Historia ya TANU Ilifichwa?

Historia ya TANU Ilifichwa?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,242
Reaction score
33,851
  • Mohamed Said anahoji inakuwaje historia ya chama kikubwa kama TANU, kilichoongozwa na Mwalimu Julius Nyerere, imepotea kiasi kwamba waasisi wake hawafahamiki wala kazi zao hazijulikani. Anasema kuwa kusoma historia ya TANU haitoi msisimko kama ule unaopatikana unaposoma historia za harakati za Kenya au Afrika Kusini.
  • Kusahaulika kwa Mashujaa walio hai: Anashangaa kwanini historia iliandikwa vibaya wakati waasisi wengi walikuwa bado hai, kama vile Ally Sykes (mwenye kadi namba mbili), Ali Mwinyitambwe (aliyeambatana na Abdulwahid Sykes kwenda kumtafuta Nyerere), na Dkt. Vedastus Kyaruzi. Dkt. Kyaruzi anatajwa kuwa aliandika mswada wa historia hiyo lakini mchapaji akaukataa.
  • Mchango wa Watu wa Kawaida: Mohamed Said anaeleza kuwa alifanya utafiti kwa kuwatembelea watu waliokuwa na harakati hizi ambao walimfurahia sana. Anawataja mashujaa wa kawaida kama:
    • Mshamwa Wadhi kule Mikindani, ambaye alikuwa muuza vipodozi na mafuta nyumba kwa nyumba, lakini ndiye aliyeingiza TANU kusini kwa kuchukua kadi Dar es Salaam.
    • Salum Mpunga kutoka Lindi, aliyewakilisha mkoa wa Kusini (Southern Province) kwenye mkutano wa kwanza wa TANU mwaka 1955 katika ukumbi wa Arnautoglu.
    • Mohammed Abdallah wa Mtwara.

View: https://youtu.be/ohsLCBNfxcY?si=JFu5lf1OvBVOOkJR
 
Hiizi stori hunichekesha kwani nimeanza kuzisikia ningali kijana mdogo humu jf hadi sasa hivi mtu mzima na familia yangu?!🤣🤣
 
Inside 10,
Mimi mwenzio ni sehemu ya historia hii.

Baba yangu alipata kuniambia kuwa mara ya kwanza kumuona Nyerere ilikuwa mwaka wa 1952 nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Aggrey.

1952 ndiyo mwaka niliyozaliwa.
 
Scars,
Nilipata kumwambia mtu mara tu Tundu Lissu alipofunguliwa mashtaka ya uhaini kuwa kesi hiyo itazua balaa kubwa.

Wewe mwenzangu una lipi la kusema?
Tupe tathmini yako kupitia ukongwe wako, unaona kesi hii ina msingi wowote?

Wewe unavyoona tuhuma ambazo anashtakiwa Lissu unaziona zina ukweli?
 
Mzee Mohamed Said historia ya ANC kuanzia kuanzishwa kwake na harakati nzima za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini ziko well documented na zinasisimua sana

Utapata kuona uzalendo, kujitolea na kuhatarisha maisha kwa ajili ya heshima ya watu wao na taifa lao kutoka kwa akina Giovani Mbeki(baba yake Thabu Mbeki), Oli Tambo(kama Oliver Tamba alivyokua akiitwa na makomred wenzake), Walter Sisulu na Ahmed Kathrandu

Walikuwepo kina mama kama Florence Matomela, Mama Nomzane Winnie Medikizela (Winnie Mandela) na wanaharakati wengi wake kwa waume na hata viongozi wa vyama vya wafanyakazi chini ya COSATU

Sidhani kama kuna historia ya harakati za kupambania uhuru na haki katika nchi iliyohifadhiwa vizuri na kubakia salama mpaka sasa kama ya Afrika ya Kusini

Ukiisoma ukiisoma utakutana na watu walikua na misimamo mikali sana dhidi ya ubaguzi wa rangi kuliko Nelson Mandela

Walikuwemo kina Chris Honey, Steve Bantu Biko na wengine wengi. Hata Mama Winnie alikua mtu wa misimamo mikali sana tena wakati huo mumewe yupo gerezani

Nakumbuka hata baada ya ANC kushika dola na ilipoundwa tume ya ukweli na maridhiano zilitumika nguvu za ziada kumshawishi Winnie akubali kuomba radhi kwa aliyoyafanya dhidi ya waliokua wapinga harakati za kupinga siasa, sheria na sera za Apartheid

Kuna wakati Nelson Mandela baada ya kua ametoka gerezani alisema akiwa ziarani nchini Sweden kua lolote analosema Oli Tambo(wakati huo Baba Tambo akiwa Mwenyekiti wa ANC) ndio msimamo wake yeye Mandela na hakika anamuelezea Baba Tambo kua ni kiongozi mahiri kwelikweli

Kwa kifupi wametajwa watu wengi na ushiriki wa kila mmoja katika mapambano ya kudai haki zao na historia imehifadhiwa vyema

Katika nchi za Afrika Mashariki( Angalau Kenya Uganda na Tanganyika kuna kasoro hiyo. Harakati zao za kupigania uhuru wa nchi zao zimerekodi na kuwatambua watu wachache sana ambao walikuaja kua viongozi wakuu wa nchi hizo

Tena angalau Kenya na harakati za MauMau unakutana na watu wengi zaidi yaani kina Dedan Kimathi, General Mathenge na wengine wengi na vitabu vimeandikwa juu yao. Japo Jomo Kenya ndio alikua kinara lakini wametajwa watu waliopambana kwa machozi jasho na damu

Zanzibar pengine sababu ya udogo wa nchi yao oral tradition imesaidia ku preserve utajiri wa historia yao kabda, wakati na baada ya mapinduzi

Wito wangu tusome. Tusome kila kila kitu na tusijifunge kwenye box.

Tusome historia rasmi ya nchi yetu kama inavyo fundishwa shuleni, tusome historia kama ilivyo andikwa na watu wengine kama Joseph Mihangwa, Mohamed Said, Pius Msekwa na hata kina Mohsi Ali Baruani (au Ali Muhsin Baruan) kwa Zanzibar na wengine wengi

AIdha masimulizi ya mdomo kwa watu walio iishi historia yenyewe ni vyanzo muhimu vya kujua historia zetu. Tutakapo jielewesha na kujua zaidi tutakua katika nafasi nzuri ya kuhakiki, kukubali au kukosoa
 
Sesten...
Juma lililopita nimepokea kalenda kutoka Johannesburg iliyokuwa na picha ya harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Kalenda hii inaeleza historia nzima ya mapambano hadi kufikia uhuru.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom