Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Mzee ES, karibu na pole ya kupotea na heshima na wewe...! sijasema CCM ni safi, nilisema kuwa kama wapinzani wataendelea kuwa jinsi walivyo, CCM bado ni chaguo la Watanzania wengi (sijabadili msimamo huo!) Pia nilisema kuwa ni kutokuwa mkweli mtu akisema CCM haijafanya jambo lolote zuri kwa wananchi (sijabadili msimamo huo pia) Nilichosema kwenye makala hii (ambayo hujaisoma) ni kuwa mazingira yakiwa sawa CCM itaondoka! Unabii ninauzungumzia siyo wa kwangu wala wa sheikh Yahya, bali ni yale mananeo ya Mwalimu "CCM siyo Mama yangu"! Sikusema pia kuwa CCM itaondoka kama ukungu la hasha, kuna mambo lazima yafanyike! Na msimamo huo bado sijaubadili pia.

Njia kubwa ya kumfundisha mtu siyo tu kumwacha aendelee kuboronga, ni kumweka pembeni na kumuonesha jinsi mambo yanavyopaswa kuwa. Kama matatizo yangekuwa mwalimu mzuri kuliko wote, CCM basi wangekuwa washafuzu! Nafikiri kwa wengine matatizo ni mwalimu mkali ambaye hana huruma! Kama mwanafunzi hafundishi darasani, wakati mwingine tunamhamisha shule au tunampeleka tuition! CCM kwa miaka arobaini imeelewa kidogo, lakini haijajifunza, hadi pale tutakapoipa darasa nje ya serikali ndio wanaweza kuelewa somo la utawala!
 
Hii posting inanoga tu kuisoma, lakini haina chembe ya point ndani yake.

Nilitarajia mwandishi atueleze process ya kuanguka kwa ccm, sio sababu za kuanguka kwake na siasa mpya zitakazojitokeza.

Tell us the process of ccm downfall. Tueleze kuanguka kwa ccm kutaanzia wapi na lini, nini hasa kita-triger kuanguka huku, je kuanguka huku kutaanza ndani ya ccm au kwenye kambi ya upinzani, je ccm itaangushwa na demokrasia au kimabavu, je kuanguka huku kutatokea hata kama demokrasia inapindishwa na ccm?

Unless these are answered, your posting doesn't add anything to current the understanding of the future of ccm.
 
Mzee Mwanakijiji,

Heshima yako mkuu, lakini I beg kukupinga bro, maneno yako pamoja na kwamba sijayasoma yote kutokana na shughuli nyingi ninajaribu kukielewa kichwa chako cha habari, na nimesoma mstari wa kwanza kwamba eti kuna siku wananchi wataamuka na kukuta CCM hawapo na ukataja baadhi ya viongozi wa CCM na serikali wengi wao wakiwa wastaafu na ambao hawahusiki kabisa na maaamuzi ya serikali yetu ya leo,

What a joke? eti serikali iliyochaguliwa kwa njia zote za kidemokrasia na zinazokubalika duniani katika civil world, kwamba itayeyuka tu au itaondoka tuuuu kama kusadikikika, unless sikuelewi vizuri, ila kama ninakuelewa vizuri ni kwamba uliyoyasema ni ndoto ya alinacha.

Wananchi wengi haturidhishwi na serikali na matendo yake, lakini what to do about it so far imekuwa ni hadithi kichaaaa, but kuwaaambia wananchi walale usingizi tu lakini siku moja kuna utabiri somewhere ulitabiriwa either na wewe au sijui ni Shehe Yahya, kwamba nji yetu itaamuka na kukuta CCM hawapo ni underst satement of the century bro!

............., but Mwalimu tunampa heshima kubwa kwa sababu kuna machache kati ya mazuri yametusaidia big time, otherwise viongozi wote waliowahi kuwa na wanaotaka kuwa wote ni bureeee, labda hii generation iondoke kwanza ndio watakuja viongozi wa kweli huko mbele, ninarudia wote ni bure, wewe Mwanakijiji majuzi tui ulikuwa unalia na watu hapa kuwa CCM ni safi na srikali ni bomba leo kulikoni blaza? ....
......., jana CCM leo kuwang'oa CCM, sounds like a sell out! sasa tofauti yako na Kaburu, Tambwe, na Lamwai ni nini?

Eti umegeuza mawazo yako over CCM kwa sababu kuna kiongozi mmoja wa CCM iliyekuudhi? that is all? Serikali ya awamu ya nne ina walakini, lakini pia nayo imeyarithi matatizo sugu ya toka tupate uhuru, na ina matatizo mengi tunyajua na tunayasema kila siku hapa ili yarekebishwe, na ni vyema kwamba awamu ya nne imeingia na kurithi matatizo makubwa, maana matatizo ndio mwalimu bora kuliko mwalimu yoyote duniani!

Mzee Es, I salute,

Nina hakika hapo juu si kwamba una hard feelings na Mzee Mwanakijiji kwa ghafla kuwa point blank aginst CCM; ila hapa napata hisia kwamba a part of you is: Mz Es - an intellectual of high caribre and intergrity and another part being a disappointed and frustrated Mtz who doesn't visualize our country as being in a state and process of seing a light at the end of the tunnel!

Maneno kama ya Mzee Mwanakijiji ndio moto unaopashwa kuwashwa huko kwa wapiga kura mbumbumbu (mimi nafanya hivyo: kila nipatacho kwenye forum lazima nikiwakilishe bush). Watanzania walio wengi mpaka sasa hivi hawaamini kama wana uhuru wa kujieleza au kutoa maoni yao bila kubughudhiwa wanafikiri ukiongea maneno kukosoa serikali utapelekwa pabaya. Mbaya zaidi, ikitokea mtu akapata maisha ahueni kwa sababu labda katika uchaguzi uliopita alichuma na sasa ana kibanda chake Tandale Squatter, ki corolla kakifanya teksi na huko Kinyerezi anafuga nguruwe - baasi huyo mtu ukimwambia serikali ya sasa hivi inaboronga mtapigana. Sasa watu kama hawa wanapaswa wapigiwe kelele ili wauone ukweli.

Mzee Es, inaonyesha kuwa disappointed kwamba haya mabadiliko ya kuipiga chini SiSiieem hayewezi kutokea kwa sasa labda generation ijayo! Does it matter as long as CCM are gone for ever? I think better late than never wqould be right phrase. Sisi humu wengi tunasikitika kwamba sisi tukisha ondoka duniani kizazi cha sasa kitatushangaa baadae - watatuona kama sisi wazazi hatukuwa either serious na life au tumepoteza muda wa maisha yetu tukiwa bila dira. TUWAPIGIE SISIIEM KELELE JUST FOR THE SAKE YA KIZAZI KIJACHO. Lakini nina imani pia hata 2025 inawezekana. Kingunge, Kawawa, Msuya, Malecela, Sitta, Msekwa and the like will definetely be gone while Mkapa, EL, FS, Mramba, Msabaha, SAS and the like will be too old to engage themselves into active politcs.
 
Mwanakijiji,
Hongera kwa nondo kali uliyoishusha angalau imesaidia kidogo kukausha machozi yangu.Kwani leo kila sehemu nilijaribu kusoma nimekutana na kashfa nzito zinazoihusu Siri-kali za wanamtandao wa CCM.
Nasikitika pia kuwa sijui ni wangapi wanapata fulsa ya kusoma makala kali na inayogusa kama hii.
Mwanasiasa,umenigusa sana kwenye suala la kupigika kwa watanzania.
Mie nami nilikuwa na wazo kama hilo ila ambacho nimegundua ni kuwa, the more wanavyopigika watanzania, the more they use less time on reasoning why??Hawatafuti chanzo cha tatizo bali wanazima tatizo kama zima moto.
 
Mzeee Wambadwa,

Heshima yako mkuu, ninakusikia mkuuu. maneno ya hamasa hapa bongo sidhani kama kuna ya kumzidi Mtikila, ambaye mpaka serikali kwa kuyaogopa huamua kumuweka ndani, lakini yamesidia nini? Kazi yote ya Freeeman, kwenye uchaguzi uliopita ikaishia kumpa Muuungwana kura 80%, wewe leo mwaka 2007, huko Majuuu kuna wabongo wanaenda kwenye mkutano wa rais na uniform ya CCM, bila hata aibu, leo watu tunaowaamini hapa kuwa ni nguzo ya upinzani wanasema kuwa eti kwa sababu mfanyakazi wa serikali ya CCM ametoa namba yake ya simu ya mkononi, na ukimpigia anajibu, basi ni kiongozi anayefaaaa, hivi ndugu yangu huoni kuwa bado tuna safari ndefu sana kuitoa CCm kwa kura?

Great, maneno ya Mwanakijiji yanatia moyo, sawa so is maneno ya Mtikila na Mrema, halafu at the end of the day wanaenda kulipwa na CCM sasa tunamuamini nani? Wewe unafikiri CCM hawajui kuwa Mrema mpaka leo hajaeleza zile dhahabu alizozikamata Airport akiwa waziri wa CCM ziko wapi? Sasa huyu atatuletea mabadiliko gani? Mtu wa kuaminika ni Freeman, ambaye sasa hivi ndio kwanza yuko shule ambayo CCM waliiisoma in the 50's, hivi kweli haya maneno ya Mwanakijiji yanatupeleka wapi? Au ndio feel good now, halafu do nothing?

Ndio maana mimi siku zote ninaikataaa issue ya Independent Candidates unless kuna mabadiliko ya kikatiba ili kuuuimarisha, maana ninajua CCM wataitumia kama walivyoitumia issue ya upinzani period! Watawaweka watu wao na kudai ndio independent wenyewe, matokeo yake wataendelea na ujanja! I mean nina heshima kubwa kwa Mzee Mwanakijiji, na mawazo yake siku zote ambayo no question kwamba huwa ni welll thought kabla ya kuyaaandika hapa, lakini kwenye solution ya matatizo tuliyonayo kisiasa na hasa kiuongozi, nina wasi wasi kuwa so far hakuna mwenye best ideas what to do, ingawa sio dhambi kujaribu kama Mzeee MJJ!
 
Mgonjwa wa Ukimwi, mimi sisemi maneno matupu, na mikakati ya kisiasa ni fani yangu. Kuhusu ni hatua gani zitatakiwa ili kuingusha CCM ukifuatilia maandiko yako hapo juu nimesema naandika mkakati wa kuing'oa CCM. Tatizo langu sifikiri kama kupost hapa itakuwa vizuri! So nikimaliza kuandika nitatafuta viongozi ambao wako tayari kuyafanyia kazi.

Siasa ni mikakati! Udhaifu mkubwa wa upinzani Tanzania ni kukosa mikakati ya kisiasa. Wanachofanya mara nyingi ni kuitikia (react) matendo ya CCM. Unless wao ndio wanailazimisha CCM kureact hawawezi kushinda!

Belive me, maneno niliyoyasema hapo juu si utani, ni jambo linalowezekana. Anayefikiria kuwa CCM itatawala milele yuko mbali sana na ukweli. Si mmemsikia Katibu Mkuu wa CCM akiwatambia huko Zanzibar kuwa wapinzani hawataingia Ikulu?
 
Mzee Mwanakijiji,

Usije sikia la mtu ndugu yangu, wewe sio mtabiri wa jinsi gani CCM itaanguka. Vyanzo vipo wazi pia njia zitajitokeza zenyewe lakini usifanye makosa ya utabiri...
 
Mgonjwa wa ukimwi nakuombea usife.Bado tunakuhitaji.Kazi unayofanya ya kuwaelimisha zaidi wakulima wetu kwa kuwafikishia nondo zito kama za akina Mwanakijiji,Mwanasiasa.Mkandala na wengineo ni muhimu sana.Hakuna kipindi ambacho nimekuja kujua umuhimu wa e-mail za ndugu,jamaa na marafiki kama baada ya kuujua huu mtandao.pamoja na umbali nilionao nahakikisha issue yeyote nzito inawafikia ili nao wakune vichwa.Huwaomba pia wapeleke kwa atleast watu 10 kila mmoja.Nataka nihakikishe 2010 napunguza kura za Chama cha majambazi kwa 50%
 
Nyangumi,

Heshima yako mkuu, now you are talking! Strong words na message kwa wote hapa ni clear toka hiyo posting yako ya mwisho!

I love it bro! maana inatia moyo on uchungu na nji yetu!
 
mimi naona ya kwamba watu wanajidanganya bila ya kuelewa wanaendesha mijadala ya aina gani.ni lazima watu wafahamu ya kwamba hivi sasa dunia yote ni moja kisiasa kiuchumi na kijamii,namaanisha ya kwamba baada ya kuanguka kwa mfumo wa kiislamu mwaka 1923, na baada kuanguka kwa mfumo wa kikomunisti ndani ya miaka themanini kwa sasa umebakia mfumo mmoja tu ambao unaitwa ubepari,mfumo huu kwa sasa ndio unatawala dunia nzima kisiasa,kijamii na kiuchumi.

Eleweni ya kwamba siasa ya demokrasia inatokana na mfumo huu wa kiuchumim wa kibepari,na kwa kweli mfumo huu wa kibepari una siri nyingi sana na ni complex kuzichambua kila mmoja akaelewa,kwa kweli mfumo wa kibepari umeigawa dunia katika makundi matatu kiuchumi kama inavyoeleweka dunia ya kwanza ya pili na ya tatu;na kutokana na mgawanyiko huu wa kiuchumi ni wazi kwamba hata utekelezaji wao wa demokrasia unatofautina.

Kwa wale wenye maisha ya dunia ya mwanzo wao ndio wanaishi katika demokrasia halisi na kwa kawaida wao huwa ndio walinzi wa demokrasia,na ndio wanaotoa maelekezo ni jinsi gani demokrasia itatekelezwa na makundi mawili yaliyobakia.Hapa sitoongelea siasa za nchi yeyote zaidi ya Zanzibar.

Kama nilivyosema mwanzo kwamba mfumo wa kibepari uko complex sana ndio maana inakuwa vigumu watu kuelewa wanaenda wapi baadhi ya wakati.Kwanza tujue kwamba kwa kawaida mfumo wowote wa maisha ni lazima uweke juhudi ya hali ya juu na ulinzi kamili wa kupambana na mifumo mingine kifikra na hata kimaada,kwa hakika mfumo wa kikomunisti hauwezi kuja juu tena kwani ulidondoshwa kifikra,lakini kwa uislamu ambao umedondoshwa kimaada ni rahisi kuja juu kwani fikra yake bado iko hai na inaeleweka(qur-an).Ndio maana kama mtaona kwa sasa jicho la dunia ya kwanza linaangalia zaidi kuyabana maeneo ambayo yanaonekana kwamba yanaweza kuwa mahala salama kwa waislamu kukaa na kuijadili fikra yao juu ya kuendesha tawala,kisiasa kijamii na kiuchumi;ndio maana leo kuna tafsiri ya jumla juu ya uislamu kwamba ni ugaidi,ili kuwatia watu hofu juu ya kutulia na kusikiliza fikra za kiislamu juu ya utawala na mambo mingine.

Sijatoka katika mada bado nakuja.

Tuelewe ya kwamba Tanzania(Zanzibar) iko Afrika,na ina waislamu wengi kiasi,kwa maana hiyo ni sababu tosha kwambaiendelee kuwa confused na concept of democracy,kwa sababu ni kwamba kwa sasa hao wenye dunia ya kwanza wameifanya Afrika kuwa ndio shamba ambamo wao watakuwa wanavuna mazao, ni wazi kwamba endapo waafrika watakuwa na siasa safi,basi itakuwa ni vigumu sana kwa watu wa dunia ya kwanza kuingia na kujikombea rasilimali, kwa maana hiyo ni lazi ma siasa za Afrika ziwe ni zisizoeleweka ili iwe ni rahisi kwa wao kuja kwa kutumia mgongo wa migogoro,kuweka misingi yao thaqili ya kiuchumi na kwa maana hiyo kuendelea kufaidika na matunda yake;kwa wao demokrasia wanayoitaka kwa waafrika ni kujenga imani tu kwamba demokrasia ndio suluhisho la matatizo yao tu basi.Hata kama inawatia matatizoni wataendelea kuitumia kwa ajili ya kutafuta suluhu kisha matatizo tena kisha suluhu,na huku wajanja wakitumia migongo ya matatizo na suluhu,kuweka misingi migumu ya kiuchumi na masharti ya misaada yasiyotekelezeka ili kuendelea kuzibana kiuchumi nchi za kiafrika.Katika kitovu hiki namalizia kwa kusema kwamba migogoro ya nchi za kiafrika inazinufaisha sana nchi za magharibi kiuchumi na kwa maana hiyo si rahisi kuondokana na migogoro kwani inaambukizwa kwa makusudi.

Kwa hapa Zanzibar au Tanzania naweza kusema kwamba endapo Marekani ambao ndio walinzi wa demokrasia namba moja,watataka CCM iache madaraka basi ni suala la kun-fayakun tena haipigwi hata risasi moja hata ile ya hewani,ni Bush tu kusema ondokeni haraka,siku ya pili tukiamka tunashuhudia serikali mpya,lakini kwa bahati hao Marekani ndio wanaoiweka CCM madarakani.kisha sisi kwa bahati mbaya tunaishia kuyumbishwa kifikra,mara Balozi wa Marekani ameionya CCM,mara sijui nini,kumbe hii ni kuwayumbisha watu na kuwajengea matumaini wale ambao wamedhulumiwa katika uchaguzi.
CCM ina masilahi makubwa kisiasa na kiuchumi kwa nchi za magharibi,kwa maana hiyo itaendelea kuishi madarakani kwa miaka inayotaka bila ya bughudha,hata kama itabaki na mfuasi mmoja na mgombea wake.Kwa maana hiyo tatizo la siasa za hapa sio CCM bali ni Magharibi na siasa yao nzima ya demokrasia na mtazamo wake juu ya nchi za dunia ya tatu.

Chengine abaa nataka tujue kwamba hata kwa mfano CUF ipate madaraka leo na kushikilia khatamu za uongozi basi hatutopata maendeleo kama tunavyotumai;na hali itakuwa mbaya zaidi kuliko sasa.........!
 
Shy you have a point...
Tumeshuhudia hayo kwa Palestina baada ya Hamas kushinda kidemokrasia lakini wakakataliwa!
 
Shy

endapo Marekani ambao ndio walinzi wa demokrasia namba moja,watataka CCM iache madaraka basi ni suala la kun-fayakun tena haipigwi hata risasi moja hata ile ya hewani,ni Bush tu kusema ondokeni haraka,siku ya pili tukiamka tunashuhudia serikali mpya,lakini kwa bahati hao Marekani ndio wanaoiweka CCM madarakani.kisha

Tafadhali Shy unaweza kukaa kimya eh! Kama wewe unawaogopa hao wamarekani au whatsoever, usilete mambo ya mzaa hapa, hizi porojo zako peleka kwenye udaku pleaseeeeeeeeeeee
 
CCM ina masilahi makubwa kisiasa na kiuchumi kwa nchi za magharibi,kwa maana hiyo itaendelea kuishi madarakani kwa miaka inayotaka bila ya bughudha,hata kama itabaki na mfuasi mmoja na mgombea wake.Kwa maana hiyo tatizo la siasa za hapa sio CCM bali ni Magharibi na siasa yao nzima ya demokrasia na mtazamo wake juu ya nchi za dunia ya tatu.

Chengine abaa nataka tujue kwamba hata kwa mfano CUF ipate madaraka leo na kushikilia khatamu za uongozi basi hatutopata maendeleo kama tunavyotumai;na hali itakuwa mbaya zaidi kuliko sasa.........!

Kila kitu Marekani mwe!
Yaani Marekani ndio waiosema tununue ndege ya Rais, tununue Radar, tuingizwe mkenge na Richmond? Kwanini wakati wa CUF kusiwe na mabadiliko endapo watakataa kusaini mikataba ya kijinga?
 
Kundi moja linaweza kujitoa na kuunda chama kipya au kujiunga na chama kingine. Hii inaweza kusababisha CCM isiwe na nguvu kama ilivyo sasa na hatimaye kupata Wabunge na Rais ambao watatoka katika chama kingine na kuleta mapinduzi ya kweli Tanzania, badala ya kuendelea na hawa majambazi wanaouza rasilimali za Tanzania kwa wageni na kuendelea kufuja mabilioni ya pesa za walala hoi.
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

CCM yanyemelewa na kashfa ya makundi

na Charles Mullinda

KUNA kila dalili za wazi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa kinanyemelewa na kashfa nzito ya viongozi wake kutokuwa na maadili mema ya uongozi, ambayo chanzo chake ni makundi yaliyoota mizizi ndani ya chama hicho.
Ingawa hakuna ushahidi wa wazi wa kulithibitisha jambo hilo, ushahidi usio na tone la shaka unaothibitishwa na hali ya mambo inavyoendelea sasa ndani ya chama hicho wakati kikielekea katika uchaguzi wa viongozi wake, unaonyesha hivyo.

Kuibuka kwa kashfa ya ufuska inayomwandama Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Amina Chifupa, ambayo imesababisha atalikiwe na mumewe, Mohamed Mpakanjia, ni mlolongo wa vita ya kuchafuana na kukashifiana, kwa nia ya kuwania madaraka.

Vita hiyo chafu ambayo imekuwa ikiendeshwa na kundi la wanamtandao, sasa inaonekana kushika kasi tena wakati chama hicho kikielekea katika uchaguzi wa viongozi wake, baada ya kutulia kwa muda, ulipomalizika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Amina, mmoja wa wabunge vijana wanaoibukia, na mwenye ushawishi katika kundi lake la vijana, anadaiwa kuundiwa kashfa ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake na kundi la wanamtandao, ambalo limekuwa na sifa ya kuwaengua katika mchuano wa kugombea nafasi za uongozi wale wanaotofautiana na kundi hilo.

Amina, ameingia katika mtego wa wanamtandao baada ya kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya juu ya uongozi wa Umoja wa Vijana wa chama hicho, UVCCM, nafasi ambayo inadaiwa kuwa tayari amekwishaandaliwa mtu wa kuirithi na wanamtandao, baada ya mwenyekiti wa sasa wa umoja huo kumaliza muda wake hivi karibuni.

Mwenyewe alikiri hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, alipozungumza na vyombo vya habari kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake, na kueleza kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM walikuwa wameamua kwa makusudi kuiharibu ndoa yake ili kupunguza kasi yake ya kuwania uenyekiti wa UVCCM.

Ingawa aliahidi kumtaja mmoja wa viongozi waliohusika na mpango huo, adhima yake hiyo haikufanikiwa baada ya kushindwa kufika Idara ya Habari (MAELEZO) kwa ajili ya kulipua bomu kama alivyopanga, kwa kile kilichoelezwa na baba yake mzazi, Hamis Chifupa, kuwa familia imemkataza.

Hata hivyo, Amina alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa kashfa ya ufuska iliyomfanya aachike kwa mumewe iliundwa na mmoja wa viongozi wa juu wa CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Kwamba, mumewe kabla ya kumpa talaka alionekana akitoka ofisini kwa kiongozi huyo wa CCM na serikali, kiongozi ambaye alikwisha kuonyesha nia ya kutomuunga mkono katika azima yake ya kuwania uenyekiti wa UVCCM.

Jambo hilo lilitafsiliwa na Amina mwenyewe pamoja na baadhi ya mashabiki wake kuwa kiongozi huyo ndiye aliyezusha uongo huo, lengo likiwa kumchafua ili ashindwe kutekeleza azima yake.

Mumewe Amina, naye amekwisha kukiri kufika ofisini kwa kada huyo wa CCM muda mfupi kabla ya kwenda kumtaliki mkewe, ingawa hajaweka wazi kitu walichokiongea na kada huyo wa CCM anayedaiwa kuwa mwanamtandao.

Kashfa hii inayodaiwa na Amina kuwa ni ya kuunda, inaingia katika orodha ndefu ya kashfa za aina hii zilizowahi kuwakuta wana CCM wengine waliokuwa wakipambana na kundi la wana mtandao katika chaguzi mbalimbali na kuonekana kuwa tishio.

Tuhuma za ufuska wa Amina zinaingia katika rekodi ndefu ya siasa za kuchafuliana majina zilizoanza kujitokeza waziwazi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, baada ya wagombea waliokuwa wakilipinga kundi la wanamtandao, kuandamwa na kashfa nyingi nzito, ambazo kwa kiasi kikubwa ziliwachafulia majina na kusababisha waonekana kuwa viongozi wasiofaa kushika hatamu za uongozi wa taifa hili.

Miongoni mwa waliokumbwa na makali ya joto la kuundiwa kashfa na kundi la wanamtandao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu Tatu, Frederick Sumaye, aliyekuwa mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Sumaye alikabiliana na wakati mgumu baada ya kuanza kuandamwa na vyombo vya habari ambavyo wakati akiingia madarakani vilimpamba kama kiongozi mchapakazi, vilipoanza kumshambulia kwa kuanika kashfa mbalimbali zilizodaiwa kufanywa naye, huku ikiwa haifahamiki chanzo cha kashfa hizo.

Kiboko kilichotumiwa na wanamtandao kumpiga Sumaye kilitumiwa pia kumchapa Profesa Mark Mwandosya ambaye alihusishwa na uuzaji mbaya wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), akidaiwa kuhongwa na wawekezaji walionunua kampuni hiyo.

Prof. Mwandosya alijikuta akichafuka vibaya mbele ya macho ya jamii baada ya kudaiwa kuwa kampuni iliyonunua TTCL ilimpa kazi mwanawe wa mwisho, na baadaye akadaiwa kuchangisha fedha za chama huku akiwa si mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Wengine waliokwisha kushughulikiwa na kundi hili la wanamtandao na kuonekana watu wasiofaa kushika nafasi za uongozi walizokuwa wakizitaka ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye alidaiwa kuwa Mwarabu, pamoja na kashfa nyingine nyingi mbaya ambazo ziliharibu kabisa sifa yake ya utumishi uliotukuka kwa taifa hili.

John Samuel Malecela, naye ni muhanga wa vita hii na alijeruhiwa kwa kukashifiwa kwamba Mwalimu Nyerere tangu awali hakumkubali kuwa kiongozi wa juu wa taifa na pia umri nao ulitumiwa kama kigezo cha kummaliza.

Kuibuka kwa vita ya kuchafuana ndani ya CCM kulianza kuonekana katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ambayo ina wanachama wengi katika kundi la wanamtandao, baada ya Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo, Dk. Emmanuel Nchimbi, kutofautiana na aliyekuwa Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Frank Uhalula.

Mgogoro baina ya viongozi hao wa UVCCM ulimlazimisha Rais Mkapa kuamua kuwatenganisha kwa kuwapangia majukumu makubwa yaliyowafanya wasikae pamoja makao makuu ya umoja huo kwa muda mrefu.

Dk. Nchimbi ambaye alikuwa tayari amekwishamvua madaraka ya Katibu Mhamasishaji, Uhahula, na kuyakabidhi kwa Dk. Diodorus Kamala, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Uhahula aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya.

Kinachoashilia kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanakerwa na tabia hiyo ya kukashifiana ambayo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na kuwapo kwa makundi, ni hatua ya hivi karibuni ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuyavunja makundi ndani ya chama hicho.
 
ninaunga mkono maoni yako kwa asilimia mia moja. Ndiyo maana tuliwahi kusema kuwa makundi haya ndiyo mwanzo wa mwisho wa CCM
 
Hata kama ikitokea kumeguka kwa CCM kwa kupitia haya makundi ,Je yatamsadia vipi Mwananchi wa kawaida Katika kuleta maisha bora kwa wote?
 
Mzee Kei,

Hapo umenena sana bro, na ndio hasa inapaswa kuwa lengo letu hapa forum ni kutafuta what is there for us wananchi, ama sivyo tunakuwa wasaniii kama hao the makundis!
 
Nawaunga mkono. Makundi yanayotokana na masilahi na sio fikra hayana faida kwa watanzania. Ni hasara na hatri kubwa kwa taifa letu maana yanaweza kulivunja taifa letu ukichukulia Chama na dola hakuna tofauti yupi ni yupi.

Tanzanianjema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom