Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Tatizo Chadema wanashindwa kukubali ukweli

CCM walimheshimu sana Slaa kumpeleka Nape kuongea naye.

Chadema ni sawa na kibajaji na CCM ni sawa na treni kwa hiyo huwezi kufananisha dereva wa bajaji na wa treni hata siku moja.

Dereva wa treni ana majukumu mengi sana kuhakikisha mabehewa yote bado yako relini na abiria zaidi ya milioni arobaini wako salama wakati huyu dereva wa bajaji abiria wake wako nyuma yake tu hapo na ni wachache tu na wanafahamiana na kibajaji chenyewe kina magurudumu matatu tu ambayo anayaona kila wakati sasa iweje leo Slaa kwa sababu ni dereva wa kibajaji apewe hadhi sawa na kinanan dereva wa treni?

JITAMBUE!
 
Nape Nnauye I expected you to explain what happened na sio kulalamika, mwandishi kafanya kazi yake,Dr kaeleza yake na wewe eleza unachokiona hakijawekwa sawa sisi ndo tutajaji nani mkweli, mpaka sasa naona Dr ndo kaeleza kwa kina his side of story....
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa sana Nape, Katibu mwenezi wetu.

Kwa kuwa kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, Kwa heshima na taadhima naomba utoe kauli hapa:


  1. Kwanini kila mara Unaliita jina la Dr. Slaa kwa ku-prefix "Babu"? (kwa sababu imekuwa ni kawaida yako na huwezi kukana hili) Ni babu kivipi?
  2. Unatoa maoni gani kwa wale wote ambao pia wameamua ku-prefix jina la Dr.Slaa kwa kama "Padre" Yaani kila wakitaka kutaja jina hili husema "Padre Slaa"> Hii ilianza rasmi wakati alipogombea urais wa JMT 2010. Je unavyoona wewe kauli hii ya kumwita "Padre" wakati yeye mwenyewe hakutaka aitwe hivyo (rejea majina rasmi aliyotumia wakati wa kujiandikisha kama mgombea na mpigakura) ililenga nini? (reflect your answers on the context of what is going on now in our lovely country)
  3. Kwa usawa huohuo basi, ni sahihi pia (hata wewe unaweza) kumwita mtu mwingine kama Dr. Jakaya Mrisho kikwete, Hon Peter Pinda au Wassira kwa Prefixes kama hizo hata kama wenyewe hawajiiti hivyo? Hint: Wassira alizaliwa 1945, anamzidi Slaa kwa miaka mitatu, Slaa anamzidi J.K miaka miwili tu, (ages:Wassira 68, Dr. Slaa ana 65 and JK ana 62) Hon. Pinda alizaliwa August 12, 1948, Dr. Slaa alizaliwa October 29, 1948. (source: Bunge website and other sources) Hivyo Wassira na pinda wamemzidi siku za umri Slaa. Kama kumwita mtu babu ni heshima, na Umri wa miaka >65 ndio base year yako kuita mtu kwa heshima ya "Babu", Je unataka tuelewe kuwa huna heshima kwa Wassira na Pinda kama unavyomheshimu Dr. Slaa?

Majibu tafadhali...
 
Nape Nnauye hatuoni anachokifanya.ingekuwa nafasi hiyo inapigiwa kura tungeshamtema long time.
 
Chezea slaa yeye alimtaka Mwizi wa Tembo ili atueleze kwanini anatuibia Tembo wetu alivyosikia Kasepa akaona hakuna haja
 
Sarakasi zetuuuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kama ungekuwa na babu kama Dr Slaa naamini hata hekima na busara yako ingejieleza yenyewe ila malezi ya asubuhi hadi jioni kwenye vikao yamechangia uwe kama hivi.
 
Tatizo Chadema wanashindwa kukubali ukweli

CCM walimheshimu sana Slaa kumpeleka Nape kuongea naye.

Chadema ni sawa na kibajaji na CCM ni sawa na treni kwa hiyo huwezi kufananisha dereva wa bajaji na wa treni hata siku moja.

Dereva wa treni ana majukumu mengi sana kuhakikisha mabehewa yote bado yako relini na abiria zaidi ya milioni arobaini wako salama wakati huyu dereva wa bajaji abiria wake wako nyuma yake tu hapo na ni wachache tu na wanafahamiana na kibajaji chenyewe kina magurudumu matatu tu ambayo anayaona kila wakati sasa iweje leo Slaa kwa sababu ni dereva wa kibajaji apewe hadhi sawa na kinanan dereva wa treni?

JITAMBUE!

Mzee wa pumba, endelea kujikomba unaweza pewa ubunge wa kupendelewa 2015
 
hivi kuna mtu anasomaga Tanzania Daima kweli??
 
Dah ! Nimeamini siasa si Mchezo ! Yaani huyu aliyeandika haya ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama ? Hata haieleweki alikuwa anamaanisha nini ! Haieleweki analalamika, anatoa maelezo , anasikitika au anajuta !
Tena wa chama kinachotawala. No wonder we, as a nation, are stuck.
 
Nape ameshindwa kurithi busara za baba yake......Ungekuwa kama baba yako ungeheshimiwa sana ila kwa sasa naona unapuliza tu vuvuzela kila kukicha....ama kweli moto huzaa majivu

acha uzushi wewe unamjua babake nape?? Niambie wapi alipo na uko unaomyambua nape ni upi??
 
Mbona watanzania mnakuwa na akili kama za samaki!!?? (Karume Jnr 2012)

Naomba tuweke rekodi sahihi, Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alimkimbia Dr. Slaa kufanya naye mdahalo wa wazi wakati wa kampeini 2010. Huu ni Ukweli hata MUWEKE SIASA VIPI HUWEZI KUFUTIKA. Katibu Mkuu wa CCM wakati huo Yussuf Mkamba akaenda mbali zaidi kwa kuwazuia wagombea wa nafasi mbali mbali wa CCM kushiriki Midahalo ya wazi baada ya mgombea UBUNGE wa CCM Hawa Ngh'umbi KUTOKA kwa JJ Mnyika Mgombea wa CDM Ubungo. HUU NI UKWELI AMBAO HATA MUWEKE SIASA HAUWEZI KUTENGULIWA.

Tanzania imeingia tena kwenye kitabu cha WORLD GUINESS OF RECORDS, ambapo Watanzania walimchagua mgombea URAIS aliyekimbia midahalo ya wazi Mhe. JAKAYA MRISHO KIKWETE. Haya ni maajabu mengine ya dunia. I can BET MY NECK kama Barack Obama angemkimbia Mity Romney, make no mistake leo asingekuwa RAIS wa USA. Hata Wakenya wametuzidi kama Uhuru Kenyatta angemkimbia Raila Odinga kufanya naye midahalo, I tell you leo asingekuwa RAIS wa Kenya. Lakini mambo yote yasiyowezekana duniani kote Tanzania yanawezakana. Tunaye RAIS aliyekimbia midahalo ya Wazi na wagombea wengine. Huu ulikuwa ni UDHAIFU mkubwa kwa Kikwete na kama zingekuwa nchi MAKINI za wenzetu angeishia kupata kura za familia yake na CC ya CCM. Sio kura za watanzania MAKINI.

Sasa kama M/Kiti wako Nape alimuogopa Dr. Slaa na kumkimbia leo akisikia kwamba wewe unamumudu Dr. Slaa na humuogopi kama yeye (M/kiti) wako, hivi atachukulia vipi hayo majivuno yako? Yaani wewe una uwezo zaidi ya M/kiti wako? na Kwamba M/kiti wako ni kilaza/hajiamini ndiyo maana alimuogopa Dr. Slaa. Nape uwe unapima kauli zako zinaweza kukurudia wewe mwenyewe na kukuingiza matatani.

NI ushauri wa bure unaweza kuuchukua au kuuacha.
 
Mbona Nape anashindwa kujibu hoja.Mimi nasikitishwa na kauli za Nape lazima ziwe na kejeri, kwa sisi wasomi mtu hata kama humpendi vipi lazima uheshimu elimu yaka.Kama ni Dr utamuita Dr kama ni professor Utamuita ivyo.Kwa kauli kama hizo za Nape mimi napata mashaka na vyeo mnavyopewa.Nikiangalia naona ni siasa za chuki tu.
Nape hajaenda shule huyo ni alshaababu ya kisiasa
 
Nape for real hufaham siasa,sijawahi kukukubali hata siku moja,naona unajitekenya na kucheka mwenyewe..ID ya Tandaleone ni wewe na usilete siasa za ujangili humu.Hamuwezi kuifitinisha chadema na sisi wenye nchi kwa bei rahisi kipropaganda..HIYO NAFASI ULONAYO imekupwaya.
nape komaa ni wakati wa vijana huyo mzee asikutishe keshaisha hana jipya؛
 
Ni kwanini mtunawe (1) na ujasiri kusema uwongo (2) ambao dakika ya pili, utaonekana dhahiri ni uwongo (3). Ni kielelezo cha jinsi Taifa letu lilivyozama kwenye Tope (4) nene.

1) kwanza noisome(5) kuwa ninkweli(6) tukio lilikuwepo. Majira ya saa 3.00 asubuhi, muda uliopangwa nilikuwa kwenye Gate la ITV, na kupokelewa na Mwandishi na mratibu(7) wa Program hiyo. Nyuma yangu likawa linaingia Gari(8). Alitelemka(9) Nape, nikadhani amemsindikiza Katibu Mkuu wake, Mhe. kinana(10). Tukasalimiana kwa kishikana mikono, na kutaniana kidogo.

2. Ndipo nikamwuliza(11) Boss wake yuko wapi, ndipo akanijibu kuwa amemtums(12) yeye. Nikauliza, mbona sikujulishwa, kwa kuwa ningelijua, ningemtuma afisa(13) wangu, size ya Nape. Nape alikubaliana nami.(14) Nikamwambia basi, kipindi hakitawezekana, na Nape na Mwandishi wote wakakubaliana nami.(15) Kipindi kikaahirishwa.

3. Waandalizi(16) wa kipindi tukakubaliana kuwa kwa kuwa ni vigumu kupata ratiba itakayokubaliana, basi Mimi nitaendelea na kipindi Kesho ( kurekodiwa)(17) saa 5 asubuhi na CCM itakuwa na siku yake. Sijui sasa Propaganda ya nini hata katika jambo Kama hili. Nami ningelipenda ningelienda mbali zaidi, kwani kipindi tangu kinapangwa zaidi ya siku 10 iliyopita(18) nilihusika mmoja kwa mmoja(19). Kimsingi ni viongozi wa ajar(20) wasioheshimu appointments, na Kama kweli kulikuwa na dharura si tungelipeana taarifa basi? Nadhani nisiendelee zaidi, wenyenkuelewa(21) watakuwa wameelewa, na walioleta propaganda ya Dr Slaa kukimbia.... Wajue kuwa propaganda itajibiwa vilivyo, na ukweli utashinda daima.
 
Hapana. Nadhani ni wanyama ndo wanaosomaga Tanzania Daima kama kina Nape Mnauye maana hata nukuu yake alotuletea hapa kaisoma huko Tanzania Daima.

asante kwa taarifa, basi hata mmiliki wake atakuwa ni mnyama!
 
Ndugu mwenezi Nape Nnauye kama nilivyokueleza tangu awali kwamba wewe bado ni mtoto mdogo unanuka maziwa ya mama, hujakomaa kiasi cha kukaa meza moja na Dr.Slaa kujadili mambo ya nchi hii.

Huko ccm wamekupa hiyo nafasi ili upate fursa ya kujifunza na kukua ili hatimaye upate kufikia kiwango cha kuyajua na kuyakabili mambo makubwa ya nchi hii. Sasa huu muda unaoupoteza kwa kumjadili Dr.Slaa kukataa kufanya mjadala na wewe ungeutumia vizuri kuendelea kujifunza siasa za nchi hii zenye mrengo wa kujenga umoja na mshikamano badala ya kujikita katika kueneza chuki, ubaguzi, fitna, majungu na kila aina ya uzushi.

La mwisho, gazeti la uhuru halina wanunuzi kwenye vibanda vya wauza magazeti, ndio maana mmeilazimisha serikali yenu kulinunua kwa lazima katika maofisini ambako halisomwi na mtu yeyote. Tanzania Daima ni mojawapo ya magazeti machache yanayoaminika na kusoma na watu wengi sana kiasi kwamba ukifika vibandani hadi saa nne hupati nakala hata moja iliyododa mezani.Sasa ni wazi kuwa huwezi kulinganisha gazeti makini la Tanzania Daima na kijarida cha udaku kinachoitwa uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Tafadhali wana JF!

Kuna yyt hapa ANAYEWEZA kuniambia hasa Nape thesis yake kwenye bandiko lake hili ni nini au ilikuwa nn?
Maana nimesoma tena na tena lkn sikuweza kujua hasa lengo lake la kutuambia lilikuwa nn zaidi ya kujichanganya tuu!Pls nisadieni!!
 
Nape ameshindwa kurithi busara za baba yake......Ungekuwa kama baba yako ungeheshimiwa sana ila kwa sasa naona unapuliza tu vuvuzela kila kukicha....ama kweli moto huzaa majivu

List ya watoto wa mzee Nnauye umeiona? hajawahi kuorodheshwa kama mtoto wa Nauye kwenye mirathi.Ofcoz inawezekana ni kwa sababu ni mtoto wa nje ya ndoa, yan huku kwetu huitwa Mwanakharamu, sasa tangu lini Mwanakharamu akarithi mazuri ya babakharamu wake?
 
Back
Top Bottom