Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Nlikuwa namtetea sana Makonda ila kwa upumbavu wake alioongea jana nmemdharau sana!

Jamaa ni kama hajatoka kijijini vile yani. Maneno kama yale ilitakiwa waongee kina Rizi one watoto wa mjini wasiojua shida za watu huko mashambani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kumtetea mkuu,yaani ile shombo ya juzi ndio ikutoe usingizini? Kashavurunda mangapi kwani,endeleeni kupiga zumari tu hadi siku damu zikiwatoka masikioni ndio mtaelewa.
 
Nilikaa hadi saa saba nasubiri wazime lakini hola,nikalala nikaamka asubuhi nakuta bado minara imesimama ndo nimejua zilikua porojo tu hawana jeuri hiyo
 
Ni mwendo wa kata funua...

Serikali ikishaanza ona tule tuchenji twa VAT kwenye miamala na vocha tumeanza pungua, naamini watakuja upya na utaratibu mwingine wa namna ya kusajili
 
Wabongo tuache kulalamika mimi nilienda nida pale kinondoni mwaka 2018 mwezi wa 3 nilikuta kweupee hakuna watu nikajaza form nikakaa wiki nikaenda kupiga picha baada ya wiki 2 nikapata kitambulisho .. ukiwauliza watu miaka yote hiyo walikua wapi watakwambia foleni

Wacha sheria zitunyooshe tu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
wengine 2metimiza miaka 18 wiki iliyopita co sio kosa le2
 
line haziwezi kuzimwa , ilikuwa ni mikwara tu watu wakasajili, muda utaongezwa, makampuni ya simu hayawezi kukubali hiyo hasara, kuna matatizo sana ya nida maeneo ya mipakani kigoma, bukoba, tunduma , watu wengi wameshindwa kujiandikisha, i
 
jamani mimi leo tarehe 21/1/2020 saa 08:24 bado line yangu iko hewani sijajua huenda wamenisahau au bado wanazirecord ili ziweze kuzimwa kwa pamoja
 
Naomba kutofautiana na wewe kwenye hili... Wananchi walijitokeza kwa wingi sana 2013.. Foleni zilikuwa ndefu mno watu wakaacha kazi.. Mimi nakumbuka nilienda mara 3 pale Riverside ubungo, kila nikifika watu walishafika tangu alfajiri.. Hatimaye nikafanikiwa kujiandikisha siku ya nne
Mpaka kufika 2014 nikawa bado sijapata kitambulisho
Siku moja nikaenda bank pale mlimani city nikakuta tangazo la kusajili tena kupitia bank.. Nilafanya hivyo kwa mara ya pili nikaambiwa nisubiri nitapata ujumbe wa NIDA.. Ikawa holla mpaka nilipoenda kujisajili tena 2019 ambapo ilinichukua miezi sita kupata number na si kilambusho kwa maana ya hard copy na mpaka leo bado
Je ni wangapi wamehangaika na kuhangaishwa kama mimi? Hiyo 2018 unayosemea wewe watu walikuwa wamekwisha kata tamaa... Hivyo kuwalaumu pekee bila serikali si sahihi
Wabongo tuache kulalamika mimi nilienda nida pale kinondoni mwaka 2018 mwezi wa 3 nilikuta kweupee hakuna watu nikajaza form nikakaa wiki nikaenda kupiga picha baada ya wiki 2 nikapata kitambulisho .. ukiwauliza watu miaka yote hiyo walikua wapi watakwambia foleni

Wacha sheria zitunyooshe tu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Back
Top Bottom