.

Hata hivyo, alipoulizwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Casimila Kyuki ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, hakukanusha wala kuthibitisha badala yake, alisema kwa kifupi tu kwamba sheria ziko wazi na zinaeleza kila kitu kuhusu mikataba ya serikali.

Alipoulizwa vipi kuhusu kifungu cha 18 (d) cha Katiba cha Jamhuri ya Muungano kinachohusu haki ya kila mtu kupata taarifa ikiwemo zinahusu taifa, alijibu, "Msimamo wangu ni kwamba sheria ziko wazi, kumbuka uhuru unaishia pale unapoanza uhuru wa mwingine na kumbuka siyo kila taarifa za serikali zinapaswa kutolewa hadharani."

"Kwa mfano, huwezi kudai taarifa za namna gani jeshi la polisi linapambana na majambazi au uhalifu, serikali ipo kwa ajili ya wananchi na ndiyo maana inafanya mambo kwa ajili ya wananchi, lakini si taarifa zote zinatolewa," alisisitiza Kyuki ambaye pia ni Mwandishi Mkuu wa Sheria za Serikali.

Kyuki akikataa kuingia kwa undani, taarifa hizo kutoka serikalini zinaeleza hatua ya kusambazwa kwa mkataba huo inaweza kusababisha machafuko katika jamii na kuiathiri Kampuni ya Barrick.
 
Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Feb 16, 2007
980
42
Hivi sasa wanataka watu wajichukulie sheria mkononi,kama kweli mkataba ungekuwa na manufaa kwa wananchi pasingekuwa na tatizo ,lakini huu wanajua kabisa wametuuza ndio wanatafuta pa kukimbilia.kweli tanzania tunapelekwa kubaya na hawa viongozi tena tuliowachagua wenyewe.
 
Mwawado

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
995
241
Inakuwaje Mkataba huo unazagaa ktk kila kona Dar na hapa hatuuoni?.Waungwana mliopo Tanzania tunaomba aliye na mkataba huo atupitishie humu JF ili na sisi tuuone!.Natanguliza shukrani kwa yeyote atakayefanya assignment hiyo!.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,952
287,542
Mkataba upo wakuu, ila noma kwanza tuchungulie sharubu za simba! Halafu utawekwa hapa hapa JF tukufu!

Sharubu za Simba mwenda pole ambaye mambo yamemzidi kimo hajui hata pa kuanzia!...:) Si unakumbuka ile methali,"Simba mwenda pole iko gonjwa, kama si gonjwa basi iko ganisi (hanithi)."...LOL!
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,166
Wana JF
Nadhani nimeachwa kidogo. NIngependa kujua watanzania kuuona mkataba huu kunahatarisha vipi usalama wa taifa. Na ni kwanini uwe siri kati ya serikali na wawekezaji. Serikali na wawekezaji wana siri gani dhidi ya wananchi? Hii inaonesha kabisa kuwa there is something terrible going on againts wananchi.
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
608
Inakuwaje Mkataba huo unazagaa ktk kila kona Dar na hapa hatuuoni?.Waungwana mliopo Tanzania tunaomba aliye na mkataba huo atupitishie humu JF ili na sisi tuuone!.Natanguliza shukrani kwa yeyote atakayefanya assignment hiyo!.
_________________

Usemayo ni kweli, nadhani tatizo ni kwa "MAFUNDI MITAMBO" wa JF ambao wako Tanzania kuufuata na kuusambaza, naamini humu JF zaidi ya watu 10 ninaowafahamu wanao kwa hiyo ni kwao kuufuata na kuufanyia kazi bila WOGA WA SHARUBU WALA UTUMBO WA SIMBA kwani 'kamkataba' kenyewe kana kurasa 24 tu (aibu kama gazeti la UWAZI) na hakana kipengele cha USIRI kama mikataba mingine.

Wana JF
Nadhani nimeachwa kidogo. NIngependa kujua watanzania kuuona mkataba huu kunahatarisha vipi usalama wa taifa. Na ni kwanini uwe siri kati ya serikali na wawekezaji. Serikali na wawekezaji wana siri gani dhidi ya wananchi? Hii inaonesha kabisa kuwa there is something terrible going on againts wananchi.

Hapa nadhani si USALAMA WA TAIFA ni USALAMA WA KARAMAGI na Kundi lake wanaotafuta fedha za KUNUNUA URAHISI (URAIS) "HARAKA IWEZEKANAVYO" kama si 2010 au 2015 HAWA NDIO WANAOHATARISHA USALAMA WA TAIFA KWA KUPORA RASILIMALI YETU NA KWA KUTUFANYA TUENDELEE KUWA MASIKINI WA KUTUPA, HAWA NDIO WA KUSHUGHULIKIAWA NA USALAMA WA TAIFA KWA KUWABANA NA KUWAFUATILIA HISTORIA ZAO ZA MAISHA TOKEA WAKIWA CHUONI URUSI, KAZINI KULE WAZO HILL, HADI KATIKA MAKAMPUNI YAO NA UTAJIRI WAO WA KIAINA, HAPO USALAMA WA TAIFA WATAONEKANA KWELI WANAFANYA KAZI. USALAMA WA TAIFA WAANGALIE TAIFA LA WANAFUNZI WA UDSM WANAVYONYIMWA HAKI YAO YA KIKATIBA MAANA USALAMA WA TAIFA UNAANZIA KWA KUVUNJWA KWA KATIBA AMBAYO NDIO SHERIA MAMA SI MIKATABA YA WAWEKEZAJI KUWA JUU YA KATIBA....
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,037
3,439
Hivi sasa wanataka watu wajichukulie sheria mkononi,kama kweli mkataba ungekuwa na manufaa kwa wananchi pasingekuwa na tatizo ,lakini huu wanajua kabisa wametuuza ndio wanatafuta pa kukimbilia.kweli tanzania tunapelekwa kubaya na hawa viongozi tena tuliowachagua wenyewe.

Inakuwaje Mkataba huo unazagaa ktk kila kona Dar na hapa hatuuoni?.Waungwana mliopo Tanzania tunaomba aliye na mkataba huo atupitishie humu JF ili na sisi tuuone!.Natanguliza shukrani kwa yeyote atakayefanya assignment hiyo!.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom