Kufuta namba ya simu ya marehemu inauma sana

20210219_182712.jpg

Sitosahau March 29, 2018 siku aliyoondoka kwa ajali iliyohusisha mabasi mawili na kupelekea vifo vya takribani watu 12 na yeye akiwemo (papo hapo alikatika miguu, mkono wa kulia na chuma kuingia jichoni).

Sisi wengine tuliumia vibaya na kuachiwa majeraha/makovu na ulemavu usiotarajiwa.

Lakini yote kwa yote tuliendelea kumshukuru Mungu, na kumwombea aendelee kupumzika mahala ambapo Bwana Mungu alimwandalia.

Imeniwia vigumu kuifuata hii namba yake mpaka leo 😪.
 
Siwezi kufuta no ya my wii, kila nikiiona nashindwa kuifuta. Queen ameniumiza mno.

Majuzi tu nimeota ananipigia simu akinambia mwezi wa 7 atakuja kuniona akitokea dar. Tena akasisitiza anataka akate ticket mapema kupunguza gharama. Alikuwa akicheka sana. Sauti yake ilikuwa ni ile ile dah Wakati namjibu ' wii kama unanidanganya nikashutuka usingizini. Ilikuwa mara ya kwanza namuota tangu afariki. Nyie watu udongo huu unakula watu wazuri sana.she was cute, classic, charming dah😭😭😭😭
 
Namba ya marehemu dada yangu nimeifuta mwaka jana.
Ni baada ya miaka mi4 kupita.

Kuna muda nilikuwa naiangalia na kujipa matumaini ya kusadikika kwamba itaita.

Siku naifuta nililia sana Sana.
Nililia mno.
Duuh pole mtumish i .yeah I can feel your pain Ile feeling ya kwamba hutamuona tena wala kumsikia sauti ameondoka mazima zinabaki memory tu
 
Hata Mimi na wewe hatutaishi milele je!,utakumbukwa kwa mema ...... I wish kungekuwa na jf uko tuendako tukatumie fake id kama hapa duniani maisha ni nini!,maisha ni sasa ,maisha ni fumbo,maisha ni safari ,maisha ni........!
Mwenyezi MUNGU tunakushukuru we we ni zaidi ya yeyote
 
Sijawahi futa namba ya mtu yoyote aliyefariki wala ku unfriend waliofariki ktk mitandao ya kijamii,sioni sababu,wazazi wamefariki namba zipo,wajomba,babu,marafiki wote sijawahi kufuta
 
Nililelewa na babu yangu 2019 alifariki, Nakumbuka alishawahi nambia una sura ya huruma sana acha basi kutia huruma wewe mwanaume nikacheka sana , ila ni mwaka sana siko nae kila nikipitia list ya majina nikifika herufi bi babu, natazama nairuka nikitaka kuifutaa naona kama nampoteza kama bado yupo naweza mcheki muda wowote,

..R..I..P.. babu yngu jemedali died with 95 yrs.
 
Sitakaa nisahau siku ambayo mshikaji wangu mmoja alipewa dili LA kwenda kuchukua watu moshi walioenda kwenye sendoff kuwarudisha arusha,mshikaji alipokuwa anafanya job kaachiwa funguo za magari tajiri na familia wamesafiri,mshikaji akatoka na Cruiser akaacha simu rehani kwa mlinzi Wa getini akapewa mshiko Wa mafuta kwa mkataba kuwa akirudi anarejesha hela anakomba simu yake.

Mshikaji akaenda moshi akawachukua RAIA,wakati wanarudi akala mzinga akaua watu kadhaa na yeye akafa pia.

Asubuhi mlinzi akakabidhi Lindo hakujua kama kuna Msiba akaenda home kwake,sisi tukapata taarifa kuwa mshikaji kachomoka na ajali.

Dah usiku kama SAA nane hivi siku ya pili mlinzi akapekuwa simu y marehemu akakuta no za watu ambao wanawasiliana na marehemu Mara kwa Mara si akaniichomoa,akanipigia kwa simu ya marehemu SAA mane usiku mana ilikuwa na hela ya kupiga.

SAA nane nasikia simu inaita nhriiii nkashtuka usingizini nkachukua simu niipokee dah kucheki marehemu ndo ananipigia sikumbuki simu ilifikaje sakafuni na ubabe wangu wote niliogopa hasa.
Nje ya mada ila nimekbuka hiki kisa.kilichosaidia alivyoona sipokei akatuma SMS hivi unahabari Fulani kafariki?.miaka zaidi ya kumi mpaka Leo Nina no yake,though haipatikani ila sijafuta bado.
 
Aisee, pole sana
 
Alikufa rafiki yetu,ilikua ngumu sana kuremove number yake ya simu kwenye group la whattsapp

Ilibidi ile siku kiongozi aseme kwanza ndugu tunaenda fanya tu maamuzi magumu

Ikasomeka “divain removed shose” ilikua uchungu ulirudi upya nikaanza kutoa machozi lakini ilikua haina namna

Maisha yaliendelea.
 
Umenipa uchungu sana , nimeshindwa kufuta namba ya Mzee wangu, Mungu naomba siku moja unikutanishe na Mzee wangu.
 
Back
Top Bottom