Mwana Ilala
JF-Expert Member
- Jan 29, 2013
- 1,286
- 488
Kuna jirani yangu amekuja leo kwangu anaazima gari awapeleke jamaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Jirani mwenyewe japo namfahamu kwa sura lakini hata jina lake silifahamu kwa sababu si miongoni mwa majirani ambao tuna ukaribu sana.Swali likanijia huyu bwana anafunga safari kuja kuazima gari kama fyekeo hivi akipata nalo ajali atakuja na maelezo gani?
Lazima tujifunze kuishi kwa kile mwenyezi Mungu alichotukadiria
Kwani gari ina nini usiazime mwenzio? Kama kitu cha maana sana mbona ukifa huzikwi nayo?
Cha msingi
1.mufahamiane,
2.Ajue kuendesha,
3.ujue shughuli anayoenda kufanyia.
Tuache ulimbukeni ukiwa na gari ndo kujiona umemaliza.
Sio kumaliza mkuu, mtoa mada kajieleza vizuri tu Kuwa jirani mwenyewe hawafahamiani hata majina ina maana hana mazoea naye sana. Sasa mtu wa hivyo anawezaje kwenda kuazima gari? Inawezekana hujui hata Kazi anayofanya.
Akienda kulifanyia ujambazi je? Mimi simpi. Kama niko vizuri nampa ya tax. Kama Niko ovyo namwambia nina kazi nalo.
Jamaa yangu aliniazima gari wakati naenda kuoa toka Dar kwenda mkoani, Landcruiser Prado, akaniwekea na mafuta full tank na gari nilikaa nayo wiki nzima ndio nikamrudishia. Tena ilikuwa ndio gari yake ya thamani kuliko nyingine na wakati nimesafiri akawa anashea na mkewe gari kwenda kazini. Inategemea mnahusiana vipi na uwezo wako kiuchumi. Una kagari kamoja, tena ka mkopo then unamuazima "mtu baki" hata Mimi nisingetoa.
Kweli mkuu!!Jamaa yangu aliniazima gari wakati naenda kuoa toka Dar kwenda mkoani, Landcruiser Prado, akaniwekea na mafuta full tank na gari nilikaa nayo wiki nzima ndio nikamrudishia. Tena ilikuwa ndio gari yake ya thamani kuliko nyingine na wakati nimesafiri akawa anashea na mkewe gari kwenda kazini. Inategemea mnahusiana vipi na uwezo wako kiuchumi. Una kagari kamoja, tena ka mkopo then unamuazima "mtu baki" hata Mimi nisingetoa.
Kabisaaa!Kumuazimisha Mtu Gari, Ni sawa na kumuazimisha Mtu Mkeo, Kwani hasara ni Nyingi kuliko Faida.Ni kweli huwezi kujua shughuli Maalumu ya Huyo rafikio,anaweza kwenda kupakilia Meno ya Tembo au akaenda kufanyia tukio Mtaani, au hata akamgonga Mtu Bahat mbaya.na kama ilivyo,Vitu vya kuazima sijui kwa nn watu wanakuwa na mbwembwe navyo. Mara nyingi huendesha kwa Maspeed ya mbwembwe na kufukia Mashimo bila ya kujua gharama ya Vipuli.
Jirani yangu aliwahi kuniazima gari aende kwenye dili lake Mara Moja. Kumbe alikuwa na Mtoko na demu wake.akalala na Gari yangu Night Club, asubuh ilipofika ananirudishia gari saa mbili asubuh huku mm nkiwa nshachelewa kwenda kazini. Na gari alikuwa ameigonga Nyuma. Nilisikitika sana. Tangia hapo ukawa ndio Mwisho wa kumuazima yoyote Gari. Ni afadhali umpatie 10,000 ya Taksi kuliko kmuazimisha mtu Gari yako.
Kitu Muhimu hawa wanaozima wasichokijua ni:
Gari sio Mafuta.Gari ikiwa inatembea Barabarani inakuwa na Mlolongo wa vitu vingi hadi unaiona inatembea Barabarani. Gari sio Mafuta tu. Hivyo unapoenda kuazima gari ya Mtu usifikirie kwamba Gari ni Mafuta Tu. Huwezi amini,kuna jamaangu eti ananipigia Simu kutaka kuazima gari ili akaangalie Mpira Eti Masaki. Inashangaza kwa Kweli. Kama Starehe unazipenda kwa nn usitafute na hela kwa ajili ya mambo yako ya Starehe Pia!????
Si unaazima kwa unaye mfahamu? Huwezi kurupuka tu! Kisa mshikaji huwa namuona kitaa hata kufahamiana vizuri hamfamiani!!!gari anaazima hadi ridhiwani kikwete sembuse wewe mlalahoi? au hamkusikia ridhiwani akisema msione anabadilisha magari tu hayo ni mambo ya kimjinimjini tu, yeye anamiliki toyota Camry moja tu.
wazungu walishapita kote huku ambako sisi leo mishipa ya shingo inatutoka na ndio maana walibuni rent car self driving, ili kuondokana na kumtukuza mtu kwa sababu ya makopo haya.