Je, ni kweli kupendwa au kuchukiwa na watu kunatokana imani za giza au muonekano wa mtu?

MWANAHARAKATI MWEMA

Senior Member
Dec 16, 2022
192
270
Namshukuru mwenyezimungu mwingi WA kusamehe, pia nawashukuru wazazi wangu Kwa kunizaa pia nawasalimu wote ambao tupo kwenye jukwaa hili.

Kwanza kabisa naomba niseme wazi kwamba Mimi ni miongoni mwa watu ninaojihisi nachukiwa sana katika maisha yangu, nimekuwa napitia changamoto za kukejeliwa na kunyooshewa vidole na wafanyakazi wenzangu.
Nimekuwa nikijitaidi sana kuonyesha upendo Kwa wenzangu na na KUTOA ushauri wa masuala mbalimbali inapotokea inaitajika lakini mara nyingi mawazo yangu huwa yanapingwa na kupuuzwa.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa natafakali Kwa nini imekuwa hivyo, japo nimejitaidi kujipendekeza Kwa baadhi ya watu lakini wengi wanakuwa kama hawapendi kuwa na Mimi, kila mara nimekuwa najiuliza Shida nini au nimelogwa au Kwa Sababu Sina uhandsome, au Kwa Sababu sinywi pombe au Kwa Sababu uwezo wangu fedha haunifanyi nipewe heshima.

Maswali ni mengi sana kiasi naisi nimechezewa labda na wengine wanapitia haya au ni Mimi TU, na kama Kuna vigezo vingine niambiwe Kwa maana mpaka natamani nianze kujichubua niwe mweupe au niende Kwa mganga ili kama nimetupiwa mikosi ili niitoe.

Ndugu zangu sikieni TU mtu kuchukiwa inauma sana kiasi unaweza kujitoa uhai,Mimi napitia changamoto ambazo naona hazistaili kabisa ,najiona Ni kama Kazi niliyonayo inaniponza Kwa kuwa Mimi napenda sana kutetea haki na usawa.

asanteni.
 
Usiwape watu wengine jukumu la kukuonyesha thamani yako jipe thamani mwenyewe, ukihisi wanakupuuza au hawaoni umuhimu wako stay calm Acha wakupotezee we endelea kuwaheshimu na ukae kimya fanya kazi zako na urud nyumbani fanya vitu unavyopenda vinavyokupa furaha hata ukiwa peke yako.

Ukimpa mtu jukumu la kukuonyesha thamani yako anaweza kukufanya ujihisi takataka.
 
Namshukuru mwenyezimungu mwingi WA kusamehe, pia nawashukuru wazazi wangu Kwa kunizaa pia nawasalimu wote ambao tupo kwenye jukwaa hili...
Pengine unafanya jitihada za kuwa karibu na watu hadi unapitiliza unaonekana feki.

Fanya hivi kuanzia sasa usijipendekeze

Ukiona una ushauri , shauri halafu usifuatilie tena huyo mtu kaamua kufuata ushauri wako ama la.

Usijipendekeze kwa mtu,

Tafuta hoby, hakikisha urafiki wako ni kati yako na watu wenye hoby sawa na wewe au mnafanya kazi zinaendana

Pia soma sana vitabu vya mungu na sali sana, mungu afanye mambo yako yawe mepesi

Sent from my TECNO KI5k using JamiiForums mobile app
 
Kwanza uwe unajisalia upate Amani moyoni.

Lingine kubwa jifunze kujipenda na kufanya yako, bila kufikiria wengine eti wakupe furaha maishani mwako.

Lingine usitegemee furaha yako kuipata kupitia watu, kuna watu ambao hauoni umuhimu wa kuwa nao karibu ndio wanaweza kuwa wakukupa smile ukiongea nao.

Lingine fanya yako, usisikilize maneno au kufata tabia zao kwao na ujilinde pia.

N.b. kujipendekeza inafanywa kama kuna faida unatafuta ya kukuvusha kimaisha.. sio watu kuwa karibu yako tubkupiga story na kuchekeana. Kazini Fanya kazi ionekane Usijali hao unafikiri au unaona wapo ovyo kwako. Furaha yako, Amani yako.. si unandugu pia wakuongea nao..

Kila la kheri.. enjoy nyota yako kali na nzuri.
 
You are so obsessed..acha kutafuta kupendwa na watu jipende mwenyewe watu watakuja.
 
Kuhusu hitaji la kupendwa tu hilo huishia utotoni.

Utu uzimani mtu hupendwa kutokana na jinsi unavyohitajika wewe, kumbuka na wewe unahitaji watu, ila sidhani kama unahitaji watu wa kukuchekea,
unahitaji watu useful kwako (win win partnership),
Umeshasikia Boss hanuniwi. (Unadhani huchekewa yeye au mali zake?).

Jitahidi uwe shamba pendwa, usiwachukie walao matunda, kabla hawajala hakikisha wamepalilia hilo shamba lizae zaidi.
 
Namshukuru mwenyezimungu mwingi WA kusamehe, pia nawashukuru wazazi wangu Kwa kunizaa pia nawasalimu wote ambao tupo kwenye jukwaa hili.

Kwanza kabisa naomba niseme wazi kwamba Mimi ni miongoni mwa watu ninaojihisi nachukiwa sana katika maisha yangu, nimekuwa napitia changamoto za kukejeliwa na kunyooshewa vidole na wafanyakazi wenzangu.
Nimekuwa nikijitaidi sana kuonyesha upendo Kwa wenzangu na na KUTOA ushauri wa masuala mbalimbali inapotokea inaitajika lakini mara nyingi mawazo yangu huwa yanapingwa na kupuuzwa.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa natafakali Kwa nini imekuwa hivyo, japo nimejitaidi kujipendekeza Kwa baadhi ya watu lakini wengi wanakuwa kama hawapendi kuwa na Mimi, kila mara nimekuwa najiuliza Shida nini au nimelogwa au Kwa Sababu Sina uhandsome, au Kwa Sababu sinywi pombe au Kwa Sababu uwezo wangu fedha haunifanyi nipewe heshima.

Maswali ni mengi sana kiasi naisi nimechezewa labda na wengine wanapitia haya au ni Mimi TU, na kama Kuna vigezo vingine niambiwe Kwa maana mpaka natamani nianze kujichubua niwe mweupe au niende Kwa mganga ili kama nimetupiwa mikosi ili niitoe.

Ndugu zangu sikieni TU mtu kuchukiwa inauma sana kiasi unaweza kujitoa uhai,Mimi napitia changamoto ambazo naona hazistaili kabisa ,najiona Ni kama Kazi niliyonayo inaniponza Kwa kuwa Mimi napenda sana kutetea haki na usawa.

asanteni.
Jichunguze vizuri kuna kitu unakosea yawezekana kujipendekeza, kuwasema wengine, kupinga kila kitu, ubishi, kukosa ushirikiano na wenzako. Jenga mazoea ya kujiamini na kujishughulisha na mambo yako zaidi kuliko ya wengine.
 
Back
Top Bottom