Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Moja ya masomo niliyoyapenda ni Historia. Historia inatusaidia kujua tulikotoka, tulipo; na kwa maana hiyo tunaweza kupanga aina ya maisha yatu ya baadaye. Jengo la TANU Mtaa wa Lumumba- mahali palipotumiwa na waasisi wa Taifa letu kuanzisha chama hicho cha ukombozi, sasa linabomolewa. Binafsi, naiona hii ni dhambi ya kihistoria.

Umuhimu wa jengo hilo haupo kwa wana CCM pekee, bali kwa Watanzania wote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hapo ndipo wazee wetu walipokutana na kuanzisha chama ambacho baadaye kiliongoza mapambano ya kumng'oa mkoloni Mwingereza. Naamini kwa dhati kabisa kuwa jengo hilo si mali ya CCM kama chama, bali ni jengo la Watanzania wanaoheshimu historia ya Taifa lao.

IMG_4947.JP

​

Sikuona sababu za msingi za kubomolewa jengo hilo na kujengwa kitu kingine eti kitega uchumi. Makosa haya ya kubomoa majengo ya kihistoria yanashamiri. Tumeshuhudia jengo la Salamander likivunjwa. Jengo la Forodhani ambako sasa kuna Mahakama ya Rufani, ndilo lilitumiwa kama hoteli ya kwanza katika Jiji la Dar es Salaam.

Kwa siku za karibuni kuna mipango madhubuti ya kulivunja ili kupisha upanuzi wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski! Jengo la pale Magomeni ambalo kulikuwa na chumba kilichotumiwa na Mwalimu Nyerere alipojiuzulu ualimu, limevunjwa. Jengo hilo kwa hakika ndipo mahali ambako Mwalimu alitumia muda wake wote kuandaa maandiko na mikakati mbalimbali ya ukombozi wa nchi hii. Watawala wetu hawakuona umuhimu wake, wamelibomoa.

Ndugu zangu, nimezuru nyumba za kihistoria kama ile ya Keneth Kaunda kule Zambia na nyumba ya Nelson Mandela, Soweto Afrika Kusini. Nyumba zile zimeachwa katika uhalisia wake kwa ajili ya kumbukumbu za vizazi vijavyo. Kinachofanywa ni ukarabati tu ambao haupotezi maaana wala asilia ya nyumba husika.

Kubomolewa kwa Jengo la TANU, Mtaa wa Lumumba ni kosa kubwa kihistoria. Walioamua jambo hilo hawawatendei haki Watanzania wa miaka ijayo. Pengine mambo kama haya yanayokuwa kwenye fikra za watu fulani fulani ni vema ukawapo mjadala mpana ili kusikia Watanzania wanasema nini.

Ubomoaji majengo ya kihistoria ni dhambi kihistoria.

=============
Kutoka CCM:
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amesema CCM haiwezi na wala haina mpango wa kupoteza historia ya mahali ilipozaliwa TANU.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wahariri wa gazeti la JamboLeo alipotembelea ofisini kwao katika ziara ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Alisema kumekuwa na maneno mengi kama vile ukarabati unaofanywa kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba ni kupoteza historia ya TANU.

Alisema kinachofanyika ni maboresho ya ofisi ndogo ya CCM Lumumba ifanane na hadhi, mahitaji na wakati wa Chama hicho, lakini historia itabaki kama kielelezo cha Mahala ilipozaliwa TANU.

Alifafanua kuwa awali ofisi ya mwanzo ilikuwa nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa makuti, kisha ikaondolewa makuti na kuezekwa mabati ya madebe,baade ikabadilishwa na kuwekwa bati za kisasa.

“Historia ya TANU iliyopo kwenye jengo la Lumumba, tutaendelea kuitunza na hatutoibomoa kwani ni kielelezo cha tulikotoka na tunajivunia historia hiyo, tutaitunza”

Alisema kama tusingefanya maboresho maana yake tungekuwa na jengo la udongo ambalo limeezekwa makuti mpaka leo. Akadai wanaolalamika hawajui historia ya eneo hilo, ila akawashukuru kwa mapenzi yao mema kwa Chama hicho.

Aliongeza kuwa hakuna namna CCM itaruhusu historia ifutike na huku ikiendelea kuhifadhi historia za vyama vingine, hasa bile vya ukombozi kusini mwa bara la Afrika.

Nape pia alikanusha uvumi kuwa CCM inawekeza kitega uchumi eneo hilo, akasema wanakarabati ofisi na itakuwa ofisi sio kitega uchumi.
 
Mkuu ukubwa wa maneno wengine macho kwisha habari yake ziku nyingi.
 
Ni ukweli husio na chenga kuwa jengo hilo ni mali ya watanzania wote bila kuangalia itikadi ya kisiasa hasa kwa jengo hilo, ila kwa ccm ukiyasema hayo utaonekana ni adui namba moja.
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!
 
Ni mfumo wa vyama vingi, sina uhakika kama watanzania wenye itikadi tofauti za vyama wanahitaji kuwa na kumbukumbu ya Jengo la chama kimoja.
 
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco
 
Last edited by a moderator:

Kweli kabisa, mimi ningewaelewa wanaopinga kubomolewa kwa jengo hilo kama wangependekeza lisiwe la CCM kwanza ili historia yenyewe iwe na maana wakati ambao nchi inafuata mfumo wa vyama vingi, lakini kama wanakubaliana ni jengonla CCM sioni tabu kama wameamua kulivunja.
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!

Biblia inasema mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye. Unahitaji kupimwa IQ yako. There is something wrong somewhere. Haiwezekani mtu mzima akafikiri kama wewe. Haiwezekani. Ni lazima utakuwa mgonjwa.
 
Ni mfumo wa vyama vingi, sina uhakika kama watanzania wenye itikadi tofauti za vyama wanahitaji kuwa na kumbukumbu ya Jengo la chama kimoja.
Historia ya TANU na nafasi yake katika historia ya Tanzania, itabaki kuwa ni ya kila Mtanzania bila kujali itikadi. Ukweli unabaki kuwa ukweli tu. Hapa tunazungumza historia ya chama kilichoongoza mapambano ya kuleta Uhuru wetu. Historia hiyo inabaki kuwa ya TANU na wala si CUF wala Chadema. Hili si suala la kiitikadi, ni suala la ukweli wa kihistoria ambao haupaswi kupindishwa au kuvurugwa.
 
Manyerere Jackton
Mkuu Manyerere asante kwa hii, This is sad!, very sad indeed! kama ni kweli, Mzimu wa Babu yako, utawaibukia!.
Kuna uzi humu niliwahi kuuliza Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!. Huu ni uthibitisho hata viongozi wetu ni ignorants mpaka basi!,

Japo mimi sijapita hapo Lumumba, naomba kutoa angalizo lenye some minimum reasonable doubt, kuwa kinachofanyika, sio lazima iwe ni kuvunja, bali wanaweza kuvunja baada ya kujiridhisha restoration haiwezi kulidumisha kwa sababu original structure ni udongo ambao hauwezi kudumu miaka milioni moja ijayo, hivyo kinachofanyika sasa ni ku demolish the old structure, kisha kujenga replica vile vile, halafu ile ample wastage space, ndio inakuwa put to more economical news ikiwemo kujenga ghorofa on top for investment!.
This is my assumption tuu!.

Pasco

Kamanda, nakushuruku kwa kuliona hili jambo. Lile jengo bado lilikuwa imara, tena lingeweza kuwapo kwa miaka mingine 100 au zaidi. Hapakuwa na sababu ya kubomoa jengo ambalo bado liko imara na si hatari kwa maisha ya binadamu. Hoja ya CCM, kama umefuatilia vema, ni kuliondoa ili kuweka 'Kitega Uchumi'! Kwa hiyo hoja si uzee, bali kuingia pesa! Unaweza kujiuliza, nchi hii imekuwa finyu kiasi kwamba uwanja pekee wa kuwekwa kitega uchumi cha chama ni kubomoa Jengo la TANU? Hakika uamuzi huu naulaani.
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!
Mkuu Manyerere Jackton ni mwana CCM mwandamizi. Nyakati kama hizi ni kawaida yake kuwa kinyonga kutegemea ugali ulipo.
 
Last edited by a moderator:
Hivi hilo jengo kama lina umuhimu kwa taifa kwa nini bado ni mali ya CCM?
 
Usitake kupindisha mada. Mijadala ya aina hii waachie wenye weledi.

Manyerere Jackton ukisoma post ya Pasco hapo juu utaona hajawa wazi ila tuliomwelewa amekukosoa 'kisomi' kwamba umekurupuka. Na hii ni sababu ya ukanjanja wako na kuhusudu kutumikia wenye fedha. Ulipaswa uende mbali ufanye homework yako vizuri, vikao vilivyoamua kuvunja hilo jengo, wana sababu zipi za msingi baada ya hapo ndipo ungekuja na bandiko lililo balanced.
Ukae ukijua unaingia kwa jina lako verified tofauti na Pasco kwaiyo unapoleta thread tunaamini haina msukumo wa tofauti.
 
Last edited by a moderator:
alama kuu ya kujua kama Mungu amekucha....hauko pamoja na Mungu au huna kibali cha Mungu kuwaongoza wenzako au kuongoza taifa ...Mungu anakuondolea hekima!Viongozi wa CCM Mungu kawaondolea hekima.....hawaoni hawasikii hata tupige kelele kiasi gani....hawaoni....hawanahaibu yaani wapo tu kama debe tupu!wanafanya mambo ya ajabu tena ya kijinga....hata wananchi wapige kelele hawasikii....hawaoni....hawajali!mifano ni mingi lakini tuangalie majengo na kumbukumbu za kihistoria kama hili jengo la TANU....kulibomoa ni kuondoa na kufuta historia ya TANU na Tanganyika pia Muungano wa nchi hii!najua hawapendi kusikia jina Tanganyika labda ndo sababu ya kulivunja.....😱...TANU ilipinga unyonyaji...ukupe...ujinga....umasikini...maradhi...uonevu na ukandamizaji...TANU ilileta azimio la Arusha....Iringa....Musoma nk.....leo tunavunja tunaona hivi vyote havina maana!!!!Huu ni mwisho wa CCM japokua hawaoni....hawasikii hata mpige kelele vip....za escrow....sukari......wizi&uchafu wote hawaoni..hawasikii....MUNGU KAWAONDOLEA HEKIMA...NDO MWISHO WAO
 
Hivi hilo jengo kama lina umuhimu kwa taifa kwa nini bado ni mali ya CCM?

Mkuu, inaaminika kuwa Abdulrahman Kinana anaweza akawa mgombea Urais kwa kupitia CCM. Makundi na wasaka madaraka ndani ya CCM wameazimia kuwatumia wanahabari njaa kuhakikisha wana challenge kila uamuzi uliofanywa na chama wakati Kinana ni Katibu mkuu. Kazi imeanza...
 
So CCM are getting rid of their own reminiscences in this sense,What a bunch of muppets!
 
CCM ina vichwa makini hayo yote yamejadiliwa kwa muda mrefu katika vikao husika, hivyo uamuzi ulifikiwa ni huo! Nyie msiotakia mema CCM kwa nini kila uamuzi unaofikiwa na chama chetu unatilia mashaka? Umefika wakati wa kutumia raslimali kuingiza pesa na si vinginevyo. WEWE MBONA nyumbani kwenu hukuzuia kubomolewa kwa nyumba ya aliyezaliwa babu mzaa babu yako!!!!!

Vichwa makini vya CCM ndivyo vinalea wizi Kama Wa ESCROW, MEREMETA NA RADA?
Hivi umeielewa concept ya mleta mada au huu ndo uwezo wako unapoishia ktk kuelewa mambo?

Mwenzio kajitahidi kujenga hoja wewe unaleta shombo umewahi jiuliza why UNESCO huyapa hadhi baadhi ya majengo Kama urithi Wa dunia?
 
Back
Top Bottom