Kuchukiwa pasipo sababu...

Kiziza

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
439
77
Hivi ni kweli kwamba kuna mtu anakuwa anachukiwa bila sababu,yaani kwamba kazaliwa tu hivyo.

Acha ile hali ya kawaida kwa mwanadamu
kuwa hawezi kupendwa na wote,hata manabii hawakupendwa na wote.

Lakini kuna ile unakuta mtu popote anapokuwepo inatokea hapendwi yaani iwe chuoni,ofisini au kwenye jamii kwa ujumla.

Sasa je ni kweli kuna kitu kama hicho yaani mtu anakuwa tu hapendwi?Au muhusika anakuwa ndio sababu ya yeye kuchukiwa kwa sababu mbalimbali ikiwepo tabia n.k?

Nimeshawahi kusikia neno ...damu ya kunguni...,utasikia fulani ana damu ya kunguni anachukiwa tu bila sababu,ni kweli???
 
Mkuu kuna watu yaani damu haziendani,unakuta sio wewe tu au hata wengine,au unakuta kuna familia watu wanaikwepa.
kuna kaukweli
 
Siamini kuzaliwa na "Bahati ya kuchukiwa bila sababu"

Hakuna hicho wala kitu "damu haziendani" kwangu.

Anaekuchukia ana sababu japo ziso msingi na inawezekana mwenyewe hazijui tu
 
Siamini kuzaliwa na "Bahati ya kuchukiwa bila sababu"

Hakuna hicho wala kitu "damu haziendani" kwangu.

Anaekuchukia ana sababu japo ziso msingi na inawezekana mwenyewe hazijui tu
Gaijin ipo sana tu labda we hujawahi kuona,usijiangalie wewe angalia familia zinazokuzunguka
 
Kuchukiwa bila sababu? Sidhani kwa kweli.
Kama mtu anachukiwa constantly basi kuna kitu toka kwake (attitude, character, etc) kinamfanya achukiwe. akibadili hicho kitu ataona mambo yake yanabadilika pia.
 
Gaijin ipo sana tu labda we hujawahi kuona,usijiangalie wewe angalia familia zinazokuzunguka

Mie sijakutana nayo hiyo kwa hata familia zilizonizunguka.

Mi nadhani ni mitizamo tu, vitu ukiviangalia kwa jicho fulani ndio hivyo hivyo vinavyokuwa
 
Kisaikolojia hii inaelezewa na dhana ya projection.

Unaweza kudhani kila aliyekuzunguka hakupendi wakati huenda wewe mwenyewe ndiyo hujipendi na huko kutokujipenda ndiyo kunapelekea udhani kuwa watu hawakupendi.

Au unaona kama vile umezungukwa na watu wachoyo kumbe ukweli wa mambo wewe mwenyewe ndiyo mchoyo ila hujijui tu!
 
Kuchukiwa bila sababu? Sidhani kwa kweli.
Kama mtu anachukiwa constantly basi kuna kitu toka kwake (attitude, character, etc) kinamfanya achukiwe. akibadili hicho kitu ataona mambo yake yanabadilika pia.
Hivi unachukia tabia za mtu kutokana na kukosana naye au hata usipokosana naye bado utachukia tabia zake?
 
Mie sijakutana nayo hiyo kwa hata familia zilizonizunguka.

Mi nadhani ni mitizamo tu, vitu ukiviangalia kwa jicho fulani ndio hivyo hivyo vinavyokuwa
umeficha ukweli,ila nakuja na swali
 
I believe it has a lot to do with general demeanor and attitude. Some people apparently appear to have a negative vibe about them regardless. That being said, who doesn't have a story of feeling hated for all the wrong reasons at one or another occasion?
 
Mara nyingi mtu ambae anasema kua anachukiwa bila sababu ni tu kwamba hataki face facts kua kuna sababu zimefanya achukiwe, hizo zaweza kua sababu za msingi ama za kijinga, Lakini siamini kua kuna kuchukiwa bila sababu.... Why mtu out of No where akuchukie alafu ujustify kua umechukiwa bila sababu? Sometimes it is good kujitazama upya kupata jibu.... You may not like the truth thou....
 
Hakuna kitu kama hicho! Mtu anayesema anachukiwa bila sababu jaribu kumchunguza yeye ama wanaomchukia.........lazima kuna sababu tu!!!
 
Haiwezekani kila mtu awe ni mbaya kwako, kila mtu anakuchukia, wewe tu, kila mtu hakutendei haki, kila mtu ana kasoro?
Je wewe ndivyo unavyoishi hivi? Kama jibu ni ndiyo au kama una mtu wako wa karibu ambaye anaishi katika mtindo huu wa maisha, unapaswa kujua kwamba, una mtu ambaye ana matatizo makubwa.

Kwa nini?

Ni kwa sababu haiwezekani kila mtu akawa kama mwingine, yaani akikuchukia huyu na yule ni lazima atakuchukia, ni lazima hatakutendea haki na mengine ya aina hiyo. Kwa nini sasa wote wawe na tabia za aina moja, yaani wafikie kukuchukia?

Kwa kuwa watu hawafanani kitabia, kimwenendo na kimtazamo, ni wazi ukiona wote wanakuchukia wewe, tatizo haliko kwao, kwa sababu hawawezi wote kuwa na mkabala wa aina moja. Ina maana kwamba wewe ndiye ambaye hujipendi na kutojipenda kwako kunaonekana kwa watu hao.

Tunaposhindwa kujipenda, hasira dhidi yetu huwa tunazitolea kwa watu waliotuzunguka. Kwa hiyo kama unahisi kwamba watu wanakuchukia, jitahidi kujiuliza kuhusu jambo hilo. Ni wazi haliwezi kuwa jambo la kweli hata kidogo. Kama ni
kuchukiwa, hivi inawezekana ukachukiwa na kila mtu kweli?
 
Siamini kuzaliwa na "Bahati ya kuchukiwa bila sababu"

Hakuna hicho wala kitu "damu haziendani" kwangu.

Anaekuchukia ana sababu japo ziso msingi na inawezekana mwenyewe hazijui tu

Ni kweli sasa unakuta hakuna wa kumueleza muhusika ukweli na anaishia kuona watu wanamchukia.
 
Kuchukiwa bila sababu? Sidhani kwa kweli.
Kama mtu anachukiwa constantly basi kuna kitu toka kwake (attitude, character, etc) kinamfanya achukiwe. akibadili hicho kitu ataona mambo yake yanabadilika pia.[/
QUOTE]

Ni kweli sema unakuta mtu mwingine anajiona yeye yuko sahihi na wengine ndio wenye problem.
 
Kisaikolojia hii inaelezewa na dhana ya projection.

Unaweza kudhani kila aliyekuzunguka hakupendi wakati huenda wewe mwenyewe ndiyo hujipendi na huko kutokujipenda ndiyo
kunapelekea udhani kuwa watu hawakupendi.

Au unaona kama vile umezungukwa na watu wachoyo kumbe ukweli wa mambo wewe mwenyewe ndiyo mchoyo ila hujijui tu!

kweli matokeo yake mtu anaanza kuhisi watu wanamuona vile anavyojiona.
 
Mara nyingi mtu ambae anasema kua anachukiwa bila sababu ni tu kwamba hataki face facts kua kuna sababu zimefanya achukiwe, hizo zaweza kua sababu za msingi ama za kijinga, Lakini siamini kua kuna kuchukiwa bila sababu.... Why mtu out of No where akuchukie alafu ujustify kua umechukiwa bila sababu? Sometimes it is good kujitazama upya kupata jibu.... You may not like the truth thou....

Ni kweli na kuna aina ya watu unakuta anafahamu kabisa ni nini kinafanya watu wamuone hivyo lakini anakuwa na ile attitude ya kutokujali na anaendelea kuumiza wenzake.
 
Back
Top Bottom