Kuchapwa kwa Maggid Mjengwa ni fundisho kwa waandishi KANJANJA?

Pole sana Majjid lakini umefanya kosa kwa kuli undermine hilo tukio, inawezekana siyo yeye bali anatumiwa na mtandao. Nakushauri uwe makini sana na watu dizaini hiyo, halafu unatakiwa uwe na hisia endapo mtu anakufuafilia ushituke na ujue nini cha kufanya mapema.
 
Sasa kama kamsamehe na hakupress charges nia ya kuandika ni nini?

Mwanahabari anatakiwa kutojifanya yeye kuwa habari unless it is absolutely necessary and there is a greater reason than one's own emotions and ego.

Angekuwa anaongelea elimu ya udereva na umuhimu wa madereva kudhibiti "road rage" ningemuelewa.

Angekuwa anasema kuna a grand political conspiracy against him kwa sababu kawaandika watu vibaya, na hili linaingilia uhuru wa waandishi wa habari, ningemuelewa.

Lakini sioni story. Naona kama vile anasema kamsamehe wakati bado hajamsamehe na ndiyo mana kamuumbua kwa jina.

Maggid, ukisamehe una move on. Ukirudia rudia palepale kwa kuandika andika kwenye mitandao story za mtu local hata hatumjui bila hata ya kum link na a greater narrative hujasamehe bado.

Unakuwa bado uko katika personal squabbles with the local village ignoramus ambaye anakuvamia kwa fist fight bila kujua kwamba unaweza kuwa na a fully loaded M16 pembeni ya kiti hapo. Ukamfyatua na ku claim self defense quite rightly.
Kiranga you are right, newsmen are not supposed to be part of a news stories unless they are the victims and in this case it ought to be reported by a third part to avoid biased reportage!.

Namheshimu sana Maggid esp his frankness ila kwa story hii sijapata the motive behind wala the subject matter!. Pole Maggid kwa fungua mwaka ya maswahib hayo, utaufunga mwaka vizuri!.
 
Traffic regulation Act inasemaje kwa huyu mtu kutandikwa hivyo? What was the reason behind the scene of incident?
 
Mi mara nyingi huwa against na huyu mtu, lakini kwa hili mleta maada umegeuka kuwa kama watangazaji wa klauz, Sasa kama barabara ilikuwa nyembamba alitakiwa afanyaje? Wat if angemruhusu afu Jamaa akasababisha ajali, ulitaka MjengwA achukue lawama? Acheni unazi usio na mantiki aseee..:(

Watangazaji wa clous wakoje tena? Au ndo hawa wanasema hawana tofauti na wapiga debe
 
Siku nyingine utafia kwenye usukani. Jamaa anaku-Tyson wewe unajiinamia utakufa nyambaf.. Mjomba hata kama hujui kusumbwilise inabidi ujikakamue! Ila mleta habari hajatutendea haki kwa hicho kichwa cha habari!
 
Angekuwa amemsamehe jamaa wala asingekuja kupoteza muda wote kuandika haya.
 
images

kisa na mkasa cha mwaka champata Maggid Mjengwa


Ndugu zangu,Hizi si habari njema. Juzi alhamisi kunako saa kumi na mbili na nusu asubuhi nilipatwa na balaa la barabarani.Ilikuwaje? Niliondoka Iringa Jumatano jioni kuelekea kijijini kwetu Nyeregete. Nilifika Madibira, Mbeya jioni ya saa kumi na mbili na nusu. Kwa vile giza lilikaribia, nikaamua kulala kijijini Mahango, nyumbani kwa ndugu yangu aitwaye Salim Raphael Mjengwa.

Alfajiri tukaondoka pamoja maana naye alitamani kufika kijijini Nyeregete kumsalimu baba yake mzazi. Tukiwa katikati ya pori eneo la Ikoga kuelekea mji wa Rujewa nikabaini gari iliyokuwa ikija nyuma yetu kwa mwendo wa kasi.Nikamwambia ndugu yangu Salim juu ya uwepo wa gari nyuma yetu. Akaniambia kuwa ni basi dogo la abiria. Kupitia sight mirror nikamwona dereva wa nyuma yangu akijaribu kunipita mahali pasipostahili na kwa mwendo wa kasi. Kwa vile barabara ilikuwa ni nyembamba sana , basi, akalazimika kukatisha jaribio la kunipita.Baada ya mwendo wa nusu kilomita hivi nikapaona mahali muafaka pa kuegesha gari yangu pembeni kumruhusu apite.


Nikawasha indiketa, nikaweka gari yangu pembeni.Dereva yule akapita na kusimamisha gari yake katikati ya barabara. Akatoka kunifuata. Nami nikaanza kujiandaa kufungua mlango na mkanda wangu ili nitoke tuongee.Kabla hata sijafungua mlango, yeye akauvuta mlango wangu na kunishambilia kwa ngumi usoni. Nikainamisha uso wangu kwenye usukani. Nikasikia pia ndugu yangu Salim akitamka; " Seme unafanya nini?" Salim alimfahamu kwa jina dereva huyo, anaitwa Seme. Mara, dereva mwenzangu akaacha kunishambulia na kunitukana.

Nikainua kichwa. Nikamwona akiondoka huku kundi la vijana waliokuwa abiria wake nao wakirudi kwenye gari lao. Walikuja kushiriki shambulizi dhidi yangu.Walikuwa na dhamira mbaya sana. Kama si uwepo wa ndugu yangu Salim ambaye wote walimtambua hadithi ingekuwa nyingine.Tulipofika Rujewa nikaripoti tukio hilo kituo cha Polisi Mbarali. Dereva mwenzangu naye akafika kituoni. Afande Mwamakula, ambaye ni mkuu wa kituo aliweka wazi kuwa alichofanya dereva yule ilikuwa ni jinai.Kwa vile nilihitajika kufika kijijini kumwona mgonjwa aliye taabani.

Na kwa vile nilihitajika kurudi Iringa kupokea ugeni kutoka Ubalozi wa Sweden. Na kwa vile dereva yule alikiri kosa lake na kuniomba radhi. Na kwa vile dereva yule aliweka wazi kuwa ni msomaji wa makala zangu, basi, nikaamua kutoendelea na shauri lile. Nilimsamehe kwa kumwambia; hupaswi kufanya tendo kama lile kwa mtu yeyote yule. Ule haukuwa uungwana.

Wenu,Maggid Mjengwa,Iringa.

Unawaza ufisadi tu...sasa hapa ukanjanja unakujaje?!!! yani nyie maccm mnawaza wizi tu..ovyooo...
 
Hiii inaweza sababisha ajali kama tena kwa watu wengi ..kama dereva wa basi alikuwa anahitaji ku cut you off na wewe una speed up ati kwa lengo la kwamba asifanye hivyo ni hatari.Kama alivyo fanya kuwasha indicator na kumpisha ndio akngefanya kumtaadhalisha asipite kwa kuwasha indicator ya upande mwingine ndio usilikiano barabarani .Ingawa na huyo dereva basi naye hakutakiwa kupeleka ngumi...
 
Madereva kama hao wapo wengi sana. Huyo alikuwa hafai kusamehewa angekwenda ndani akajifunze heshima na adabu.
 
too trivial a stuff to get this publicity.

kwa bahati mbaya na jf inajikuta inakuwa trivial kwa kuruhusu mediocrities za jinsi hii ku-feature humu.
trivial stuff like this should stay where they belong.......the likes of mjengwa's blogs!

this is my last contribution on this thread. i expect many volunteers - a lasting measure to stamp out triviliaties hapa jf.
 
Title na habari vinaonyesha mleta mada umeileta kiunafiki na kimbea kutulazimisha tumuone Maggid mbaya na tumshambulie
May be i miss something here, hebu unganisha dot hilo la fundisho kwa waandishi kanjanja na matukio ya ugonvi wa barabarani

Hangover!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom