Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Nyumba inavunjwa na kuanza kujenga upya lakini mwenezi anasema ukarabati wa kawaida.

Lugha ya Taifa inazidi kubomolewa na yenyewe.
 
Ujue hapo ndio laana inapoanzia. Lile jengo lilistahili kubakia lilivyokuwa karne na karne! Vizazi vijavyo vifunge safari kutoka mikoan kuja kuona TANU (UKOMBOZI) ilipoanzia.

Ulianzia hapo ila naona kama unahamia kinondoni sasa...
 
Ni mfumo wa vyama vingi, sina uhakika kama watanzania wenye itikadi tofauti za vyama wanahitaji kuwa na kumbukumbu ya Jengo la chama kimoja.
mkuu, ni historia ya nchi. jengo lingeweza kuhifadhiwa likatafutwa eneo lingine.
 
Kweli kabisa, mimi ningewaelewa wanaopinga kubomolewa kwa jengo hilo kama wangependekeza lisiwe la CCM kwanza ili historia yenyewe iwe na maana wakati ambao nchi inafuata mfumo wa vyama vingi, lakini kama wanakubaliana ni jengonla CCM sioni tabu kama wameamua kulivunja.
historia inaonyesha kuwa kuna wakati CCM ilikuwa ni ya watanznia wote. majengo yote ya wakati huo yalikuwa mali ya watanzani kwa hiyo yakipewa heshima ni jambo jema
 
It is unfortunate - nafikiri kuna "mwekezaji" mkubwa anayeheshimiwa kapewa tenda hapo. Tanzania hatujui kuliachia historia
 
Ni kweli usiopingika kuwa historia ya jengo hili ingeweza kuhifadhiwa halafu hicho kitega uchumi kikajengwa eneo lingine,..kwa sababu Tzania sio kama Hong ambao hawana hata ardhi ya kuzikia!..
 
....Hii ni dalili ya KUBOMOKA kwa CCM!
Tusubiri WABOMOE jengo lilipozaliwa Azimio la Arusha hapo Kaloleni.... Hawana kitu hawa. Eti Chipukizi wanaowatumia katika halaiki za chama ni WATOTO wa WANACHAMA wa CCM.... Haya anayasema Kiongozi wa Serikali Bungeni! Tuna watu hapa? Wabomoe....Waache wabomoe wabomoke!
 
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco

And it will remain so,wewe unafikiri hao wana akili kama zako, kwani pale Magomeni wamefanyaje,kinachoangaliwa pale ni financial gain,hiki ni kipindi cha lala salama its now or never.
Nadhani juzi ulimsikia mkulu mwenyewe anatamka kwamba atahakikisha kura ya Katiba inayopendekezwa inafanyika kabla hajang'atuka,pamoja na kwamba muda hauruhusu kura kufanyika.
Elewa kinachoandaliwa sasa hivi ni kuzikomba za mwisho kupitia zabuni za kifisadi.
 
halafu utaona wabunge wanaandaliwa ziara na nhc kwenda uturuki wakirudi wanakusifia hawajui kuwa sifa kubwa ya uturuki ni kuhifadhi majengo yake ya zamani bado lumumba nafikiri watabomoa muda wowote maana wameliacha limekuwa kama gofu
 
Hili suala limenifanya kuona kwa Tanzania hao wanaojiita wapinzani na wanaharakati ni wachumia TUMBo tu, Historia ya TANI sio ya CCM pekee bali ni ya nchi nzima, leo hii utamuonesha wapi mwanao zilipo zaliwa siasa za nchi yake?....
 
Yani Watanzania tuna akili za ajabu kweli!!! Mtu mzima kabisa na watoto nyumbani unashinda mitandaoni eti kutetea majengo machakavu kisa tu "kulinda historia!!!"

Historia gani hiyo ya kulindwa isiyokuwa na maslahi mapana kwa taifa!? Nchi zingine zenye watu wenye akili hulinda tu zile historia mahususi za kuingizia taifa mapato ili serikali zao zizidi kutoa huduma kwa wananchi. Hapa kwetu eti tunataka kulinda majengo machakavu yaliyo katika maeneo "prime" kisa tu kutunza kumbukumbu za ukombozi!!! Is this for really!

Hivi ni kweli vichwa vyetu vinajali sana historia kuliko kuendana na ulimwengu na mabadiliko yake? Newyork, Dubai, Taipei, Tokyo na Abu Dhabi huko kote zilifanyika controlled demolition ili kupisha skycrapers kujengwa kwa maendeleo mapana ya taifa. Hapa kwetu mtaa wa Lumumba ukiguswa utasikia wahuni wachache wanaanza kulia lia mara historia mara sijui nini!

Kama kweli wewe mleta mada unajali historia basi ungefanya utafiti kujua aina ya chupi aliyokuwa akivaa babu kizaa babu yako ili na wewe uiendeleze kuivaa na pia kuwarithisha wajuu zako.
 
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco


PASCO Lile Jengo lilikuwa imara tena Sana ....,Mamyerere nakubaliana na wewe na katika LAANA kubwa anayo acha JK ....nikubomoa Jengo Hilo ...unajua dalili Za kufa ...au sikio la kufa halisikiii dawa .....ccm wamevuna LAANA kubwa sana...
NA UKISIKIA ALIYEWASHAWISHI WAVUNJE WAINGINE UBIA NI YULE YULE ........MWARABU KIPENZI CHA FAMILIA KUBWA ...NA ALIYEELETA KILIO BANDARINI ...
Nadhani soon ataihamisha kabisa ccm pale Baada ya kuwa ameshajenga ghorofa jirani pale ...

TUSUBIRI HALMASHAURI KUU YA CHAMA NA WAASISI WA CHAMA .CCM..WATASEMAJE JUU YA HILO
 
Nadhani kwenye hili tumekosea. Hizo nchi zote zilizotajwa hazijawahi kubomoa majengo yenye historia
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!

Tena na kwenye kaburi lake ndipo wamejengelea na zizi la kondoo/mbuzi!!

Hahahaa! shida sana mambo haya.
 
Ban inanukia hapa.

Hawa CCM ni washamba, wapumb*vu na wash*nzi kupindukia. Yani hawa watu tukiendelea kuwatizama, kuna siku wata bulldoze Ikulu yote. Na ule mwenge wa uhuru muda si mrefu wataufyekea mbali ili wajenge kitega upumbavu wao

Majengo ya kihistoria yote wamekaribia kuyamaliza mjini, sasa wameanza kubomoa historia wanayoisimamia wao wenyewe.

Ndio maana Transparency ni muhimu sana kwenye hii nchi, ndio njia pekee ya kuwakumbusha hawa washamba umuhimu wa vitu vya msingi. Mnaitengea wizara ya utalii mabilioni ya kutangaza utalii na historia yetu nje ya nchi wakati vitu vilivyotakiwa viwe sehemu ya historia hiyo mnaviondoa.

Umaskini wa fikra kitu cha hovyo sana, yani hawa vichwa maji wa Lumumba wanafikiria ule m-concrete jungle wa morogoro road ndio jengo la kisasa? na majengo ya kisasa yaseme nini?

Uingereza, Ufaransa, Hispania, Italia combined zinapokea watalii wasiopungua milioni 300 kwa mwaka na sababu kuu ni kuitunza historia yao.

Sehemu kubwa ya majengo ya italia yako kwenye Ruins stage lakini bado wanayatunza.

I am really upset by this.
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!


USA keep all their COUNTRY HISTORY na HIYO ILIPATA UHURU 1770
 
Kuna ambalo umewahi kuwaunga mkono katika maamuzi wanayofanya wenyewe! Tena wazee wa mujini walitoa wakfu na ktk hizo mnazoita historia hata kuwakumbuka mnaona taabu kutokana na ubaguzi wenu. Leo wenzenu wanaboresha historia kwa kuweka mile stone mpya mnaanza nongwa kama ilivyodesturi yenu mambo mazuri ni yale mnayoamu nyie tu wakiamua wengine ndio utata wenu mnaposhindwa kujizuia, historia ya Mandela na Tanu haziwezi kuwa sawa wala kufananishwa.

Hakuna dhambi hapa kwani hata ingebaki isingefika miaka mingine mia, huu ni wakati mzuri kuweka jengo kubwa ambalo litakuwa na historia na kudumu kwa vizazi vinavyokuja kutokna na industry ya ujenzi ndio iko katika Boom. Historia unayosema Manyerere bado ipo na patakumbukwa tu, kumbuka ilikuwa ni ofisi na mahitaji ya ofisi yanaongezeka na Chama kinakua pia.

Moja ya masomo niliyoyapenda ni Historia. Historia inatusaidia kujua tulikotoka, tulipo; na kwa maana hiyo tunaweza kupanga aina ya maisha yatu ya baadaye. Jengo la TANU Mtaa wa Lumumba- mahali palipotumiwa na waasisi wa Taifa letu kuanzisha chama hicho cha ukombozi, sasa linabomolewa. Binafsi, naiona hii ni dhambi ya kihistoria.

Umuhimu wa jengo hilo haupo kwa wana CCM pekee, bali kwa Watanzania wote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hapo ndipo wazee wetu walipokutana na kuanzisha chama ambacho baadaye kiliongoza mapambano ya kumng'oa mkoloni Mwingereza. Naamini kwa dhati kabisa kuwa jengo hilo si mali ya CCM kama chama, bali ni jengo la Watanzania wanaoheshimu historia ya Taifa lao.

IMG_4947.JP

​

Sikuona sababu za msingi za kubomolewa jengo hilo na kujengwa kitu kingine eti kitega uchumi. Makosa haya ya kubomoa majengo ya kihistoria yanashamiri. Tumeshuhudia jengo la Salamander likivunjwa. Jengo la Forodhani ambako sasa kuna Mahakama ya Rufani, ndilo lilitumiwa kama hoteli ya kwanza katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa siku za karibuni kuna mipango madhubuti ya kulivunja ili kupisha upanuzi wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski! Jengo la pale Magomeni ambalo kulikuwa na chumba kilichotumiwa na Mwalimu Nyerere alipojiuzulu ualimu, limevunjwa. Jengo hilo kwa hakika ndipo mahali ambako Mwalimu alitumia muda wake wote kuandaa maandiko na mikakati mbalimbali ya ukombozi wa nchi hii. Watawala wetu hawakuona umuhimu wake, wamelibomoa.

Ndugu zangu, nimezuru nyumba za kihistoria kama ile ya Keneth Kaunda kule Zambia na nyumba ya Nelson Mandela, Soweto Afrika Kusini. Nyumba zile zimeachwa katika uhalisia wake kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vijavyo. Kinachofanywa ni ukarabati tu ambao haupotezi maaana wala asilia ya nyumba husika.

Kubomolewa kwa Jengo la TANU, Mtaa wa Lumumba ni kosa kubwa kihistoria. Walioamua jambo hilo hawawatendei haki Watanzania wa miaka ijayo. Pengine mambo kama haya yanayokuwa kwenye fikra za watu fulani fulani ni vema ukawapo mjadala mpana ili kusikia Watanzania wanasema nini.

Ubomoaji majengo ya kihistoria ni dhambi kihistoria.
 
Back
Top Bottom