Mbunge Bahati Ndingo Aiomba Serikali Kuwalipa Wazee Wastaafu wa NARCO Mbarali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
"Je, lini Serikali itawalipa mafao wastaafu wa shamba la Kapunga Wilayani Mbarali lililokuwa linamilikuwa na NARCO? - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Wakati wa ubinafsishaji kati ya mwaka 2003 na 2004 Serikali ililipa mafao ya wastaafu wote wa shamba la Kapunga isipokuwa mafao ya mkataba wa hali bora ambayo hujumuisha mishahara miwili baada ya Notes, gunia tatu za Mpunga kila mwaka waliyofanya kazi au fedha taslimu kwa bei ya wakati huo ilipofunga mkataba wa mwisho walipwe mshahara wa miezi minne kila mmoja kwa kila mwaka waliofanya kazi" - Mhe. David Silinde, Naibu Waziri wa Kilimo

"Madai ni ya muda mrefu takribani miaka 14 iliyopita na baadhi ya wanaodai taarifa zao hazijahakikiwa. Serikali inaendelea na uhakiki wa madai hayo ili kupata ufumbuzi kulingana na Sheria, Kanuni na Miongozo ya Serikali" - David Silinde, Naibu Waziri wa Kilimo

"Tathimini tayari imeshafanyika na barua imeshaenda Wizara ya Fedha na wazee wapo 65 na wanadai Serikali Shilingi Milioni 261. Naomba msimamo juu ya hili! - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Ni kweli tumepokea madai ya wazee wa Mbarali na maeneo mengine. Nimerichukua nitampa status ili kabla hajarudi awape taarifa wananchi wake" - Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Fedha.

maxresdefaultqaswer.jpg
1620896080895416-0.jpg
 
Hela za wazee mnazifanyia nini zinawapa laana
Mbarali mmewatapeli

SPM mgololo mmewatapeli

STAMICO Kyela mmewatapeli

Lipeni hela za wazeee acheni uhuni
 
Back
Top Bottom