utantambua
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,367
- 321
Dereva na abiria wote mabazazi, hawana ustaarabu hata chembe
Hua napenda sana baadhi ya style za karate kama vile Age-uke, Uchi-uke, gedan-zuki
Kiranga you are right, newsmen are not supposed to be part of a news stories unless they are the victims and in this case it ought to be reported by a third part to avoid biased reportage!.Sasa kama kamsamehe na hakupress charges nia ya kuandika ni nini?
Mwanahabari anatakiwa kutojifanya yeye kuwa habari unless it is absolutely necessary and there is a greater reason than one's own emotions and ego.
Angekuwa anaongelea elimu ya udereva na umuhimu wa madereva kudhibiti "road rage" ningemuelewa.
Angekuwa anasema kuna a grand political conspiracy against him kwa sababu kawaandika watu vibaya, na hili linaingilia uhuru wa waandishi wa habari, ningemuelewa.
Lakini sioni story. Naona kama vile anasema kamsamehe wakati bado hajamsamehe na ndiyo mana kamuumbua kwa jina.
Maggid, ukisamehe una move on. Ukirudia rudia palepale kwa kuandika andika kwenye mitandao story za mtu local hata hatumjui bila hata ya kum link na a greater narrative hujasamehe bado.
Unakuwa bado uko katika personal squabbles with the local village ignoramus ambaye anakuvamia kwa fist fight bila kujua kwamba unaweza kuwa na a fully loaded M16 pembeni ya kiti hapo. Ukamfyatua na ku claim self defense quite rightly.
Mi mara nyingi huwa against na huyu mtu, lakini kwa hili mleta maada umegeuka kuwa kama watangazaji wa klauz, Sasa kama barabara ilikuwa nyembamba alitakiwa afanyaje? Wat if angemruhusu afu Jamaa akasababisha ajali, ulitaka MjengwA achukue lawama? Acheni unazi usio na mantiki aseee..
kisa na mkasa cha mwaka champata Maggid Mjengwa
Ndugu zangu,Hizi si habari njema. Juzi alhamisi kunako saa kumi na mbili na nusu asubuhi nilipatwa na balaa la barabarani.Ilikuwaje? Niliondoka Iringa Jumatano jioni kuelekea kijijini kwetu Nyeregete. Nilifika Madibira, Mbeya jioni ya saa kumi na mbili na nusu. Kwa vile giza lilikaribia, nikaamua kulala kijijini Mahango, nyumbani kwa ndugu yangu aitwaye Salim Raphael Mjengwa.
Alfajiri tukaondoka pamoja maana naye alitamani kufika kijijini Nyeregete kumsalimu baba yake mzazi. Tukiwa katikati ya pori eneo la Ikoga kuelekea mji wa Rujewa nikabaini gari iliyokuwa ikija nyuma yetu kwa mwendo wa kasi.Nikamwambia ndugu yangu Salim juu ya uwepo wa gari nyuma yetu. Akaniambia kuwa ni basi dogo la abiria. Kupitia sight mirror nikamwona dereva wa nyuma yangu akijaribu kunipita mahali pasipostahili na kwa mwendo wa kasi. Kwa vile barabara ilikuwa ni nyembamba sana , basi, akalazimika kukatisha jaribio la kunipita.Baada ya mwendo wa nusu kilomita hivi nikapaona mahali muafaka pa kuegesha gari yangu pembeni kumruhusu apite.
Nikawasha indiketa, nikaweka gari yangu pembeni.Dereva yule akapita na kusimamisha gari yake katikati ya barabara. Akatoka kunifuata. Nami nikaanza kujiandaa kufungua mlango na mkanda wangu ili nitoke tuongee.Kabla hata sijafungua mlango, yeye akauvuta mlango wangu na kunishambilia kwa ngumi usoni. Nikainamisha uso wangu kwenye usukani. Nikasikia pia ndugu yangu Salim akitamka; " Seme unafanya nini?" Salim alimfahamu kwa jina dereva huyo, anaitwa Seme. Mara, dereva mwenzangu akaacha kunishambulia na kunitukana.
Nikainua kichwa. Nikamwona akiondoka huku kundi la vijana waliokuwa abiria wake nao wakirudi kwenye gari lao. Walikuja kushiriki shambulizi dhidi yangu.Walikuwa na dhamira mbaya sana. Kama si uwepo wa ndugu yangu Salim ambaye wote walimtambua hadithi ingekuwa nyingine.Tulipofika Rujewa nikaripoti tukio hilo kituo cha Polisi Mbarali. Dereva mwenzangu naye akafika kituoni. Afande Mwamakula, ambaye ni mkuu wa kituo aliweka wazi kuwa alichofanya dereva yule ilikuwa ni jinai.Kwa vile nilihitajika kufika kijijini kumwona mgonjwa aliye taabani.
Na kwa vile nilihitajika kurudi Iringa kupokea ugeni kutoka Ubalozi wa Sweden. Na kwa vile dereva yule alikiri kosa lake na kuniomba radhi. Na kwa vile dereva yule aliweka wazi kuwa ni msomaji wa makala zangu, basi, nikaamua kutoendelea na shauri lile. Nilimsamehe kwa kumwambia; hupaswi kufanya tendo kama lile kwa mtu yeyote yule. Ule haukuwa uungwana.
Wenu,Maggid Mjengwa,Iringa.
Title na habari vinaonyesha mleta mada umeileta kiunafiki na kimbea kutulazimisha tumuone Maggid mbaya na tumshambulie
May be i miss something here, hebu unganisha dot hilo la fundisho kwa waandishi kanjanja na matukio ya ugonvi wa barabarani