Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Wamepitiwa na usingizi. Ngoja tusubiri asubuhi wakiamka huenda wakakumbuka kuzima line
Ni saa 09:00 sasa, ninavyojua mimi TCRA hawana uwezo wa kuzima line zote at once zoezi la kuzima laweza kuchukua zaidi ya mwezi, uwezo wetu kiteknolojia ni mdogo sana,
Na kuna uwezekano wakaanza kuzia hata line ambazo zimesajiliwa kwa alama za vodole

tapatalk_1579554207357.jpeg
 
Tatizo sio uzembe wa raia, shida ni nida hawajajipanga vizuri kuwahudumia watz,
Vituo vyao ni vichache na huduma zao ni taratibu mno! Kiasi ukianza kufuatilia uache kila kitu!

Hii ni shida sana wakati kuna njia nyingi tu za kurahisisha hili zoezi.

Kimfano mtu mwenye leseni ya kuendeshea, kadi ya mpiga kura ama pasport. Huyu tayari alishafanya fingerprint.

Angewezeshwa kuatach doc zake angewekewa nafasi ya kujaza maelezo ya ziada wanayoyataka online kisha akapewa namba ya nida hapo hapo online.

Shida mamlaka zetu zimejaa rushwa kiasi unakuta mnyarwanda ana kadi ya mpiga kura ya tz! Nk. Nk.

Namwomba mh. Raisi wa wanyonge,
Kama itakupendeza mh. Watumbue wote waliokupotosha na kutusababishia sisi wanyonge usumbufu mkubwa na hasara!

Mf. Mh mimi jana usiku imebidi nitoe vijisenti vyangu kwenye line na nimekatwa!
Kwahiyo kutoka 2014-2019 ulikosa ila wengine walipata mfano mimi nilichelewa sikujiandikisha mapema ila nilikomaa mpaka nikapata kitambulisho tukubali tu tulizembea sana japo kwa sasa tunajisahau mno na kuona serikali haiwezi kufanya chochote

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Redmi Y2
 
Nyie mnao sema TCRA hawawezi kuzima line za simu lazima mtakuwa mmesha sajili msituchongee sisi tafadhali, hivi mna mchokoza nani?????.

Kweli wabongo NYOSO.

TCRA mnaweza kuzima simuzetu wakuu achaneni na hawa wahuni please,please please.




Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kaa ule bata Mkurugenzi wao ameshasema kwamba watakuwa wana edit line moja moja, na pia wanakuachia uwezo wa kutuma na kupokea sms, usitie shaka.
 
Imebakia robo saa kutimia saa sita kamili ya tarehe 20. January. 2020.. Muda ambao ni kikomo cha mwisho kwa wasiosajiliwa kwa alama za vidole wafanye hivyo la sivyo kuanzia saa sita na dakika moja laini zote ambazo hazijafanya USAJILI WA vidole zitazimwa... Ina maana baada ya hapo laini kwenye simu husika haitafanya kazi tena...

Huu ni mtego wa hatari mno kwa serikali kama haijajipanga vema na tayari kuna baadhi ya wananchi wameshaanza kubeza hiyo hatua kama hili zoezi la kuzima lisipofanyika ama lisipofanikiwa

Kuna machache kwenye mengi ya kujadili hapa...
1. Je serikali imeshafanya upembuzi yakinifu kwenye hili, hasara na faida zake? Je hasara ni zipi na faida ni zipi?

2. Je muda huu mamlaka ya mawasiliano kupitia mitandao husika wako kazini wakisubiri dakika zilizobakia waminye kitufe cha kuzima laini? Je mamlaka kupitia mitandao husika ina uwezo na zana zenye nguvu za kuweza kuzima laini zaidi ya milioni 20 ambazo bado hazijapata usajili?

3. Je hili haliwezi kuchukuliwa kama uhujumu uchumi kutokana na serikali kukosa mapato makubwa ndani ya saa 24 zijazo? Kuanzia miamala ya pesa, manunuzi ya muda wa maongezi, vifurushi vya data nknk?

4. Je serikali haiwezi kushitakiwa kwa uzembe na usumbufu? kwakuwa kama wangetuma watu wao kwenye vituo vya usajili wangeona wananchi wanavyopatishwa tabu kwenye kupata vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kupata usajili wa simcard?

5. Dhihaka ni jambo baya sana kwenye mambo muhimu ya KITAIFA.. Lakini mkuu wa mkoa wa DSM katoa dhihaka kwa wale watakaozimiwa simu zao usiku huu kama ni watu waliokuwa na michepuko... Je ana ushahidi na ithibati kwenye hili? Nini maana ya kuwa kiongozi?

Tayari ni saa sita na dakika tatu siku ya tar 21 January 2020... Nadhani muda huu tayari zoezi la kuzima limeshaanza... Likifanikiwa hili kuna madhara mengi yatatokea usiku huu.. Kuna dharura hazitafanyiwa kazi.. Kuna vifo vitatokea kwa kukosa mawasiliano... Kuna watu watakwama kusafiri, kutuma pesa ya dawa, chakula nk kwa kukosa kufanya miamala nknk...

Kuna nafasi bado ya kutafakari kwenye hili... Lakini je serikali iko tayari kujishusha na kukiri wazi kuwa haikutafari vema kwenye hili? Muda utasema kukipambazuka.. Lakini tayari kejeli zimeshaanza
View attachment 1329002

Jr
Mkuu Mshana, kumbukumbu zangu zinanionesha kwamba serikali hii haijawahi anzisha jambo likaenda smoothy kwa sababu hawana Plan bali ni kukurupuka, yote uliyoyasema hapo juu hawana majibu yake na ni bora wewe ndie ungekuwa rais, kama serikali inaongozwa na watu ambao tuaambiwa wengine sijui vichaa mara wengine wanakiri wameokotwa toka jalalani, na pia

tapatalk_1579554207357.jpeg
 
henrykilenga,
Acha kiudanganya,watu tumejiandikisha 2018 mwezi wa tatu kwa kupanga foleniu ndefu,na hadi leo tumeambulia kudownload vitambulisho online,huo mwaka unaosemea wewe tayari zoezi liliazna Dar es salaaam na watu hawakupata.
Na kumbuka ndani ya hiyo miuaka miwili,umri wa miaka 18 umeongezeka,ina maana na wao wana lalamika,acha kutetea NIDA,mamlaka imekwama na ndio inakwamisha watanzania na ndio maana wanatimuliwa kazi na mwingine jana kakamatwa.
 
Ilikuwa ni janja ya kuwasukuma watu wapate vitambulisho vya uraia?
Maana naona laini za simu ambazo hazijasajiliwa bado zipo hewani.
Au deadline bado?
 
Back
Top Bottom