Kuchepuka raha

kisia

Member
May 5, 2017
20
117
Toka niolewe miaka mingi tu toka niolewe sijawahi hata kuwaza kuna siku ntakuja kuchepuka, nilimpenda sana mume wangu.

Tatizo mwanaume huyu amekua jipu maana sio kwa umalaya huu na majibu ya karahaa. Hajawahi kuniambia samahani na mara zote nimemkuta na ushahidi na nilichokua nahitaji ni kuniambia samahani tu.

Ila kwanza ukimkuta kwanza ananuna hata mwezi hakusemeshi, hakugusi kosa lake ila ndio anakugeuzia wewe kibao.

Nimetafakari nikaona ya nini kujitia jakamoyo na mimi natongozwa. Nimejichukulia zangu mzigo loh! Si kwa raha hizi sijui hata nilichelewaga wapi mie!

Nimejiona mjinga kweli yaani baada ya kuchepuka nimekuja kujiona bonge la mjinga kumbembelezaga na kulilia kadudu kake kumbe kabamia hata hajui kitu kumbe!

Sasa hivi tunaenda sawa tu hakuna ugomvi raha tupu, asiponigusa nashukuru, zamani ningeumia. Asiporudi nyumbani naagiza soda nakunywa.
 
Hahahaaaa wazee wazamani usidhani walikuwa wanaishi mpaka wanafanana haya yalikuwa hayapo yalikuwepo, ila sasa hivi utandawazi tu mwanaume anaenda kuhemea kushoto mwanamke unaenda kupumuliwa kulia, mkikutana usiku mnageuziana migongo mkiamka asubuhi mnatoka vyumbani na nyuso za tabasamu, watoto wenyewe wanafurahiii baba na mama wanapendana, mkilala mkiamka mara miaka 3 ya ndoa, ukipindua miaka 10 , unajisemea niende wap bas mnaishi ila kila mmoja siri yake anavyoishi na mwezake.
 
Nadhani umefurahia tendo la ndoa si kwamba huyo mwanaume mpya anajua kufanya mapenzi no but ni vile upo na simanzi ukipata jawabu sahihi utarudi kwa mumeo, hujiulizi kwanini kabla ya malumbano na mumeo ulikuwa unafurahia mapenzi na mumeo? Nway kila lakher katika mahusiano ya memory card
 
Nimeshitushwa na Maneno yako! Wenzako wanachepuka wakiwa kwenye mahusiano na sio ndoa. Wacha nikukumbushe jambo, Ndoa ni kiapo kwa Mungu na uliapa mbele ya ndugu jamaa na wazazi wenu ukifanyacho leo kitaondoa baraka zote ndan ya nyumba yenu. Nendeni mkatubu!
 
Mama hebu leo usiku anza kusali tena mpe Mungu jukumu awarekebishe. Ukisali kumrudisha mume ama mpenzi aliyekengeuka ama kudangangika yataka uvumilivu yaweza chukua miezi hata 6. Rafiki yangu aliachana na mpenzi wake kisa kapa mchepukk/mpenzi mwingine alianza kusali neno lake kuu 'MUNGU WANGU NAJUA NILIMPENDA NA KUMUHESHIMU, NILIJITOA KWA DHATI ILA IKIWA NI MAPENZI YAKO BASI ARUDI ENDAPO HUKO ALIKO SIO MIKONO SALAMA' niliona huyu best ni chizi mwanaume kamsusia kampa kibuti akituma sms hajibu 6 months bado anaimani?? Kilichotokea yule kaka alikuja kumtafuta akaomba msamaha kabadilika dharau kaacha wameoana juzi
 
wanaume hapa wanakupinga sana,kisa umefanya wewe mwanamke ila angekua mwanaume mwenzao ndo kafanya hivi wangempongeza na kumwona mjanja.....
mama just do what makes you happy katika maisha yako ila tu uwe makini na magonjwa,yani kabinadam kamoja ndo kakukoseshe amani mtoto wa watu loh...u deserve better mama...
 
Mama hebu leo usiku anza kusali tena mpe Mungu jukumu awarekebishe. Ukisali kumrudisha mume ama mpenzi aliyekengeuka ama kudangangika yataka uvumilivu yaweza chukua miezi hata 6. Rafiki yangu aliachana na mpenzi wake kisa kapa mchepukk/mpenzi mwingine alianza kusali neno lake kuu 'MUNGU WANGU NAJUA NILIMPENDA NA KUMUHESHIMU, NILIJITOA KWA DHATI ILA IKIWA NI MAPENZI YAKO BASI ARUDI ENDAPO HUKO ALIKO SIO MIKONO SALAMA' niliona huyu best ni chizi mwanaume kamsusia kampa kibuti akituma sms hajibu 6 months bado anaimani?? Kilichotokea yule kaka alikuja kumtafuta akaomba msamaha kabadilika dharau kaacha wameoana juzi
Siku hizi umepata wapi?? Hii hekima mpenzi wangu mwajuma..!
 
Back
Top Bottom