Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

Kubomolewa Jengo la TANU ni dhambi ya kihistoria

sioni hajabu kwani hata nchi ambayo hicho chama kiliipatia uhuru si haipo so hakuna umuhimu wa kuwa na kumbukumbu
for me No TANU without Tanganyika
 
historia inaonyesha kuwa kuna wakati CCM ilikuwa ni ya watanznia wote. majengo yote ya wakati huo yalikuwa mali ya watanzani kwa hiyo yakipewa heshima ni jambo jema

Kutunza historia ya TANU ni sawa na kutunza mazalia ya CCM, wayavunje na kuyaondoa yote tu, hiyo historia itunzwe vitabuni kama wanataka, Kuanza upya si ujinga!
 
Ndugu zangu tuache mzaha. Mjadala huu si mdogo. Majengo ya kihistoria kama haya ni vitu muhimu sana kwa kizazi kijacho. Tukiendekeza bomoa bomoa hii si ajabu hata ikulu ikabomolewa. Hii ni dhambi ya kihistoria.
 
....Hii ni dalili ya KUBOMOKA kwa CCM!
Tusubiri WABOMOE jengo lilipozaliwa Azimio la Arusha hapo Kaloleni.... Hawana kitu hawa. Eti Chipukizi wanaowatumia katika halaiki za chama ni WATOTO wa WANACHAMA wa CCM.... Haya anayasema Kiongozi wa Serikali Bungeni! Tuna watu hapa? Wabomoe....Waache wabomoe wabomoke!

Naunga mkono hoja yako 9999%! Yavunjwe tu!
 
Unajua hawa jamaa wanachukia asili yao. Wanachukia kukumbuka walikotoka kisa wanataka kuhalalisha ubepari. Kwa akili hizi kunawengine wanatamani wangezaliwa kwa mabepari. Hii inaonyesha jinsi mkulu na wenzake wanavyochukia waasisi wa taifa hili na wako tayari kuwatukuza wakoloni. Hawa lazima waadhibiwe kwa hili, hawataachwa hivi hivi.
 
Kama wanataka kuweka kitega uchumi.kwanini wasinunue eneo jingine hapo lumumba na kujenga kitega uchumi chao? Ccm washaona kwamba hawana chao kwahiyo mali zote zilizoachwa na mkoloni wanajimilikisha kama chama.
 
Ndugu zangu tuache mzaha. Mjadala huu si mdogo. Majengo ya kihistoria kama haya ni vitu muhimu sana kwa kizazi kijacho. Tukiendekeza bomoa bomoa hii si ajabu hata ikulu ikabomolewa. Hii ni dhambi ya kihistoria.
Kaka yangu Manyerere Jackton nikusaidie vitu vichache usivyovijua.
Mosi: Mzaha unaousema, labda wachangiaji wametazama aliyeleta thread yaani wewe. Wengi wetu tunaelewa kwa hakika kuwa msukumo wako kwenye uandishi wako popote pale ni TUMBO. So waungwana 'wameupotezea' kiaina uzi wako.
Au Ungeazima busara za kaka Pasco kwa kujaribu kutuletea thread za mademu wenye vikuku miguuni, mademu wenye rangi za khaki, au mademu wenye makalio manene utaona utakavyopata wachangiaji. Mwenzio Pasco alianza taratibu sasa yupo kwa wabunge. Sasa wewe dondosha uzi hapa anzia kwa mawaziri! Wallah utashangaa ndani ya Dk 2 uzi una page 20 na zote ni nondo. Anza na Dk. Fenella yule mama anayejua Michezo...
Au mwisho, anzisha thread ya udini. Mtukane Kadhi au Mpongeze Nyerere kwa kuweka misingi ya umoja Tanzania. Au isifie Bakwata. Wallahi utafarijika. Huu uzi wako watu washautosa maana tumbo limetangulia mbele akili umeziacha nyuma. Ahsante!
 
Last edited by a moderator:
Yani Watanzania tuna akili za ajabu kweli!!! Mtu mzima kabisa na watoto nyumbani unashinda mitandaoni eti kutetea majengo machakavu kisa tu "kulinda historia!!!"

Historia gani hiyo ya kulindwa isiyokuwa na maslahi mapana kwa taifa!? Nchi zingine zenye watu wenye akili hulinda tu zile historia mahususi za kuingizia taifa mapato ili serikali zao zizidi kutoa huduma kwa wananchi. Hapa kwetu eti tunataka kulinda majengo machakavu yaliyo katika maeneo "prime" kisa tu kutunza kumbukumbu za ukombozi!!! Is this for really!

Hivi ni kweli vichwa vyetu vinajali sana historia kuliko kuendana na ulimwengu na mabadiliko yake? Newyork, Dubai, Taipei, Tokyo na Abu Dhabi huko kote zilifanyika controlled demolition ili kupisha skycrapers kujengwa kwa maendeleo mapana ya taifa. Hapa kwetu mtaa wa Lumumba ukiguswa utasikia wahuni wachache wanaanza kulia lia mara historia mara sijui nini!

Kama kweli wewe mleta mada unajali historia basi ungefanya utafiti kujua aina ya chupi aliyokuwa akivaa babu kizaa babu yako ili na wewe uiendeleze kuivaa na pia kuwarithisha wajuu zako.

Yaani kwa utumbo ulioumwaga hapa , ndiyo mjumbe wa kamati kuu yenu!Kazi ipo.
 
Mkuu, inaaminika kuwa Abdulrahman Kinana anaweza akawa mgombea Urais kwa kupitia CCM. Makundi na wasaka madaraka ndani ya CCM wameazimia kuwatumia wanahabari njaa kuhakikisha wana challenge kila uamuzi uliofanywa na chama wakati Kinana ni Katibu mkuu. Kazi imeanza...

Mi nafikiri mkuu labda una chuki zako binafsi kwa Manyerere, hoja mbona imekaa vizuri, hakuna atakayefurahi majengo ya kihistoria yakibomolewa kipuuzi namna hiyo, watoto wetu wataona nini?

Nchi hii imejaa wapuuzi, wameacha majengo machache sana ambayo wameshindwa kuyabomoa baada ya Serikali ya Ujerumani na South Africa kuwasihi wasibomoe na watayatunza kwa gharama zao, Garrison ya Bagamoyo, Solomon Mahlangu na kwingineko.
 
Kinana na sekretariet yake lazima wapige deal ....deal za pembe za ndovu ..zimepigwa marufuku duniani ..sasa wanaanza kuuza nyumba
 
Ndugu zangu tuache mzaha. Mjadala huu si mdogo. Majengo ya kihistoria kama haya ni vitu muhimu sana kwa kizazi kijacho. Tukiendekeza bomoa bomoa hii si ajabu hata ikulu ikabomolewa. Hii ni dhambi ya kihistoria.

Huenda ameuziwa Edward Lowassa kama ilivyo kwa yale maghorofa ya Umoja wa Vijana pale Morogoro Rd/Lumumba, maana ana hisa 50% na ndio chanzo cha ugomvi wa Nape na Lowassa.

Lowassa huwa hana huruma linapokuja suala la ardhi, yupo tayari hata kubomoa makanisa au misikiti ili ajenge vitega uchumi vyake???

Huyu bwana ni hatari sana.
 
Mi nafikiri mkuu labda una chuki zako binafsi kwa Manyerere, hoja mbona imekaa vizuri, hakuna atakayefurahi majengo ya kihistoria yakibomolewa kipuuzi namna hiyo, watoto wetu wataona nini?

Nchi hii imejaa wapuuzi, wameacha majengo machache sana ambayo wameshindwa kuyabomoa baada ya Serikali ya Ujerumani na South Africa kuwasihi wasibomoe na watayatunza kwa gharama zao, Garrison ya Bagamoyo, Solomon Mahlangu na kwingineko.
Mkuu sina chuki na kaka Manyerere Jackton. Hata yeye anajua. Tumekaa wote Kijitonyama miaka ileeee. Yeye alipanga banda la uani kwenye nyumba ya babu na bibi waliokuwa wanapendana sana.
Manyerere nimeshiriki nae vikao vya kutaka kujaribu kuihujumu Chadema pale soma book cafe pale mikocheni pamoja na omarilyasi. Nilipogundua kuwa vikao vile ni vya kupanga mkakati wa kuiua chadema nilitimka hata sikuaga. Manyerere anajua kuwa namwelewa sana. Hivi karibuni alikuja ofisini kwangu kuomba tuweke tangazo la biashara kwenye kijarida chake cha JAMHURI kinachofadhiliwa na jamaa yake yuleee.... Mi nilimkwepa hakuniona lakini hadi PRO alimpuuza. Mimi nilimkwepa kuogopa kupigwa mzinga. Otherwise Manyerere Jackton ni kaka yangu, swahiba wangu na ni best yangu ingawa yeye ni mwana CCM maslahi na mimi ni Kamanda wa ukweli wa Chadema. Asante
 
Haya Mkuu wangu
 
Last edited by a moderator:
Mnashangaa nini wakati CCM Na serikali yake walitumia mamilioni ya pesa kwenda kufukua makaburi Msumbiji na kuja kufukia mifupa pale Mtwara. Unashangaa nini kwani kwa kitendo kile Tanzania iliamua kufuta historia ya harakati za watanzania Kwa Msumbiji na watu wakajipigia madili yao. Siwezi kushangaa kwa hili na ninakushangaa kwa wewe kushangaa, kwa sababu hata na wao wanakushangaa kwa kushangaa.
 
Juzi nilikuwanaangalia documentary yaBBC(Dangerous road).
Wasafiri wa documentary walikuwa Georgia. Walipofika njiani kati ya kimji cha Ushughul na Svaneti
walisimama nyumbani kwa kiongozi wa Urusi (Starling) miaka ya vita kuuya dunia

Waliingia nyumbani kwake kama kulivyokuwa kuanzia shuka hadi vitambaa vya mezani.
Walionyesha hadi treni aliyotumia wakati huo. Jengo limebaki kama lilivyo, watu wanakwenda kwa historia

Wiki hii Uingereza iliadhimisha miaka 50 tangu alipofariki Churchill.
Walitumia boti iliyobeba jeneza lake kupita mto Thame. Walionyesha kila kilichomhusu.

Mwaka jana mwishoni nchini Canada kulikuwa na mzozo. Hoteli ya kwanza ‘royal mountain’ iliyotumiwa na watawala wa Uingereza walipouzuru koloni hilo miaka mingi ilitakiwa kuuzwa na kubadilishwa jina.
Watu walichachamaa sana kuhusu kufutwa kwa historia

Taj Mahal ni landmark ya India. Leo situ ni sehemu ya historia bali imekuwa kitega uchumi na eneo la utalii.

White house ni jengo la zamani. Hutasikia hata siku moja ikifikiriwa kujengwa upya
Ile meza ya oval office ni mbao za mabaki ya meli.Haibadilishwi

London imebaki kama ilivyo, miji ya kisasa ni kamamachester.
Yaani zile ‘terrace’ house za London ni sehemu ya historia.

Tanzania hatuna uhaba wa ardhi au maeneo. Dar es Slaam ya 1880 ilitakiwa ibaki kama mji wa zamani. Majengo mengine yajengwe nje ya mji.

Kuvunja jingo la TANU ni makosa. Ile ni sehemu ya historiaya nchi ambayo utake usitake ipo na inabaki kuwa historia. Leo wanavunja, kesho akina Nape watanadi ile gari iliyotumika na Nyerere ili kupata pesa za kampeni

Sasa tunaita wachina watupangie mji. Sishangai maana tumerudi nyuma kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.

Hatuji tambui,tunafikiria matumbo. Hilo jengo ni mradi wa watu.

Utashangaa Jiji, na manispaa zina mameya!
 
Huyo ndiye great great grandmother wa FaizaFox.
Ni statement au swali? Kama ni swali jibu ni hapana. Hawezi kuwa uzao wa mkereketwa kama huyo mama. Contibutions za FaizaFox ni za ushabiki na tunavyojitokeza kwa watu kunaonyesha malezi tuliyopata na experiences za wazazi au walezi wetu
 
Mkuu sina chuki na kaka Manyerere Jackton. Hata yeye anajua. Tumekaa wote Kijitonyama miaka ileeee. Yeye alipanga banda la uani kwenye nyumba ya babu na bibi waliokuwa wanapendana sana.
Manyerere nimeshiriki nae vikao vya kutaka kujaribu kuihujumu Chadema pale soma book cafe pale mikocheni pamoja na omarilyasi. Nilipogundua kuwa vikao vile ni vya kupanga mkakati wa kuiua chadema nilitimka hata sikuaga. Manyerere anajua kuwa namwelewa sana. Hivi karibuni alikuja ofisini kwangu kuomba tuweke tangazo la biashara kwenye kijarida chake cha JAMHURI kinachofadhiliwa na jamaa yake yuleee.... Mi nilimkwepa hakuniona lakini hadi PRO alimpuuza. Mimi nilimkwepa kuogopa kupigwa mzinga. Otherwise Manyerere Jackton ni kaka yangu, swahiba wangu na ni best yangu ingawa yeye ni mwana CCM maslahi na mimi ni Kamanda wa ukweli wa Chadema. Asante

Nilikuwa namuamini sana huyu jamaa, lakini tangu alivoanza kuihujumu CHADEMA nikaacha kufuatilia maandiko yake
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom