Adaiwa kuuawa na jirani kisa kukuta namba kwenye simu ya mkewe, alimcharaza bakora jirani akajibu na panga

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
121
202
Mwita Kitamwi (55) mkazi wa Kitongoji cha Kegonga Kata ya Matare Wilaya ya Serengeti ameuawa kwa kukatwa shingo kwa panga na jirani yake aliyekuta namba yake kwenye simu ya mke wake.

Tukio hilo limetokea Machi 23 majira ya kati ya saa 11 hadi 12 jioni mwaka huu eneo la mtoni katika Kitongoji hicho limethibitishwa na uongozi wa Kitongoji na Polisi Wilayani hapa zinadai mtuhumiwa ambaye jina lake tunalo alitokomea na panga lake baada ya mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kegonga Joseph Mogoyo anasema, Kitamwi (marehemu) aliuawa kwa kukatwa na panga na jirani yake ambaye alilazimika kujibu mashambulizi baada ya kushambuliwa kwa fimbo na Kitamwi akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake.

“Kabla ya mauaji hayo Kitamwi (marehemu) alimpiga mke wake mkubwa baada ya kukuta namba ya huyo Jirani yake kwenye simu ya mke wake, hata hivyo huyo anayemtuhumu ndiye aliyeamulia ugomvi na kila mmoja akaenda kwake,” amesema Mwenyekiti.

“Baada ya muda alimfuata mtuhumiwa nyumbani kwake akitaka wapigane, watu wakawaamua na kurudi kwake. Jioni akitambua kuwa mtuhumiwa huwa anachemsha gongo mtoni alimfuata kazini kwake na alipofika akamcharaza fimbo mara mbili kichwani, ndipo akachomoa panga na kumkata shingo na kubakiza sehemu ndogo kichwa kitoke,” amebainisha.

Mwenyekiti huyo anadai mtuhumiwa alitokomea na panga lake huku mke wa mtuhumiwa aliyekuwa akisaidiana na mume wake kuchemsha gongo akipiga kelele na watu kukusanyika, juhudi za kumsaka mtuhumiwa zinaendelea kwa kushirikiana na Polisi.

Mmoja wa mashuhuda jina tunalo anadai kuwa, wakati mtuhumiwa anaamua ugomvi wa awali baada ya kumkuta Kitamwi ambaye ni marehemu kwa sasa akimpiga mke wake hakujua kuwa chanzo cha mgogoro huo ni yeye.

Jeshi la Polisi wilayani hapo wanadai wanamsaka mtuhumiwa na huku wakiitaka jamii kutoa ushirikiano.

Source: Serengeti Media Centre
 
Back
Top Bottom