Ndoto gani uliwahi kuota ikakufikirisha sana?

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,160
11,483
Nilijikuta niko kwenye nyumba yenye njia kama barabara ya kwenda underground floor (basement hivi). Kuta za hiyo nyumba zilipakwa rangi ya yellow (njano) na nilivyopiga kama nusu mzunguko niliona ukutani kulikuwa na picha ya nyoka mkubwa kichwa kama kilikuwa juu kama kwanye ground-floor kwa vile sikukiona na urefu wake uliipotelea mpaka chini ya hiyo nyumba (niliona kama sehemu ya tumbo lake hivi). Basi, nilienda kutelemka taratibu mpaka chini kukamilisha mzunguko hivi na pembeni ya njia kulionekana watu wamesima wakinitizama. Ghafla! Ile picha ya nyoka ikaoneka inabadilika na kubakiwa mbavu na mifupa kuashiria kama ana njaa anataka kula!!?? Duh! Nikashtuka nikaanza kukimbia na kurudi kutoka kwenye shimo ambapo wale watu waliokuwa pembeni wakaanza kuja kwangu kwanguvu kutaka kunishika ili wanitupe ndani (sijui niliwe??)! Wakashangaa kila wakijaribu kunishika kwa nguvu zao zote na kwa umoja wao nilikuwa na nguvu kuwashinda! Nikakimbia saana kutoka ndani ya eneo la hilo jengo mpaka nikakutana na lango kubwa (gate). Basi, hao watu wakaanza kunidhiaki kuwa hapa hawezi kupita hata hakifanyaje! Nikaomba "damu ya Yesu nena na malaika sasa hivi iniletee malaika wanitoe hapa". Basi huku nikikimbilia Gate nikalipita katikati bila lenyewe kufunguka jamaa wakashangaa!! Basi! Hile nakimbia nikaona gari katika uwiano wa spidi yangu na hiyo gari ilionekana gari lilikuwa na spidi kuliko mimi na aliyekuwa analiendesha kafunguka mlango na kunishika mkono na kuendelea kukimbia huku kama nimeninginia mlangoni kwasababu hakukuwa na muda wa kupunguza spidi! Wakati nimepita kwenye Gate nilisikia amri ikitolewa ya aina fulani ya majeshi yanikimbize na kunikamata na yalionekana kuwa na nguvu nyingi na spidi kubwa ndo maana hilo gari lililokuja kunichukua halikupunguza spidi. Waliendelea kutufukuza mpaka tukawaacha! Nakumbuka nilianza kumuelekeza yule dereva ninakokaa! Basi! Pale kwangu kuna nguzo kubwa ya nondo na zege kali kuzuia gari zisigonge nyumba yangu kwasababu nimejenga karibu na barabara! Lile gari lilikuwa na matairi mapana na marefu kama trekita hivi na katika ndono ilionekana tunaenda spidi ya kawaida, ila nilikuja kujua tulikuwa tunaenda spidi kubwa kwasababu nilipokaribia kwangu nilimwambi kwangu hapa nimefika ambapo yule dereve alikanyaga breki na kuligongesha taili kwenye hiyo nguzo ya zege kiasi kwamba lilibonyea kiasi cha taili kushikana na rimu (kuonyesha kwa jinsi gani tulikuwa spidi). Nilivyofika nyumbani nikaamka usingizini. Kusema ukweli ndoto hii ilikuwa clear bila chenga kiasi kwamba hiyo nyumba ya nyoka mtu akinipeleka naweza kuitambua. Hii ndoto huwa siisahahu japo miezi kadhaa imepita!
Je! Wewe ulishawahi ota ndo dhahiri kama hii?
 
nimeota hivi karibuni nikmuona huyu mwamba wa unyiramba ,anayesimamia hazina yetu akiwa anang'ara
sijui atang'ara kwenye nini
 
Watu wanachukulia poa ndoto wakati ndoto ni dhahiri! Kuna jamaa aliota ndoto akigongwa na nyoka (kwenye ndoto) katika kidore gumba cha mguu wake wa kulia. Akiwa kwenye ndoto kasikia maumivu makari hadi kaamka! Akawasha taa na kuangalia kidore kakuta mahari alipogongwa kunatoka damu! Akawaita watu wa karibu yake wakampeleka kanisani wakamuombea sana! Baada ya hapo, maisha yake kiuchumi na kiafya yalibadilika saana maana alifilisika na kuandamwa na magonjwa! Bila kuishi maisha ya maombi kwa wale wanaomtegemea Mungu, hutoboi!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom