Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Haya Ndiyo maamuzi ya kikao cha CCM (CC-Wiki iliyopita)
1.Kutohudhuria mdahalo na Dr.Slaa; Nape akamuwakilisha mtego ambao Dr.Slaa alishtuka naye akachomoa
2.Waziri Nchimbi wiki iliyopita alihamasisha wabunge hasa wa CCM na mawaziri kuperuzi mitandao ya kijamii kama JF ili kujua hisia za wananchi, na wanatumia fedha nyingi kuwalipa wanafunzi vyuoni ili wajiunge JF na hizo ID zao anazo Nape ili kufuatilia utendaji kazi wao post moja 7000/- kufifisha hoja.....ila imekuwa ngumu kuna madogo UDOM wamesema ''CCM hawajui mioyo yetu''
3.Kinana kumshurutisha Mch.Msigwa amuombe radhi kupitia mwanasheria wake....nadhani barua mmeiona humu JF.
4.Kushawishi wabunge wa CCM kumuongeze JK muda hadi 2017 .ili kuchakachuwa katiba kwani imeonekana wazee ndani ya CCM hawaaminiani so kuna sheria kandamizi zinaandaliwa kuuwa (assasination) wapinzani na kuwateuwa baadhi ya wapinzani serikalini (serikali ya umoja wa kitaifa) ili kupata Katiba mpya, Hili likipitishwa na viongozi wa upinzani wakikubali kufanya kazi na CCM nchi itakuwa mbaya sana kwa nchi.
5.Kuna tetesi kwamba Mjomba (JK) akapangua CC, kwani Mwigulu ni mzigo............,
Wenye Data zaidi tiririka.........., ila magamba dhibitini hasira na povu.
 
Jana kuna topic ilitumbukizwa humu 'Dr slaa amkimbia Nape' mbona hukusema, au kwasababu tittle hiyo haikupewa uzito na kuandikwa Uhuru.Naskia uliwaomba waweke title hii uson mwa gazeti la Uhuru wakakukatalia
 
Nape ameshindwa kurithi busara za baba yake......Ungekuwa kama baba yako ungeheshimiwa sana ila kwa sasa naona unapuliza tu vuvuzela kila kukicha....ama kweli moto huzaa majivu
...Baba yake yupi? Huoni anavyohangaika kutafuta undugu kwa Dr Slaa? unajua kwa nini anamuita Babu?
 
Hata mimi jana niliandika baada ya kuona hizi propaganda za huyo mtu wa propaganda wa CCM.

Sijui ni kwa nini Katibu mkuu wa CCM na Mwenyekiti wake Jakaya kikwete wanaogopa mdahalo na Dr.Slaa kiasi hiki.Leo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amemkimbia Dr.Slaa kama alivyofanya Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete wakati akiwa mgombea Urais Mwaka 2010 alipokimbia mdahalo kwa kumhofia Dr.Slaa.Taarifa za awali ni kwamba Kinana amehofia kuumbuliwa zaidi hadharani na Dr.Slaa kuhusu tuhuma zinazomkabili kuhusiana na nyara za Taifa ambazo ameshindwa kuzitolea majibu.Leo ITV waliwaalika makatibu wakuu wa vyama vya siasa kujadili hali ya kisiasa nchini.Dokta Slaa alikubali na kuitikia wito ila alipofika kwenye ofisi za ITV Kinana hakutokea na baadae akatokea Nape Nnauye-mpiga gitaa na mnenguaji kwenye mikutano yao ya hadhara (literally mistaken kama kATIBU WA ITIKADI NA UENEZI)bila kuzingatia itifaki.Dr.Slaa akataka itifaki izingatiwe akaamua kuondoka.Walialikwa makatibu wakuu na itifaki ilistahili kuwa hivyo


Wananchi wanajiuliza sasa ni chama gani hiki ambacho mwenyekiti na katibu mkuu wanaogopa mijadala kiasi hiki?.Rais kikwete (kwa kuhofia uwezo wake mdogo kama inavyojulikana sana)alikimbia mdahalo mwaka 2010 kwa kumuogopa Dr.Slaa,leo imekua zamu ya katibu mkuu Kinana.



Tujifunze kuzoea mijadala/midahalo(debate).This is the age in which you must be yourself na uwe tayari kwa public condemnation or appraisal and not otherwise.


Th
 
By Nape Nnauye Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la Chadema la TanzaniaDaima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu.

Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya TanzaniaDaima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la Chadema limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la Chadema leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda.

WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.
Hivi ndivyo hali ilivyo kwa sasa.

hivi haya ni mapenzi kwa cdm/Dr. Slaa au ni chuki!?
Na ni taasisi gani unayoifanyia uenezi kati ya cdm na ccm, maana umeitaja ccm mara moja tu!!

Mkuu; majibu yako hapa.Huu utafiti ulifanyika kweli si masikhara!
A simple Research: Viongozi wa CCM wanaihubiri CHADEMA kuliko chama chao!
 
Mwandiko wa Nnape Mwandosya na TandaleOne unafanana sana.
 
wewe ukitaka kutoelewana na CCM we andaa mdalao na CDM, wanatoka nduki hao na visingizio kibao.
 
Hamocha😛amoja na sintofahamu ya historia yako,bado mm naamini wewe ni "mnyampaa".Viti yule mla fisi(mnyiramba,mtani) yupo au kapeleka ushahidi mbinguni? msalimie

Ayu mnyampaa,huyu Nape na Mwigulu ni kabila moja,Nape ni mnyiramba kwa mama aliyemlea peke yake,jina lake pia ni la kinyiramba ingawa \melifupisha kwani hataki watu wafahamu,anaitwa Napegwa (maana yake "nimepewa"Jina hili hutajwa baada ya mtu kukosa mtoto kwa muda mrefu hivyo kuelezea shukrani kwa Mungu kuwa Nimeoewa na Mungu!
 
Mkuu huna haja ya kujisumbua na hizo street rags.
Wanahabari hapo hawako objective, wangekuwa ni wa maana wangemshauri Dr Slaa aendelee kugombea urais ili ajijue umaarufu wake!

Nimewahi mimi mwenyewe kumpigia simu mhariri wa habari gazetini hapo ili arekebishe habari fulani iliyokuwa factually wrong, nikaishia kuambiwa eti mimi ni mtu wa usalama nawafuatilia nini!!!!

Nilishangaa sana wahriri wasiotaka kukosolewa, wasijue kuwa hata sisi ni wadau wakubwa wa habari.
Sasa watu wenye mind set ya aina hiyo wanaishia kuandika habari za kupika na kuelekezwa na wanao watumia.
 
Nape, kwani wewe usingependelea CHADEMA wafilisike kisiasa? Ushauri wangu wa bure kwako ni huu: wewe (na wenzako ndani ya ccm) waache CHADEMA waendelee na hayo wanayoyafanya - maana watazidi kufilisika kisiasa - na nyie muendelee kufanya mnayoyafanya. Au huoni kwa wewe na vijana wako kuendelea kuwasema hapa na kwingineko mtakuwa mnawagutusha?
 
Mheshimiwa sana Nape, Katibu mwenezi wetu.

Kwa kuwa kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, Kwa heshima na taadhima naomba utoe kauli hapa:


  1. Kwanini kila mara Unaliita jina la Dr. Slaa kwa ku-prefix "Babu"? (kwa sababu imekuwa ni kawaida yako na huwezi kukana hili) Ni babu kivipi?
  2. Unatoa maoni gani kwa wale wote ambao pia wameamua ku-prefix jina la Dr.Slaa kwa kama "Padre" Yaani kila wakitaka kutaja jina hili husema "Padre Slaa"> Hii ilianza rasmi wakati alipogombea urais wa JMT 2010. Je unavyoona wewe kauli hii ya kumwita "Padre" wakati yeye mwenyewe hakutaka aitwe hivyo (rejea majina rasmi aliyotumia wakati wa kujiandikisha kama mgombea na mpigakura) ililenga nini? (reflect your answers on the context of what is going on now in our lovely country)
  3. Kwa usawa huohuo basi, ni sahihi pia (hata wewe unaweza) kumwita mtu mwingine kama Dr. Jakaya Mrisho kikwete, Hon Peter Pinda au Wassira kwa Prefixes kama hizo hata kama wenyewe hawajiiti hivyo? Hint: Wassira alizaliwa 1945, anamzidi Slaa kwa miaka mitatu, Slaa anamzidi J.K miaka miwili tu, (ages:Wassira 68, Dr. Slaa ana 65 and JK ana 62) Hon. Pinda alizaliwa August 12, 1948, Dr. Slaa alizaliwa October 29, 1948. (source: Bunge website and other sources) Hivyo Wassira na pinda wamemzidi siku za umri Slaa. Kama kumwita mtu babu ni heshima, na Umri wa miaka >65 ndio base year yako kuita mtu kwa heshima ya "Babu", Je unataka tuelewe kuwa huna heshima kwa Wassira na Pinda kama unavyomheshimu Dr. Slaa?

Majibu tafadhali...

Hawezi jibu kwasababu anamkejeli Dr. Slaa kwa kumuita 'babu'. Malezi mabovu kwa waliomlea!
 
Acha kuzunguka hata bwana Nape anakuona mzushi jibu hili kutoka kwa Nape!

"Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile"


Nyote wanafiki tu!!!!

Mkuu MTAZAMO,huyo tandale one ndiye huyohuyo Nape!
 
Amealikwa kinana unaenda wewe vuvuzela,inaonekana unapenda sana kudowea
 
....... nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

bwahaaaaa.hahahahahah...mr itikadi na uenezi!!!!....bora hata sinema ya yomba yomba. Ninaamini wakati wa sinema hii ulikuwa hata hujazaliwa.
 
"kufilisika kisiasa kwa nape nnauye kunatisha"
 
Back
Top Bottom