Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Ndugu zangu tuache mzaha. Mjadala huu si mdogo. Majengo ya kihistoria kama haya ni vitu muhimu sana kwa kizazi kijacho. Tukiendekeza bomoa bomoa hii si ajabu hata ikulu ikabomolewa. Hii ni dhambi ya kihistoria.
Mbona Tanganyika ilivunjwa? wavunje tu ili tulisahau hili jinamizi!
 
Moja ya masomo niliyoyapenda ni Historia. Historia inatusaidia kujua tulikotoka, tulipo; na kwa maana hiyo tunaweza kupanga aina ya maisha yatu ya baadaye. Jengo la TANU Mtaa wa Lumumba- mahali palipotumiwa na waasisi wa Taifa letu kuanzisha chama hicho cha ukombozi, sasa linabomolewa. Binafsi, naiona hii ni dhambi ya kihistoria.

Umuhimu wa jengo hilo haupo kwa wana CCM pekee, bali kwa Watanzania wote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hapo ndipo wazee wetu walipokutana na kuanzisha chama ambacho baadaye kiliongoza mapambano ya kumng'oa mkoloni Mwingereza. Naamini kwa dhati kabisa kuwa jengo hilo si mali ya CCM kama chama, bali ni jengo la Watanzania wanaoheshimu historia ya Taifa lao.

IMG_4947.JP

​

Sikuona sababu za msingi za kubomolewa jengo hilo na kujengwa kitu kingine eti kitega uchumi. Makosa haya ya kubomoa majengo ya kihistoria yanashamiri. Tumeshuhudia jengo la Salamander likivunjwa. Jengo la Forodhani ambako sasa kuna Mahakama ya Rufani, ndilo lilitumiwa kama hoteli ya kwanza katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa siku za karibuni kuna mipango madhubuti ya kulivunja ili kupisha upanuzi wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski! Jengo la pale Magomeni ambalo kulikuwa na chumba kilichotumiwa na Mwalimu Nyerere alipojiuzulu ualimu, limevunjwa. Jengo hilo kwa hakika ndipo mahali ambako Mwalimu alitumia muda wake wote kuandaa maandiko na mikakati mbalimbali ya ukombozi wa nchi hii. Watawala wetu hawakuona umuhimu wake, wamelibomoa.

Ndugu zangu, nimezuru nyumba za kihistoria kama ile ya Keneth Kaunda kule Zambia na nyumba ya Nelson Mandela, Soweto Afrika Kusini. Nyumba zile zimeachwa katika uhalisia wake kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vijavyo. Kinachofanywa ni ukarabati tu ambao haupotezi maaana wala asilia ya nyumba husika.

Kubomolewa kwa Jengo la TANU, Mtaa wa Lumumba ni kosa kubwa kihistoria. Walioamua jambo hilo hawawatendei haki Watanzania wa miaka ijayo. Pengine mambo kama haya yanayokuwa kwenye fikra za watu fulani fulani ni vema ukawapo mjadala mpana ili kusikia Watanzania wanasema nini.

Ubomoaji majengo ya kihistoria ni dhambi kihistoria.

Jamani mbona hata jengo lililokuwepo kabla ya kuvunjwa siyo lenyewe? Jengo halisi lilivunjwa kitamba sana
 
Kubomoa majengo ya kihistoria ni kupoteza historia na kuua utalii (town tourism). Kama assumption ya Pasco kwamba labda wanataka kujenga replica ni sahihi sina tatizo na kuvunjwa hilo jengo. Lakini ni majengo mangapi yamevunjwa halafu yakajengwa mengine kwa mfano uleule? Mara nyingi majengo haya yanapovunjwa ujue kuna mwenye pesa anahitaji hilo eneo kwa ajili ya uwekezaji kibiashara
 
Mkuu sina chuki na kaka Manyerere Jackton. Hata yeye anajua. Tumekaa wote Kijitonyama miaka ileeee. Yeye alipanga banda la uani kwenye nyumba ya babu na bibi waliokuwa wanapendana sana.
Manyerere nimeshiriki nae vikao vya kutaka kujaribu kuihujumu Chadema pale soma book cafe pale mikocheni pamoja na omarilyasi. Nilipogundua kuwa vikao vile ni vya kupanga mkakati wa kuiua chadema nilitimka hata sikuaga. Manyerere anajua kuwa namwelewa sana. Hivi karibuni alikuja ofisini kwangu kuomba tuweke tangazo la biashara kwenye kijarida chake cha JAMHURI kinachofadhiliwa na jamaa yake yuleee.... Mi nilimkwepa hakuniona lakini hadi PRO alimpuuza. Mimi nilimkwepa kuogopa kupigwa mzinga. Otherwise Manyerere Jackton ni kaka yangu, swahiba wangu na ni best yangu ingawa yeye ni mwana CCM maslahi na mimi ni Kamanda wa ukweli wa Chadema. Asante

Ndugu zangu mnaosoma hapa JF, huyu mpuuzi anataka kuni provoke na kutaka kuniharibia heshima yangu. Sijawahi kuishi Kijitonyama katika banda ya uani. Sijawahi kushiriki kikao chochote cha kuihujumu Chadema, na wala sina mpango wa kijinga wa aina hiyo. Sijawahi kwensa chombo chochote kuomba JAMHURI litangazwe kwa sababu naamini Jamhuri limejitangaza lenyewe vya kutosha. Huyu mpuuzi anayesema nilikwenda kumpiga mzinga ni uongo kwa sababu vijisenti vya kubadili mboga na mafuta kwenye escudo yangu ya mwaka 1998 ninavimudu. Naomba mchukulie taarifa hii kuwa ni uongo na kutaka kunichafua mbele ya maelfu ya Watanzania wanaotambua na kuheshimu mchango wangu hasa kwenye suala la demokrasia na utawala bora.
 
Ni vizuri umekuja kujibu hii tuhuma
 
Nakubaliana ulicho-ripoti... Jengo la TANU na Salamander... Ila ndugu yangu nyumba ya Nyerere Magomeni iko Chini ya makumbusho ... In fact kuna mabango barabarani siku hizi yanaelekeza iliko nyumba yenyewe. Nyumba hiyo haijavunjwa. Manyerere Jackton
 
Last edited by a moderator:
BELIZE CITY -- A construction company has essentially destroyed one of Belize's largest Mayan pyramids with backhoes and bulldozers to extract crushed rock for a road-building project, authorities announced on Monday.
The head of the Belize Institute of Archaeology, Jaime Awe, said the destruction at the Nohmul complex in northern Belize was detected late last week. The ceremonial center dates back at least 2,300 years and is the most important site in northern Belize, near the border with Mexic
o-MAYAN-PYRAMID-DESTROYED-570.jpg

belize-mayan-pyramid.png

Kim, ndio maana wamesema destruction was noted! it was not demolition? inawezekana huyo mkandarasi hakujua! lakini mwenye akili timamu na msomi yeyote anayejua kuna kitu kinaitwa heritage ' tunu'. hawezi kubiashania upuuzi kama huu.
 
Historia ya TANU wala sio historia ya CCM. Ni vitu viwili tofauti kabisaa! Mnipatie TANU any time - lakini sio hicho kingine!
 
Ndugu zangu tuache mzaha. Mjadala huu si mdogo. Majengo ya kihistoria kama haya ni vitu muhimu sana kwa kizazi kijacho. Tukiendekeza bomoa bomoa hii si ajabu hata ikulu ikabomolewa. Hii ni dhambi ya kihistoria.

Mi naungana nawe, hii sii tu kwa kizazi ni ajira kubwa sana duniani! ulaya hawana utalii mkubwa isipokuwa wa heritage, hususani majengo! hapo wameua ajira kama kwa wale wasiojua, kuna ajira nyingi sana. Kuanzia engineering mpaka historians. Wenzetu likichakaa jengo wanaitwa conservation engineers, conservation architects, conservation historians, curators, tour guides, archaeologists nk. Sasa hizi shule zao za kata wakifaulu hao watu watakwenda wapi? Ni aibu kubwa! Ndio maana ajira zimebaki polisi, PCCB, magereza, uhamiaji, ualimu? halafu watuambie hakuna ajira! Sina maneno ya kuongea lakini nasikitika kuzaliwa Tanzania ya CCM.
 
Ndugu zangu mnaosoma hapa JF, huyu mpuuzi anataka kuni provoke na kutaka kuniharibia heshima yangu. Sijawahi kuishi Kijitonyama katika banda ya uani. Sijawahi kushiriki kikao chochote cha kuihujumu Chadema, na wala sina mpango wa kijinga wa aina hiyo. Sijawahi kwensa chombo chochote kuomba JAMHURI litangazwe kwa sababu naamini Jamhuri limejitangaza lenyewe vya kutosha. Huyu mpuuzi anayesema nilikwenda kumpiga mzinga ni uongo kwa sababu vijisenti vya kubadili mboga na mafuta kwenye escudo yangu ya mwaka 1998 ninavimudu. Naomba mchukulie taarifa hii kuwa ni uongo na kutaka kunichafua mbele ya maelfu ya Watanzania wanaotambua na kuheshimu mchango wangu hasa kwenye suala la demokrasia na utawala bora.

hata ccm yenyewe iko vipande vipande,imevunjwa siku nyingi,sasa ofisi ibaki ya nini?
 
Ndugu Manyerere Jackton, ulichokiandika hapa ni ile +20% watakaoweza kukuelewa na nina mashaka kama wengine watakuelewa. Hii 20% ndio waliotaka vyama vingi, ndio kura zao hazikuwa kati ya 80% ya uchaguzi wa 2005, ndio inayotaka serikali 3, ndio pamoja na wengine wanaelewa uzuri wa rasimu ya pili ya Katiba ya Jaji Warioba, nk, nk.

Ni wachache sana kuwa pamoja na mambo mengine, wanaelewa kuwa kuna mkakati wa kubadilisha mkondo wa historia ya nchi hii bila kuelewa ugumu wa hilo swala. Nitasikitika sana pia kama na ubomoaji wa hili jengo itakuwa ni sehemu ya mkakati huo japo maana itabaki pale pale. Hata lile jengo lingine lililojengwa pembeni ya ofisi ndogo inaonyesha hiki chama kilivyoshindwa kuilinda historia na heshima ya nchi hii. Walishindwaje kukichukua kile kiwanja na kukifanya hata open space badala ya kumwachia mtu ambaye hata wakiwa kwenye vikao anawachungulia ...japo haishangazi maana lingine limejengwa mkabala na ikulu!

Kwa kasi hii ya 'ubadilishaji' wa mji, waigeleza wangelifuata 'akili' zetu basi Westminister ingelikuwa imejengwa maduka kama yaliyotaka kuzungushwa Mnazi Mmoja wakati ule!
 
Nakubaliana ulicho-ripoti... Jengo la TANU na Salamander... Ila ndugu yangu nyumba ya Nyerere Magomeni iko Chini ya makumbusho ... In fact kuna mabango barabarani siku hizi yanaelekeza iliko nyumba yenyewe. Nyumba hiyo haijavunjwa. Manyerere Jackton
Da, ama kweli somo la historia ni muhimu. Nyumba ambayo ni makumbusho ni ile iliyojengwa na mwalimu. Nazungumzia ile ya serikali ya wakoloni ambayo alipanga punde tu baada ya kuacha ualimu. Ipo ubavuni mwa ofisi za TLP mbele ya kituo cha polisi magomeni.
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco
Hii ni update ya Mwenezi wa CCM!
​
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza kwenye ofisi ya gazeti la Jambo leo ikiwa sehemu ya ziara yake kwenye vyombo vya habari.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amesema CCM haiwezi na wala haina mpango wa kupoteza historia ya mahali ilipozaliwa TANU.

Alifafanua kuwa awali ofisi ya mwanzo ilikuwa nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa makuti, kisha ikaondolewa makuti na kuezekwa mabati ya madebe,baade ikabadilishwa na kuwekwa bati za kisasa.

Alisema kama tusingefanya maboresho maana yake tungekuwa na jengo la udongo ambalo limeezekwa makuti mpaka leo. Akadai wanaolalamika hawajui historia ya eneo hilo, ila akawashukuru kwa mapenzi yao mema kwa Chama hicho
Pasco
 
Da, ama kweli somo la historia ni muhimu. Nyumba ambayo ni makumbusho ni ile iliyojengwa na mwalimu. Nazungumzia ile ya serikali ya wakoloni ambayo alipanga punde tu baada ya kuacha ualimu. Ipo ubavuni mwa ofisi za TLP mbele ya kituo cha polisi magomeni.
Asante kwa Hilo somo but it seems hiyo hawaku-eye mark Kama ni ukumbukwe else wangefanya Kama hiyo nyumba yake... We must have some sort of limit else kila sehemu alikopita tutasema ni makumbusho.
 
Asante kwa Hilo somo but it seems hiyo hawaku-eye mark Kama ni ukumbukwe else wangefanya Kama hiyo nyumba yake... We must have some sort of limit else kila sehemu alikopita tutasema ni makumbusho.
Sijui unalenga nini. Tunachojadili hapa ni umuhimu wa maeneo ya kihistoria. Hayo yapo kwa wenzetu na yanaheshimiwa. Hoja hapa ni kwamba kila kitu au kila mahali. Kwa mfano, unapoambiwa hapa ndipo muasisi wa Taifa hili alipolala wakati wa harakati za kudai Uhuru, hapo ni historical site! Sehemu walipozaliwa wazee wetu wengi walioshiriki harakati za Uhuru ni vema yakatambuliwa na kutunzwa. Ukienda katika makumbusho katika mataifa mengine, utaona kabisa kuwa sisi hapa tunatania. Maeneo ya kihistoria ni sehemu za kiuchumi.
Nimezungumza na Nape Nnauye, amesema kuna taarifa inaandaliwa-ya ufafanuzi- kuhusu hili jengo la TANU, Lumumba.
 
Ndugu zangu mnaosoma hapa JF, huyu mpuuzi anataka kuni provoke na kutaka kuniharibia heshima yangu. Sijawahi kuishi Kijitonyama katika banda ya uani. Sijawahi kushiriki kikao chochote cha kuihujumu Chadema, na wala sina mpango wa kijinga wa aina hiyo. Sijawahi kwensa chombo chochote kuomba JAMHURI litangazwe kwa sababu naamini Jamhuri limejitangaza lenyewe vya kutosha. Huyu mpuuzi anayesema nilikwenda kumpiga mzinga ni uongo kwa sababu vijisenti vya kubadili mboga na mafuta kwenye escudo yangu ya mwaka 1998 ninavimudu. Naomba mchukulie taarifa hii kuwa ni uongo na kutaka kunichafua mbele ya maelfu ya Watanzania wanaotambua na kuheshimu mchango wangu hasa kwenye suala la demokrasia na utawala bora.

Manyerere Jackton nakuhifadhi ili usipate sababu ya kusema nimekuharibia uzi. Ila najua unaelewa kuwa nakufahamu in and out. Kuhusu kuihujumu Chadema hilo hatabutokwe povu namna gani hata viongozi wa chadema wanajua. Gazeti unalodai ni lako tunajua anayelifadhili. Na kwa nchi hii ilivyo hatapata urais hata akitambika uchi hadharani. Sijakuprovoke ila ukweli ni kuwa maandishi yako mengi husukumwa na TUMBO. Akili huwa imesinzia
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco
pasco sidhani kama manyerere kakuelewa. jibu lake limenichekesha sana. inaonesha kabisa jamaa sio. waliokuelewa kama akina the Boss wamekuwekea like.
 
Back
Top Bottom