VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Nipo hapa Arusha. Jana nami niliyashuhudia (lakini sikushiriki) maandamano ya amani ya CHADEMA katika viunga vya jiji la Arusha. Sikwami wala kuogopa kusema kuwa yalikuwa ni maandamano makubwa; washiriki walikuwa wamejipanga kila anga na yalipeperusha hoja za haja.
Kabla ya jana, nilioneshwa (na wahusika hasa) nyaraka za operesheni ya kuwaondoa/kuwahamisha Wamasai kutoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kuwapeleka wilayani Handeni mkoani Tanga. Nimeona kuwa hadi sasa, zaidi ya kaya/familia elfu moja zimeshahamishiwa Handeni.
Kwa mujibu wa nyaraka husika, kila kaya inayohamishiwa Handeni inapewa nyumba, shamba na pesa taslimu shilingi milioni kumi. Kimahesabu, hadi sasa kumeshatumika zaidi ya shilingi bilioni kumi ya pesa taslimu-achilia mbali zile za ujenzi wa nyumba na mashamba.
Nani anagharimia zoezi hili linalotumia mabilioni ya shilingi? Kama ni Serikali, bajeti ya zoezi hili imepangwa/imetengwa kwenye wizara gani na ni kwa bajeti ya mwaka upi wa fedha? Faida gani itakayopatikana, ikilinganishwa na hasara, kutokana na zoezi hili?
Sukari imekuwa hatari!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)