Michezo gani ya shule ya msingi unaikumbuka?

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,746
Mimi kuna wakati niliipenda shule sababu ya michezo ambayo kwa namna yeyote ile ilinifurahisha,

Machezo wa kwanza ilikuwa ni wa kucheza mpira mnaweza kuwa hata mpo 30 hivi wote mnakuwa mnaelekeza mpira lango moja kunakuwa na golikipa sasa ukifanikiwa kufunga unachagua wa kumtoa, na mtu ambaye atakuwa wa mwisho yaaniambaye atamaliza kumtoa wa mwisho yeye anakuwa golikipa,

Tunarudi tena uwanjani sasa ole wako mtu uliye mtoa akakuwahi kufunga goli, unaweza kuanza kutoka mwenyewe kabla hujaambiwa, ilikuwa raha sana.

Mchezo mwingine ilikuwa ni wakati tunarudi nyumbani tunapitishiana mpira tobo, sasa tuna chagua mti au majani ya kushika, yaani ukipitishiwa tobo unachezea ngumi mpaka ulipate hilo jani ukilishika tu wanaacha kukupiga yaani ukipitishiwa inatakiwa ukimbie mpaka uupate mti wa aina hiyo au jani pembezoni mwa barabara ulishike.

Mchezo wa tatu ilikuwa niunafunikwa uso halafu tunachora mstari kwa chaki ndani ya darasa halafu wanaingia watu kama 20 hivi unaanza kuwakamata yaani ukimgusa tu mtu hata shati tu, anakuwa ametoka mchezoni au mtu akitoka nje ya mstari anakuwa ametoka mchezoni.

Hiyo ni baadhi tu ila ipo mingi sana

Sent from my tecno ca8 using jamiiforums mobile app
 
Tuambine ukweli mimi shule hakikuwa kitu changu.Hilo darasa nilikuwa naokota konokono mwambao wa ziwa Victoria.Mtoro sugu.
 
Back
Top Bottom