Kuagwa kwa Marehemu Dk. Mvungi - ITV

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
1,718
Reaction score
463
Kupitia kituo cha Television cha ITV, kazi ya kuagwa kwa gwiji la Sheria na Siasa ndo imeanza muda huu. Tufuatilie...




Marehemu Sengondo Mvungi 1952 - 2013​

-----------------------------------------

Nami nipo hapa Karimjee kumuaga mwalimu wangu, rafiki yangu...alikuwa mtu mwema na mwenye upendo wa kweli. RIP Dkt. Sengondo Mvungi.

Mwanadamu kumbuka kuwa u-mavumbi wewe na mavumbini utarudi. Ni maneno yaliyoko katika wimbo unaoendelea sasa... Pumzika kwa amani - Dr. Edmund Sengondo Mvungi.


Waraka wa Mh. Rais Dr. J.M.Kikwete unsomwa kwa niaba yake na Makamu wa Rais. ...Dr. E.S.A.Mvungi alikuwa mzalendo wa kweli na mahili katika fani, ndo maana sikusita kumteuwa kuwa mjumbe wa tume...

Sala fupi ya Buriani inatolewa na Padri Mvungi...

MBATIA - Tukishampumzisha Dr. E.S.A. Mvungi kwa nguvu hiyohiyo tuitumie kulinda uhai wa wananchi wetu. Mh.Mbatia.

Mvua nayo inanyesha hapa kusindikiza mwili wa mpendwa Mvungi

JK: "...ni msiba wetu sote, majonzi yenu ni yetu sote...sote tumshukuru Mungu kwa fursa ya kuishi na marehemu..."

Ujumbe wa padri Kabla ya kulala hakikisha umelala baada ya kutubu makosa(dhambi) kwa Mungu kqma kuna mtu kakuudhi/kakukosea msamehe nawe kama umemkosea omba akusamehe ili ulale na Amani yaeezekana ukawa ni mlalo wako wa mwisho hapa duniani



Wanajamvi

Mhe. Mwingulu akitoa salamu za Chama kuaga Mwili wa Marehemu Dk. Mvungi.

Amekiri katika Salamu kuwa mambo ya ukatili yanayotokea Tanzania Serikali ichukue hatua.

Lakini yeye anaona, "Roho ya mauti na Mapepo"
Ndo yanafanya haya.


Shuhuli za kuuaga mwili zimeisha na jeneza limefungwa na mvua imekatika kabisa, Itv nao wanafunga kipindi kurusha hii shuhuli live. Mimi pia nalog off.
MUNGU ALITOA NA SASA KATWAA JINA LAKE LIBARIKIWE

Shughuli imekamilika, asanteni Watanzania. Mtetezi wa Serikali tatu katangulia sisi nyuma yake. Asanteni wana JF na hasa mods kwa kuboresha post #1 .

 
Pumzika Dr Mvungi ya duniani umemaliza.
 
Dr. Sengondo alifahamu kuchunga mbuzi na ng'ombe.
 
Duh! alikuwa akiuwa nyoka kwa kuwakanyaga kwa mguu/miguu. Anyway msukumo wake wa kusomea sheria ilikuwa ni kupamabana na mfumo wa kibepari
 
Nami nipo hapa Karimjee kumuaga mwalimu wangu, rafiki yangu...alikuwa mtu mwema na mwenye upendo wa kweli. RIP Dkt. Sengondo Mvungi.
 
Mavumbini tutarejea!!!!!

Muumba akupe pumziko la amani.
 
Mvua hii inamlilia dk Edmund sengodo mvungi, Mungu amrehem. Hakika hataenda bure.
 
Mvua kubwa sana inanyesha...mh Mbatia analia
 
Alikuwa hajui kuchukia, alipenda kila mtu, hakuwa na makuu. Hakika hata mimi machozi yamenitoka.wamemuua akiwa hana kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…