Ahsante kwa mleta mada hii(kisia) maana nimejifunza mengi sana juu ya mke. Mwanzo wa mada kisia amesemwa sana kama ametenda kosa kubwa sana (ni kweli) lakini ujio wa hawa wadada Ms. Lincoln, demi, Heaven Sent, miss chagga, Nalendwa, Evelyn Salt, ringson, espy, LadyRed, Msweet, Go mi num, firstLady 1,nao,...hakika,wanaume tuna la kujifunza na lazima tukubali kuwa sisi ni wajinga kiasi fulani. Hakuna haja ya kuombewa maana hicho ndio kilio cha wanawake wengi walio kwenye ndoa, tubadilike kwa hiari. Naona aibu hata kumuangalia wife tangu jana (kaa nami Bwana Yesu peke yangu siwezi). Mkuu Ngoda 95 na wengine tubadilike, tuwajali hawa viumbe. AMEN