Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Mkuu Nape Nnauye , naona umeona jinsi Vijana wako wa Lumumba wanavyo Under Perform Hapa Ndani.
Soo umeamua kuja kuwa Boost, heheheheh
 
Last edited by a moderator:
nakushauri.
1.mtafute mama yako akufundishe adabu.
2.Siasa ni siasa na utu ni utu ,mpe heshima SLAA na siyo kumuita babu.
3.Fuata maadili ya kazi yako.

4.Kuwa na mipakaya kazi yako au wewe ndo kinana?
5.Epuka cheap popularity.
6.Jitathimini kisiasa.
familia ni kitu cha msingi sana na kama ni ujenzi basi hili ndilo tofali moja moja ambayo yakijumuishwa ndio yanafanya nyumba kuwa imara, 'nyumba' kwa maana ya nchi. Tumedharau sana hii taasisi (ya familia) na sio ajabu kukuta mtu anajivuna kwa kuwa na nyumba ndogo nyingi. Matokeo yake hata wale watu tunaopaswa kuwapa heshima bila gharama tunatumia gharama kubwa kuwadharau sababu ya malezi mabaya!!!!
mwenye makosa ni huyo aliyempa kinana cheo kwenye chama
hivi kweli kuona huona hata kupapasa pia, au lao ni moja.
hapa ndio kila nikijiuliza sielewi na mpaka ninavyoandika hapa sielewi aliyempa nafasi hii ana malengo gani binafsi na uchungu wa nchi kiujumla na alishauriana na nani kabla ya kufanya hivyo!


 
Hamocha😛amoja na sintofahamu ya historia yako,bado mm naamini wewe ni "mnyampaa".Viti yule mla fisi(mnyiramba,mtani) yupo au kapeleka ushahidi mbinguni? msalimie

wewe ni mnyampaa gani mjinga namna hii mbona watu wa singida wanaheshimika na wanaaminika sana????
 
Dr. Slaa kwa sasa yuko DESPERATE kupewa Urais. Anafahamu kuwa, kama hataupata Urais 2015 basi hiyo itakula kwake kwa sababu atakuwa na miaka 67. Legally kwa sasa ni PENSIONER. Come 2020 atakuwa na miaka 72.

Kwa sasa mpaka anajaza watu kwenye mitandao kuleta uongo ambao hata hivyo unawafaa watoto wa chekechea. Mara, kapigiwa mizinga na Rais wa Zambia, mara, ooh, Nilikuwa nataka kufanyiziwa kwa ajari ya gari ya kutengeneza , mara, ooh, Ninafuatiliwa barabarani. Ilimradi vulugu tupu.

Toka uchaguzi wa 2010 ulipoisha, amekuwa akifanya kampeni za Urais karibia kila siku. Swali la MSINGI ambalo watu ingekuwa vizuri wakajiuliza, WHY HE IS SO DESPERATE TO BE THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.

Changamka Mwingulu amesharudi posho inaweza kuongezeka kwa utumbo ulioandika huku.
 
nape ni mwanasiasa kijana ambaye taifa kwa sasa linamtazama kwa macho mawili huu siyo wakati wa viongozi wazee kama mzee slaa jamani tuachiwe vijana.
 
Ndugu yangu Nape naomba nikushauri;
  • Kikatiba, sasa hivi tupo katika siasa na demokrasia ya vyama vingi hivyo sitegemei kama kuna chama chochote cha upinzani kitakachopoteza muda wake kukisifia chama tawala kama ambavyo wewe unataka iwe. Kama kuna mwanachama wa namna hiyo kutoka upinzani, huyo hajui dhana ya demokrasia ya vyama vingi wala upinzani kwa hali yoyote ile.
  • Wewe ni Mwenezi Chama Tawala, hivyo ningetazamia utatumia muda wako kukijenga chama chako na taasisi zake ili katika hali yoyote ile msilaumike ama msionekane dhaifu ama kulalamikalalamika kama ambavyo unaonekana katika mtandao huu kwa kujinasibu na vijisabababu sababu ambavyo pengine inaonekana kama havina mashiko, badala yake tumia platform (position yako) kuadress issues.
  • Pia tujaribu sote kusoma alama za nyakati. Hivi ndugu yangu Nape, ni kweli kabisa kwamba huoni viashiria vyovyote vinavyowafanya watu wengi zaidi kupenda upinzani kuliko hata chama chako CCM?
  • Mwisho, endelea kuimba wimbo wa kueneza uzuri wa chama pasipo kufahamu viashiria vingine... Hakika sitashangaa CCM kupotea katika historia kama ilivyokuwa kwa vyama vingine pigania uhuru kama vile UNIP, KANU n.k.
 
Mkuu Nape Nnauye , naona umeona jinsi Vijana wako wa Lumumba wanavyo Under Perform Hapa Ndani.
Soo umeamua kuja kuwa Boost, heheheheh

mkuu mwaka huu utamkoti nape mpaka basi hata ukiwa usingizini kumbe anawatesa sana,kweli siasa ngumu.
 
Kama JK mwenyewe hawezi kusimama kwenye madahalo na Dr. Slaa, itakuwaje Katibu wake mwenye kashfa ya ujangili? Lazima asepe hana hoja watanzania tunajuwa!
 
Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la CHADEMA la Tanzania Daima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu.

Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya Tanzania Daima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la CHADEMA limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la CHADEMA leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda.

WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

================================
Habari kamili toka Tanzania Daima
================================

Walatini wanasema FALSUS IN UNO, FALSUS IN OMNIBUS yani false in one thing , false in everything . Sentensi yako kwamba uhuru limekuewepo kabla ya CCM ni false kimantiki, hivyo inayafanya maelezo yako yote kutokuwa na mantiki.
 
Kwa mazoea yako ya kumwita BABU DR Slaa ndio maana alisepa, naamini alifikiri ungeenda zaidi ya hapo. Bora Kinana huwa anaongea kwa staha na kwa heshima.

tatizo la nape ni la kisaikolojia zaidi,nape inawezekana kweli hamjui baba yake...nasema hivo nikiwa na maana ya kuwa kama kweli nape anamjua baba yake kweli anaweza kuzaliwa na Dr.Slaa ki-umri? Kama siyo nape anapata wapi wazo la kumuita babu mtu ambaye umri wake ni mdogo kuzidi wa babae nape au nape anajiona bado serengeti boy mpaka mda huu? Au labda akisikia watoto wake wanaita babu naye anakurupuka bila kufikiria kuita hivo!
 
Nasikitika kama huyu ndiye katibu muenezi wa CCM hajuwi hata kupanga hoja lakini simlaumu kwakuwa yeye ungojea wenzie wenye akili wazungumze ndiyo azungumze kama kipaza sauti.Hiki alichokiandika humu ndani hakina maana kutokana na maneno aliyotangulizwa kama kichwa cha habari.Bado sana kajipange bwana mdogo
 
Nape ni janga la taifa. Kama vijana tulio nao kwenye chamba kinachoendesa serekali ndio hawa, basi tuna kazi ngumu. Hawa ndio makaburi yao yatachapwa na wajukuu zao
 
Babu ana ndoto za kuwa Rais wa nchi hii.Kweli Maajabu yapo Chadema.Mpaka anakufa atabaki anangalia Majengo ya ikulu tu kwa mbali.Ikulu ni mahala pakatakatifu sio mahali pa kwenda kufanyia nani kule
 
Nape tunakuitaji uje tena huku New york.unajua tulikufanya nini?.Mbona ukufika kufungua tawi la ccm hapa washington DC??????????.Unajua sisi ni akina nani.Una ubavu wa kuongea na Dr slaa.sisi unatukimbia na ni wadogo sana.
 
Babu ana ndoto za kuwa Rais wa nchi hii.Kweli Maajabu yapo Chadema.Mpaka anakufa atabaki anangalia Majengo ya ikulu tu kwa mbali.Ikulu ni mahala pakatakatifu sio mahali pa kwenda kufanyia nani kule
 
KOSA LA TANZANIA DAIMA LIKOWAPI???KUELEZA HALI HALISI KWA YALIYOTOKEA???NAPE NJOO UTUAMBIE KATIKA MANENO HAYA HAPA CHINI UWONGO UKO WAPI?????
Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema: “Ni kweli tulikuwa tumealikwa kwenye mdahalo pale ITV (leo) jana saa 3, nilipofika nilikutana na Nape, nikamsalimu nikajua kuwa alikuwa amemsindikiza Kinana, lakini nilipomuuliza mwendesha kipindi kwamba Kinana yuko wapi, alisema amepata udhuru hivyo hajafika.

“Nilimwambia Nape wewe si saizi yangu, sitaweza kuongea katika kipindi hiki kama Kinana hayupo, hivyo kipindi hiki kiahirishwe hadi Kinana atakapokuwa na nafasi ya kuja,” alisema Dk. Slaa.

“Haiwezekani mwenzangu akaahirisha ghafla kuja kwenye kipindui halafu nisipewe taarifa na badala yake nikatumiwa Nape, Nape si saizi yangu,” alisisitiza Dk. Slaa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya kuahirishwa kipindi hicho, Nape na Dk. Slaa walisalimiana na kuagana. “Naamini siasa si uadui, niliongea na Nape nikamuuliza Kinana yuko wapi, alisema alikuwa amepata udhuru, akanipigia simu nije,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, Nape alisema alikwenda ITV badala ya Kinana, kuangalia maudhui ya kipindi hicho ili aweze kushauriana na Kinana na kuamua kuja au la.

“Mimi ndiyo msemaji wa chama, katibu mkuu hawezi kualikwa mimi nisiwe na taarifa, mimi ndiyo napaswa kwenda na nilikwenda nilipokutana na Dk. Slaa tukaelezwa, Dk. Slaa alishauri kuwa inafaa kualika watu wenye hadhi zinazofanana, yaani makatibu, hivyo mimi niliondoka nikamwacha Dk. Slaa, nadhani alirekodiwa kwa kuwa walisema wanaweza kurekodi mtu mmoja mmoja na katibu mkuu wetu anaweza kwenda siku nyingine kurekodi,” alisema Nape.

 
Back
Top Bottom