Kufuta namba ya simu ya marehemu inauma sana

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270
Awe mume, mke, mtoto, mzazi babu au bibi hata rafiki au mpenzi. Marehemu akisha kufa inauma sana kufuta namba zake za simu. Wakati ule wa simu za mezani za Shirika la Posta na Simu, jirani zetu walifiwa na mama yao ambae ndiye alikua na akaunti ya simu.

Walikaa miaka mingi wakilipa ankara kwa jina lile mpaka siku ilitokea matatizo, Posta walimuomba mwenye ankra aende ofisini. Baba alikwenda, alijibiwa tunamtaka mwenye jina. Aliwajibu kuwa mwenye jina ni mke wangu alifariki miaka mitano iliyopita.

Waliomba kuona cheti cha kifo na kujiridhisha, mzee aliambiwa ni kosa la jinai kuendelea kutumia jina la marehemu. Ilibidi jina la ankra kubadilishwa.
 
Awe mume, mke, mtoto, mzazi babu au bibi hata rafiki au mpenzi. Marehemu akisha kufa inauma sana kufuta namba zake za simu. Wakati ule wa simu za mezani za Shirika la Posta na Simu, jirani zetu walifiwa na mama yao ambae ndiye alikua na akaunti ya simu.

Walikaa miaka mingi wakilipa ankara kwa jina lile mpaka siku ilitokea matatizo, Posta walimuomba mwenye ankra aende ofisini. Baba alikwenda, alijibiwa tunamtaka mwenye jina. Aliwajibu kuwa mwenye jina ni mke wangu alifariki miaka mitano iliyopita.

Waliomba kuona cheti cha kifo na kujiridhisha, mzee aliambiwa ni kosa la jinsi kuendelea kutumia jina la marehemu. Ilibidi jina la ankra kubadilisha even.
Sana Mkuu wangu...Mungu atusaidie yaani
 
Kufuta unajiskia vibaya unaona kama unampotezea ama unajaribu kumfuta kicgwani marehemu
Kuiacha nayo ni kujiongezea machungu.

Nilibaki na namba za swahiba wangu na kaka yangu kwenye simu kwa miaka takribani miaka mi3 toka umauti wao uwafike.

Allah awasamehe madhambi yao, hakika nao ni waja si wakamilifu, kukosea ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, awapunguzie adhabu za kaburi.
Inauma saana, ni mara chache saana mwanaume kumwaga chozi, inatokea mara chache mnoo
kama umepitia hali hii unaelewa.
 
Namba ya marehemu dada yangu nimeifuta mwaka jana.
Ni baada ya miaka mi4 kupita.

Kuna muda nilikuwa naiangalia na kujipa matumaini ya kusadikika kwamba itaita.

Siku naifuta nililia sana Sana.
Nililia mno.
Alikuwa anapenda Sana kunipigia.

Namshukuru Mungu kwa yote.
Yeye atabaki kuwa Mungu na ninapata sana faraja maana waliokufa katika Bwana Yesu nitawaona tena kule juu.
 
Awe mume, mke, mtoto, mzazi babu au bibi hata rafiki au mpenzi. Marehemu akisha kufa inauma sana kufuta namba zake za simu. Wakati ule wa simu za mezani za Shirika la Posta na Simu, jirani zetu walifiwa na mama yao ambae ndiye alikua na akaunti ya simu.

Walikaa miaka mingi wakilipa ankara kwa jina lile mpaka siku ilitokea matatizo, Posta walimuomba mwenye ankra aende ofisini. Baba alikwenda, alijibiwa tunamtaka mwenye jina. Aliwajibu kuwa mwenye jina ni mke wangu alifariki miaka mitano iliyopita.

Waliomba kuona cheti cha kifo na kujiridhisha, mzee aliambiwa ni kosa la jinsi kuendelea kutumia jina la marehemu. Ilibidi jina la ankra kubadilisha even.
Kuna rafiki zangu wawili wa jinsia tofauti niliwahi kufanya nao kazi Iringa, wote walikufa mwaka 2017 na 2019.

Nilishindwa kuwa-unfriend katika list ya rafiki zangu wa Facebook. Kila nikitaka kufanya roho yangu inakataa katakata.
 
Nilimpoteza kaka yangu wa damu, ambaye pia alikuwa rafiki yangu mkubwa, nilibakia na namba yake kwa miaka kadhaa, na wakati mwingine nikawa napiga huwenda ikatokea muujiza akaipokea.

Yote kwa yote kifo ni fumbo, lazima tupite tuwaachie na wengine.

RIP
 
Inaumiza sana tena sana. Nilishindwa kuifuta. Baadae Vodacom wakaigawa kwa mtu mwingine.

Siku napiga ikapokelewa. Nilishtuka nikiamini karudi. Aliyepewa baadae nilimfanya rafiki. Hata jina bado nimem-save kama ambavyo lilikuwa awali. Sijaweza kubadilisha.

Najaribu kumkwepa kwepa ili baadae nae akipotea, nisimkumbuke tena Marehemu. Mungu atusaidie.
 
Ndiyo maana kuna sheria za mirathi na ndiyo maana watu wanazaliana. Namba za marehemu, kama zilivyo hazina na mali, virithishwe kwa damu changa. ^Kata wajihi uunge pua^ walisema Wahenga.
Sio kwamba umegeuza huo msemo "kata pua uunge wajihi"
 
Back
Top Bottom