Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Hapa tatizo sio nida , tatizo ni serekali yenyewe haihitaji kuongeza ruzuku kwa nida ili nida waongeze vituo vingi vya uandikishaji , vituo vikiwa vingi zoezi linakua jepesi
Kilichobaki ni usumbufu tu kwa wananchi
Over.

Sent using Jamii Forums mobile app
Matatizo ni mengi huko NIDA sasa Mimi najiuliza mbona kuna rundo la watu mkoa wa manyara wamejiandikisha tangu mwezi wa saba mwaka Jana si namba wala kitambulisho kilichotoka sasa nao watafungiwa laini zao?
 
Ila wanatupeleka puta hawa jamaa sijawahi ona. Ila Makonda sio mtu mwenye talanta ya uongozi kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Nlikuwa namtetea sana Makonda ila kwa upumbavu wake alioongea jana nmemdharau sana!

Jamaa ni kama hajatoka kijijini vile yani. Maneno kama yale ilitakiwa waongee kina Rizi one watoto wa mjini wasiojua shida za watu huko mashambani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la NIDA. inawezekanaje mtu analala akiwa hajui hatma ya mawasiliano yake? Yaani watu wanakesha kama wanasubiri mwaka mpya. Hawajui kama watafungiwa au la!!

Hii inatisha sana kwa mustakabali wa taifa. Wakati wa kuandikisha wapiga kura na kutoa vitambulisho vya kupigia kura mnafika hadi kwenye kata. iweje hivi vya NIDA serikali ishindwe?

Kuna ulazima gani wa kufanya sasa kwamba lazima kila mtu ajisajili kwa kitambulisho cha NIDA ili hali mkijua hali halisi ilivyo!! Na sheria kandamizi eti ukimsajilia mtu naenda jela?

Ndugu zetu, wazazi wetu huko vijijini tutawasiliana nao vipi na tukiwasajilia huku mnatufunga?

IFIKIE HATUA WATANZANIA TUWE NA HATMA YA MAISHA YETU MIKONONI MWETU. HIKI KIKUNDI CHA WALIOSHIBA MADARAKA KITALIANGAMIZA TAIFA

Sent from my iPhone using JamiiForums
Umelia sana.mkuu Mungu amekusikia kilio chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wazee wa mitandao ya simu tunaliana timing tu.! Wanasubiria tujisahau na kulipa videni vyao... Thubutuuu!

Mimi voda nimekopa nipige tafu deni 4500/=, mpawa 60,000/= na songesha 11,769/=

Hii wahesabie ni hasara kwao... nasubiri wafungie tu na kama hawafungii bando langu likiisha nafanya mchakato wa kupata namba mpya
 
Taifa la kijinga sana hili, hivi MTU akijiandikisha kupitia driving license, passport, kitambulisho cha kupigia kura kuna Shida gani? Mbona nchi zingine haina haya mambo ya kishenzi shenzi? Sijui watu wana ushamba wa aina gani jamani? Tunapeana ma deadline yasiyokuwa na maana. Then wanakuja wanadai hatuzimi tena, umewatia watu pressure ya nini? Mbona tunakuwa kama tupo taifa LA wendawazimu?
 
Nadhani kufungiwa kunawahusu zaidi wale mil 6 waliokwishapewa namba za NIDA mpaka sasa hawajajisajili na wale ambao hawakuwahi hata kujaza fomu za NIDA kuomba vitambulisho

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado ni hasara pia kubwa sana Ki uchumi...huwezi amka tu unafunga funga vitu.
Tena mwenye tatizo ni wewe si wananchi..wahanga tupo wengi sana.Toka 2016-2017-2018 napambana na NIN.Hapo sijapata ile hard copy.
Imenilazimu kutengeneza tu soft yangu ya kitambulisho maana ..wajitazame vizuri sana.
 
Wabongo tuache kulalamika mimi nilienda nida pale kinondoni mwaka 2018 mwezi wa 3 nilikuta kweupee hakuna watu nikajaza form nikakaa wiki nikaenda kupiga picha baada ya wiki 2 nikapata kitambulisho .. ukiwauliza watu miaka yote hiyo walikua wapi watakwambia foleni

Wacha sheria zitunyooshe tu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo sheria zitawanyoosha wote waliosajiliwa na wasiosajiliwa, mawasiliano hayachagui ukishamkosa mtu wako muhimu kisa hajajisajili ndio utajua hii sheria imemnyoosha nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom