Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Haya Ndiyo maamuzi ya kikao cha CCM (CC-Wiki iliyopita)
1.Kutohudhuria mdahalo na Dr.Slaa; Nape akamuwakilisha mtego ambao Dr.Slaa alishtuka naye akachomoa
2.Waziri Nchimbi wiki iliyopita alihamasisha wabunge hasa wa CCM na mawaziri kuperuzi mitandao ya kijamii kama JF ili kujua hisia za wananchi, na wanatumia fedha nyingi kuwalipa wanafunzi vyuoni ili wajiunge JF na hizo ID zao anazo Nape ili kufuatilia utendaji kazi wao post moja 7000/- kufifisha hoja.....ila imekuwa ngumu kuna madogo UDOM wamesema ''CCM hawajui mioyo yetu''
3.Kinana kumshurutisha Mch.Msigwa amuombe radhi kupitia mwanasheria wake....nadhani barua mmeiona humu JF.
4.Kushawishi wabunge wa CCM kumuongeze JK muda hadi 2017 .ili kuchakachuwa katiba kwani imeonekana wazee ndani ya CCM hawaaminiani so kuna sheria kandamizi zinaandaliwa kuuwa (assasination) wapinzani na kuwateuwa baadhi ya wapinzani serikalini (serikali ya umoja wa kitaifa) ili kupata Katiba mpya, Hili likipitishwa na viongozi wa upinzani wakikubali kufanya kazi na CCM nchi itakuwa mbaya sana kwa nchi.
5.Kuna tetesi kwamba Mjomba (JK) akapangua CC, kwani Mwigulu ni mzigo............,
Wenye Data zaidi tiririka.........., ila magamba dhibitini hasira na povu.

Asante sana kwa taarifa , kila sentensi itafuatiliwa ! Hakuna kudharau .
 
Hata mimi jana niliandika baada ya kuona hizi propaganda za huyo mtu wa propaganda wa CCM.

Sijui ni kwa nini Katibu mkuu wa CCM na Mwenyekiti wake Jakaya kikwete wanaogopa mdahalo na Dr.Slaa kiasi hiki.Leo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amemkimbia Dr.Slaa kama alivyofanya Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete wakati akiwa mgombea Urais Mwaka 2010 alipokimbia mdahalo kwa kumhofia Dr.Slaa.Taarifa za awali ni kwamba Kinana amehofia kuumbuliwa zaidi hadharani na Dr.Slaa kuhusu tuhuma zinazomkabili kuhusiana na nyara za Taifa ambazo ameshindwa kuzitolea majibu.Leo ITV waliwaalika makatibu wakuu wa vyama vya siasa kujadili hali ya kisiasa nchini.Dokta Slaa alikubali na kuitikia wito ila alipofika kwenye ofisi za ITV Kinana hakutokea na baadae akatokea Nape Nnauye-mpiga gitaa na mnenguaji kwenye mikutano yao ya hadhara (literally mistaken kama kATIBU WA ITIKADI NA UENEZI)bila kuzingatia itifaki.Dr.Slaa akataka itifaki izingatiwe akaamua kuondoka.Walialikwa makatibu wakuu na itifaki ilistahili kuwa hivyo


Wananchi wanajiuliza sasa ni chama gani hiki ambacho mwenyekiti na katibu mkuu wanaogopa mijadala kiasi hiki?.Rais kikwete (kwa kuhofia uwezo wake mdogo kama inavyojulikana sana)alikimbia mdahalo mwaka 2010 kwa kumuogopa Dr.Slaa,leo imekua zamu ya katibu mkuu Kinana.



Tujifunze kuzoea mijadala/midahalo(debate).This is the age in which you must be yourself na uwe tayari kwa public condemnation or appraisal and not otherwise.


Th

Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Hapo kwenye ' mpiga Gitaa ' umenikumbusha LOKASSA YA MBONGO !
 
pole sana VUVUZELA NAPE.Kwa taarifa yako ungekuwa na maadili tu ungekula sana mema ya hii nchi...Lakini kwa kuwa heshima na adabu vimekupita pembeni bado una mlima wa kupanda si kwa sisi vijana wenzako na marika mengine yote....Heshima hainunuliwi baba.Wewe na ujana wako nakuuliza SLAA NI BABU YAKO?!!.jifunze kuwa na adabu...KWA WAKUBWA ZAKO.

mwana mwenye heshima na adabu ni mzigo wa babaye lakini kama hayo ni mzigo wa mamaye....

nakushauri.

1.mtafute mama yako akufundishe adabu.
2.Siasa ni siasa na utu ni utu ,mpe heshima SLAA na siyo kumuita babu.
3.Fuata maadili ya kazi yako.
4.Kuwa na mipakaya kazi yako au wewe ndo kinana?
5.Epuka cheap popularity.
6.Jitathimini kisiasa.

Labda tu na mimi nijaribu kumuuliza Nape kwamba N Mandela aliongoza SA akiwa na umri gani au hata M Kibaki alishika wadhifa akiwa na umri gani! Je Kiongozi Mugabe! sisi hatuangalii umri tunaangalia uwezo wa kuongoza nchi na kwa sasa mimi Dr Slaa ndiye afaaye kupewa heshma ya kuliongoza taifa hata kama Nape atamwita babu! Lowasa nae kwa mbali anafaa ila mambo mawili anayopaswa kufanya ni;
atoke kwenye chama cha ccm na afafanue tuhuma zake kwa jamii ili ajisafishe.
 
Nanukuu
" Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya Tanzania Daima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la CHADEMA limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA"
nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!! "

Ungekaa kimya kwenye suala hili,ningekushangaa.
Asante kwa kutekeleza wajibu wako.
 
Nape ameshindwa kurithi busara za baba yake......Ungekuwa kama baba yako ungeheshimiwa sana ila kwa sasa naona unapuliza tu vuvuzela kila kukicha....ama kweli moto huzaa majivu

si niliwahi kusoma humu jf kuwa yule hakuwa mzazi? kama ni ukweli, basi tungemjua yule mzazi ili tulinganishe tabia. pengine kaichota huko
 
Sijawahi kusikia Nape anamuita JK "Handsome Dr. Kikwete" lakini nasikia "Babu Dr. Slaa"......how amazing!!
 
hawezi kutokea yule yupo busy kwanza kuna mzigo wa pembe za tembo unatakiwa kusafirishwa kwa hiyo lazima kwanza ahakikishe mzigo umeondoka salama ndio mambo mengine yafuatie.Maskini tembo wetu wanazidi kwisha hadi 2015 watabakia wa kwenye zooo tu.Kinena eehh samahani KINANA hawezi kusimama na mtu makini kama Slaa ataongea nini?
 
Hivi aliyefilisika kisiasa ndo nani kwenye hii stori? Hivi kweli Nape anaweza kumwambia mtu kuwa amefilisika kisiasa? Mhh, ama kweli waswahili walisema, nyani haoni kundule.
 
Mh Nape Nnauye, naomba unijibu maswali yangu sita niliyoandika ktk thread yangu yenye kichwa kisemacho MASWALI MUHIMU 6 KWA NAPE NNAUYE KWA MUSTAKABALI MWEMA WA NCHI YETU. Ni matumani yangu kwamba ombi langu limekubaliwa.
 
pole sana VUVUZELA NAPE.Kwa taarifa yako ungekuwa na maadili tu ungekula sana mema ya hii nchi...Lakini kwa kuwa heshima na adabu vimekupita pembeni bado una mlima wa kupanda si kwa sisi vijana wenzako na marika mengine yote....Heshima hainunuliwi baba.Wewe na ujana wako nakuuliza SLAA NI BABU YAKO?!!.jifunze kuwa na adabu...KWA WAKUBWA ZAKO.

mwana mwenye heshima na adabu ni mzigo wa babaye lakini kama hayo ni mzigo wa mamaye....

nakushauri.

1.mtafute mama yako akufundishe adabu.
2.Siasa ni siasa na utu ni utu ,mpe heshima SLAA na siyo kumuita babu.
3.Fuata maadili ya kazi yako.
4.Kuwa na mipakaya kazi yako au wewe ndo kinana?
5.Epuka cheap popularity.
6.Jitathimini kisiasa.

Huu ushauri uliompa Nape ni mzuri sana lakini inahitaji mtu mwenye uelewa mkubwa zaidi kuupokea. Nape anashindwa kujua kwa kuweka prefix za ajabu kwenye majina ya watu anajidhalilisha yeye kwa kuwa watu wanaona kiwango chake cha kufikiri ni kidogo na tana na hana maadili. Mtu aliyeko kwenye level ya uongozi ya Nape anatakiwa ajiheshimu. Kuna wakati aliwaambia wakazi wa mjii fulani kuwa wanashikishwa ukuta. I was shocked. Sasa huyu ni kiongozi wa namna gani? Hawa watu kama Nape wanapaswa kufahamu kuwa wanapokuwa wanaongea hawaongei tu na hadhira inayokuwa mbele yao bali wanaongea na taifa zima. Kwa kweli Nape hajafahamu vizuri nafasi aliyo nayo katika Chama. Anapenda sana mambo ya kijiweni huyu jamaa. Kwani hana watu wazima wa kumshauri? Even the way he portrays himself on the tele, it leaves a lot to be desired. Nape, it is high time you changed your behaviour.
:iamwithstupid:
 
Nape kijana unaweza kujiuliza kwa nini vijana wenzio hawakupendi kiasi hiki ?Mbona kuna wenzako kama January ni Ma CCM lakini wanaeleweka kwa vijana wenzao wa vyama vyote umeshawahi kujiuliza au ndiyo ulevi wa madaraka ?
 
Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la CHADEMA la Tanzania Daima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu.

Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya Tanzania Daima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la CHADEMA limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la CHADEMA leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda.

WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

================================
Habari kamili toka Tanzania Daima
================================

Nukuu zangu

Ndugu yangu Nape, Huyo Tandale one nadhani inafahamika yuko mrengo gani na taarifa anayoitoa inaweza ikaonyesha inaelekea wapi (Ukweli au Upotoshaji au kejeli)

Nilitegemea kuona kitu kuhusiana na aidha kukanusha au kukubaliana na taarifa uliyoitoa wewe wakati ukihojiwa kwa simu na Mwandishi wa Tanzania Daima.

Siku zote Chombo cha habari hupata wafuasi wengi kutokana na taarifa zake kinazozitoa. Hilo gazeti unalosema ni la CHADEMA (Binafsi sijui umiliki wake ukoje)ukilinganishana Uhuru ambalo ni la serikali, wasomaji wengi wa habari wanakimbilia Tanzania Daima kwa kuwa walau linajitahiki kuchanganya Taarifa. Chukulia mfano wa Mchakato wa kesi ya Ugaidi iliyokuwa inamhusu Lwakatare gazeti hilo liliendelea kuandika inn and outside bila kujali, Pia taarifa zinazoihusu Serikali ziwe nzuri za kiutendaji au zenye makosa. Lakini gazeti letu la serikali kila siku lina taarifa za kusifia serikali na viongozi wa chama hata kama kuna makosa "Kwa staili hiyo linapoteza sifa za kuvutia wasomaji". Tokea Lifungiwe Gazeti la Mwanahalisi wasomaji wengi wamepata mbadala kwa kuhamia haswa Tanzania Daima na Mtanzania. Hata katika TV TBC toka alivyoiweka sawa Mhando kidogo ilianza kuvutia wananchi kuitizama lakini kwa sasa inakoelekea nako sio kuzuri, na hiyo yote inasababishwa na kutoa taarifa kwa kuchagua.


Ndugu yangu mdahalo huo, wahusika waliitwa kwa vyeo vyao. Pamoja na kuwa wewe ni mwenezi sidhani kama ilikuwa sahihi sana kwenda kumuwakilisha.

Nimalizie kwa kukueleza kuwa kwa sasa watanzania wameinuka na wanafuatilia taarifa kuliko hata unavyoweza kudhani. Ni vizuri Chama kikapunguza matumizi ya mababu kwa kisingizio cha kuvuruga amani kwa kuvibana vyama vya upinzani kwani kufanya hivyo ndio kukiua kabisa badala ya kukiamsha. Tunapenda kukiona chama chetu kikionyesha kuongoza kwa Demokrasia. Ni aibu sana kusikia eti DC na DED wanaenda kumkabidhi mwenyekiti wa kijiji uongozi katika kituo cha polisi kwa kuwa hakubaliki kwa wananchi.
Kweli kwa sasa Mnatutisha wanachama wa CCM kutembea vifua mbele kwani taharuki zilizopo humu mitaani hazifai kutokana na chama/Serikali kushindwa kujing'atua na baadhi ya wale wenye kukipaka matope kiutendaji wakiwemo viongozi wa serikali wanaoishia kuhamishwa kila kukicha.

Wananchi wanapenda kuona kazi zinazofanyika na sio kazi zinazosemwa zitafanyika.




 
mkuu mwaka huu utamkoti nape mpaka basi hata ukiwa usingizini kumbe anawatesa sana,kweli siasa ngumu.

mkuu mwaka huu utano quote mpaka basi hata ukiwa usingizini kumbe ninawatesa sana Vijana wa Lumumba ,kweli siasa ngumu sana Upande wenu.
Na Bado
 
Dr. Slaa kwa sasa yuko DESPERATE kupewa Urais. Anafahamu kuwa, kama hataupata Urais 2015 basi hiyo itakula kwake kwa sababu atakuwa na miaka 67. Legally kwa sasa ni PENSIONER. Come 2020 atakuwa na miaka 72.

Kwa sasa mpaka anajaza watu kwenye mitandao kuleta uongo ambao hata hivyo unawafaa watoto wa chekechea. Mara, kapigiwa mizinga na Rais wa Zambia, mara, ooh, Nilikuwa nataka kufanyiziwa kwa ajari ya gari ya kutengeneza , mara, ooh, Ninafuatiliwa barabarani. Ilimradi vulugu tupu.

Toka uchaguzi wa 2010 ulipoisha, amekuwa akifanya kampeni za Urais karibia kila siku. Swali la MSINGI ambalo watu ingekuwa vizuri wakajiuliza, WHY HE IS SO DESPERATE TO BE THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.
Kwani kuna sehemu imetangazwa nafasi za kazi ya urais?
 
Mawazo ya KIBAVICHA BAVICHA. Hiki kitengo ni janga la chama na kikubwa zaidi ni janga la kizazi kijacho.
Unajua inabidi serikali itoe chanjo kwa vijana wetu ili hili gonjwa hatari liitwalo bavicha lisije kuwasumbua.

Nina wasi wasi baada ya 2015 wengi wanweza ku-commit suicide baada ya matokeo ya uchaguzi kwani itakuwa ndio mwisho wa ndoto zao na tayari wameishapoteza muda na hela zao kuwachangia makamanda wao
 
Unajua inabidi serikali itoe chanjo kwa vijana wetu ili hili gonjwa hatari liitwalo bavicha lisije kuwasumbua.

Nina wasi wasi baada ya 2015 wengi wanweza ku-commit suicide baada ya matokeo ya uchaguzi kwani itakuwa ndio mwisho wa ndoto zao na tayari wameishapoteza muda na hela zao kuwachangia makamanda wao
Kama hii ni LIMBWATA basi hii ni kali. Hata kondoo wakati mwingine huwa wanakaidi amri ya mchungani wao. Kwa hawa vijana hakuna jingine bali ni EMPTY HEAD. Jana walikuja eti na uzi unaosema Dr. Slaa alipigiwa 'MIZINGA' na Rais wa Zambia. Wanaonyesha ujinga wao wakifikiria ni wajanja. Dr. Slaa amewajaza kwenye mitandao bila hata kuwafanyia INDUCT INTERVIEW matokeo yake, wengi wanapost madudu hapa JF. Hili ni janga la Taifa.
 
Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda.

BOSI WAKO MBONA KAMA ANAKUKATAA KIAINA
 
SIASA ZA MAJITAKA ZA CDM NA KUTAFUTA CHEAP POPURALITY ZITAWAMALIZA.
Kwenye hili hauitaji kuwa na degree kugundua ushakunaku wa cdm na mafuasi wake makanjanja.
Hivi inakuaje katibu mkuu wa ccm anatoa udhuru na kumtuma muakilishi wake na halafu mnadai kamkimbia.
Hivi mwenye akili nzima anaitaji kuelezewa jinsi hawa watu wawili wasivyolingana kiuelewa?
Dr mtu asiejiweze hata kujenga hoja inakuaje unataka kumuweka na Kanari na katibu mkuu wa ccm?
Huu ni upuuzi ambao atauamini mjinga na sio mtu anaeweza kuchambua mambo.
Poor cdm.
 
Back
Top Bottom