Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 754
- 3,097
Wakati wa chaguzi mbalimbali duniani huwa viongozi na wanasiasa wanatoa kauli mbalimbali katika kunadi sera zao na vyama vyao kwa ujumla. Kauli zinazotolewa huweza kuwa nzuri za kujenga au zikawa kauli za chuki zenye lengo la kugawa na kubagua kundi fulani.
Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa wagombea wakishindwa kujinadi kwa sera zilizo saaafi ili wakubalike, basi wanaweza kutumia njia mbadala ambazo zinaweza kuwa za chuki na kugawa jamii, hivyo viongozi hao hawapaswi kabisa kuchaguliwa.
Pia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonia Guterres alitoa hadhari kuwa hotuba za chuki zinapaswa kuchukuliwa kama tunavyochukulia vitendo vyovyote vibaya, kwa kuzilaani, kutoziendeleza, kukabiliana nazo na ukweli na kuchagiza wanaozitekeleza kubadili tabia.
Narudi kwako mdau; je, ni kauli gani zimewahi kutolewa na kiongozi au mgombea wakati wa kipindi cha uchaguzi ukaona zinaathiri mchakato mzima wa Uchaguzi?