Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Mohamed Said, tunaomba uandamane mpaka Ikulu kupinga historia ya wazee wako kufutwa kabisa
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said, tunaomba uandamane mpaka Ikulu kupinga historia ya wazee wako kufutwa kabisa

Jackline,
Ahsante kwa kunikumbusha wajibu wangu kwa wazee wangu.

Lakini kwa nini niamdamane mimi peke yangu?

Ingawa ni wazee wangu ndiyo waliojenga nyumba ile lakini nyumba
ile ndipo yalipokuwa Makao Makuu ya TANU chama kilichokomboa
Tanganyika na ukoloni.

Wewe huhisi kuwa mimi na wengine tunawajibika kuandamana
pamoja na wewe pia?

DSCN1159.JPG


Kwanza ilikuwa ofisi ya African Association na ilijengwa kwa kujitolea. Ilifunguliwa rasmi mwaka wa 1933 (soma caption)
hapo juu.
 
Ndugu zangu tuache mzaha. Mjadala huu si mdogo. Majengo ya kihistoria kama haya ni vitu muhimu sana kwa kizazi kijacho. Tukiendekeza bomoa bomoa hii si ajabu hata ikulu ikabomolewa. Hii ni dhambi ya kihistoria.

Original lilikuwa la tope na sasa linavunjwa likiwa la block don't you see progress na historia itabaki pale pale.
 
Historia za kijinga hatuzitaki UKAWA ikichukuwa nchi tunabomowa Lumumba na Chimwaga.

Ndio maana Iraq wamelibomoa sanamu la Saddam hatuhitaji ukumbusho wowote wa madikteta.
 
Historia za kijinga hatuzitaki UKAWA ikichukuwa nchi tunabomowa Lumumba na Chimwaga.

Ndio maana Iraq wamelibomoa sanamu la Saddam hatuhitaji ukumbusho wowote wa madikteta.
Wewe ndiyo msemaji wa UKAWA.

Cc: Matola
 
Last edited by a moderator:
Historia za kijinga hatuzitaki UKAWA ikichukuwa nchi tunabomowa Lumumba na Chimwaga.

Ndio maana Iraq wamelibomoa sanamu la Saddam hatuhitaji ukumbusho wowote wa madikteta.

Cc Matola shifta RAS WISER BILLIONAIRE PITGAN
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton nakuhifadhi ili usipate sababu ya kusema nimekuharibia uzi. Ila najua unaelewa kuwa nakufahamu in and out. Kuhusu kuihujumu Chadema hilo hatabutokwe povu namna gani hata viongozi wa chadema wanajua. Gazeti unalodai ni lako tunajua anayelifadhili. Na kwa nchi hii ilivyo hatapata urais hata akitambika uchi hadharani. Sijakuprovoke ila ukweli ni kuwa maandishi yako mengi husukumwa na TUMBO. Akili huwa imesinzia
Uongo ni kipaji kama vipaji vingine. Pengine kuna mtu anatumia jina langu na unashirikiana naye maana nimesikia kuna mtu anasaka fedha akisema ni Manyerere wa Jamhuri na kwamba anaanzisha chama cha wacheza bao. Inawezekana umekutana na tapeli moja makini ukadhani ni mimi. Ebu rejea tena kwenye kumbukumbu zako na ikibidi wasiliana na mimi kwa 0713 33 54 69. Yawezekana unapambana na Manyerere feki. Kama ni mimi huyu huyu Manyerere halisi, nakuomba umwage hapa kila ulilo nalo juu yangu. JF ni uwanja wa wazi kwa watu makini.
 
Nimepata mshituko wa taarifa za kufutwa kwa kumbukumbu ya ukombozi wa Tanganyika, yaana kupolromoka kwa na mnara wa ukombozi, kama ambavyo imeelezewa kwa kina kwenye makala ya Nasaha za Mihangwa katika gazeti la Raia Mwema la Februari 25- Machi, 3, 2015. Si japata ufafanuzi wa kutosha dhamira ya kufuta makumbo ya Lumumba, wazo la haraka limenijia la kuanza kusubiri lini makumbu ya Azimio la Arusha ilishushwa au kubadilishwa kwa ajili ya shughuli nyingine za uwekezaji.
Kwa hali ilivyo hivi sasa, utekelezaji wa Azimio la Zanzibar umeanza kujidhirisha. Uchaguzi 2015 Oyeeeeeeee!!!!!!!!!!
 
Aliyeamua kubomoa kumbukumbu ya Lumumba atakuwa ni miongoni mwa Mafisadi akiona TANU anamkumbuka Mwalimu Nyerere .
 
Hao jamaa wa Sisiem wameamua kuvunja jengo lao pale Lumumba, ambako ndipo TANU ilipozaliwa mwaka 1954, baadaye chama hicho kikaja ungana na ASP mwaka wa 1977.

Siri kubwa ya kuvunja kumbukumbu hiyo ya jengo lao la TANU, ni kwa kuwa hata wao wenyewe wameamua kuungana na Ukawa katika movement ya kuidelete kabisa CCM, kwa kuwa hata wao wanajua kuwa ifikapo Oktoba ya mwaka huu, ndipo Sisiem itazikwa rasmi.

Na baada ya hapo hiko chama kitabakia kwenye vitabu vya kumbukumbu ya historia ya nchi hii, kuwa kuna enzi nchi hii iliwahi kuwa na chama cha siasa, kilichokuwa kinaitwa Sisiem!
 
Wamelibomoa kwa amri ya mfadhili wao Ghalim Mohamed Said myemeni aliyepewa ubalozi wa Tanzania nchini China, kwa kubadilishana na pesa atakazowapa CCM kwa uchaguzi. Hawa ni wa yemeni wa Home Shopping Center waliowahi ku paralize shughuli za Bandari kwa faida ya Rizwani na baba yake, ndio waliofadhili ubunge wa Ridhwani wa Chalinze na waliopewa kiwanja pale corner ya Udoe na Lumumba kilichokua cha CCM pia, hakuna uwekezaji wowote na ni vizuri Jackton Manyerere mpiganaji wa enzi hizo akatuongoza katika kulirudhisha jengo letu nakuwapeleka wahusika mahakamani. Hapa Alosco ndip wanaposhinda viongozi wote wa juu wa CCM akiwemo mzee mang'ula na ndipo wanapopelekewa hela za matumizi ikiwemo ofisi kuu kupitia kwa dada yule anayetumwaga kuchukua hela. Ni aibu na kinyaaa wanavyojipendekeza kwa kutumia rasilimali na mali za watanzania, manyerere piga kipenga tuko nyuma yako, anzeni na kupamba magazeti yenu na uchafu huu kama wakitaka wakawepe majengo ya msoga kule viko vibanda vingi tu vya udongo, hebu tuanzie hapa na mimi ntakua wa kwanza ku join hiyo nguvu na wapelekwa mahakamani hivi TLs ndio imekabidhi kazi zake kwa Kibatala? wako wapi mamluki hawa?
 
Binafsi sishangai. Kuna makubwa zaidi yamefanyika chini ya utawala huu ila bado hayajatokeza kwenye limelight! Hili limegusa hisia za watu kwakuwa linaonekana kwa macho.

Ila tusisahau kuwa mchwa anapokaribia kufa huota mbawa!
 
moja ya masomo niliyoyapenda ni historia. Historia inatusaidia kujua tulikotoka, tulipo; na kwa maana hiyo tunaweza kupanga aina ya maisha yatu ya baadaye. Jengo la tanu mtaa wa lumumba- mahali palipotumiwa na waasisi wa taifa letu kuanzisha chama hicho cha ukombozi, sasa linabomolewa. Binafsi, naiona hii ni dhambi ya kihistoria.

Umuhimu wa jengo hilo haupo kwa wana ccm pekee, bali kwa watanzania wote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hapo ndipo wazee wetu walipokutana na kuanzisha chama ambacho baadaye kiliongoza mapambano ya kumng'oa mkoloni mwingereza. Naamini kwa dhati kabisa kuwa jengo hilo si mali ya ccm kama chama, bali ni jengo la watanzania wanaoheshimu historia ya taifa lao.

img_4947.jp

​

sikuona sababu za msingi za kubomolewa jengo hilo na kujengwa kitu kingine eti kitega uchumi. Makosa haya ya kubomoa majengo ya kihistoria yanashamiri. Tumeshuhudia jengo la salamander likivunjwa. Jengo la forodhani ambako sasa kuna mahakama ya rufani, ndilo lilitumiwa kama hoteli ya kwanza katika jiji la dar es salaam.

Kwa siku za karibuni kuna mipango madhubuti ya kulivunja ili kupisha upanuzi wa hoteli ya kilimanjaro kempinski! Jengo la pale magomeni ambalo kulikuwa na chumba kilichotumiwa na mwalimu nyerere alipojiuzulu ualimu, limevunjwa. Jengo hilo kwa hakika ndipo mahali ambako mwalimu alitumia muda wake wote kuandaa maandiko na mikakati mbalimbali ya ukombozi wa nchi hii. Watawala wetu hawakuona umuhimu wake, wamelibomoa.

Ndugu zangu, nimezuru nyumba za kihistoria kama ile ya keneth kaunda kule zambia na nyumba ya nelson mandela, soweto afrika kusini. Nyumba zile zimeachwa katika uhalisia wake kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vijavyo. Kinachofanywa ni ukarabati tu ambao haupotezi maaana wala asilia ya nyumba husika.

Kubomolewa kwa jengo la tanu, mtaa wa lumumba ni kosa kubwa kihistoria. Walioamua jambo hilo hawawatendei haki watanzania wa miaka ijayo. Pengine mambo kama haya yanayokuwa kwenye fikra za watu fulani fulani ni vema ukawapo mjadala mpana ili kusikia watanzania wanasema nini.

Ubomoaji majengo ya kihistoria ni dhambi kihistoria.


=============
kutoka ccm:

haya hayakufanyika miaka hiyoooo ya babu jk...
Kuwezekana kufanyika kipindi hiki basi tunapaswa ktambua kuwa ule au zile enzi za uhai wa hiki chama cha tanu-ccm ndo zimefikia tamati.
Tujiamndae tu na hitimisho la 40 yake nadhani itakuwa october ila tar siijaelewa bado.
 
hao jamaa wa sisiem wameamua kuvunja jengo lao pale lumumba, ambako ndipo tanu ilipozaliwa mwaka 1954, baadaye chama hicho kikaja ungana na asp mwaka wa 1977.

Siri kubwa ya kuvunja kumbukumbu hiyo ya jengo lao la tanu, ni kwa kuwa hata wao wenyewe wameamua kuungana na ukawa katika movement ya kuidelete kabisa ccm, kwa kuwa hata wao wanajua kuwa ifikapo oktoba ya mwaka huu, ndipo sisiem itazikwa rasmi.

Na baada ya hapo hiko chama kitabakia kwenye vitabu vya kumbukumbu ya historia ya nchi hii, kuwa kuna enzi nchi hii iliwahi kuwa na chama cha siasa, kilichokuwa kinaitwa sisiem!

40 ya marehem ccm ni lini??
 
Kubomoa majengo ya kihistoria ni kutokuona mbali kwa serikali yetu tukufu. Majengo ya zamani huwa yanakarabatiwa na kubakia jinsi yalivyo kwa vizazi vijavyo. Pia huwa ni vivutio vya utalii kama mji mkongwe kule Zenj.

Kule Marekani kila mji unatunza yale majengo yaliounzisha na ni vivutio vikubwa vya utalii.

Aliyeidhinsha ubomoaji wa haya majengo ni waziri mkuu mstaafu EDO !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kwa kuwakatalia wale wahifadhi wa mambo ya kale wa wizara ya maliasili na utalii! Walipigana kufa na kupoa kuokoa yale majengo pale Samora Avenue lakini ikashindikana!
 
Back
Top Bottom