Kuachana na mke wa ndoa (christian) ni kweli biblia imezuia?

Mathayo 5:32
Lakini mimi nawambieni, kila mtu amachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini
 
Ili ndoa iwe ndoa lazima itimize vigezo..

Kigezo kikuu ni upendo wa mke na mume.

Kupigana ngumi kila siku na suluhu hamna hiyo sio ndoa..

Kuishi bila mawasiliano yyt hata salamu tu hakuna hiyo sio ndoa

Mmoja wenu kutojali familia hiyo sio ndoa.

Kutokubaliana kwa jambo lolote lile mnalopanga kama wanandoa hiyo sio ndoa

Kupigana mangumi kila mara mpaka kutiana vilema hamna ndoa hapo.

NDOA SI GEREZA. Watu wanatafsir maandiko vibaya.

Kama Mungu tu hakulazimishi kuabudu, sembuse swala ndoa.?

Kumbuka pamoja na mitume kuwa inspired na roho mtakatifu (kwa mujibu wa biblia) kuandika maandiko ya biblia Lakin pia target yao kibinadamu ilikuwa kufikisha ujumbe kwa jamii wanazoishi ndani yake na zinazowazunguka. Wasingeongelea jamii ambazo zingekuwepo karne ya 21.

Na ndo maana kuna mambo mengi yapo kwenye maandiko yameamriwa yafanywe leo hii wengi hawayafuati kwa sababu hayakidhi tamaduni tulizonazo leo na hayana madhara ya kiroho hata kidogo kama hukuyafuata.

Maandiko ni kiongozi lakini ROHO MTAKATIFU ni kiongozi mkuu.

Mungu alimuumbia mwanadamu utashi na akili kwa sababu alijua kuna mambo atahitajika atumie utashi na akili ili aishi vizuri.

Ukipigwa ngumi na mmeo kila siku mpaka unavunjika taya au unapewa stress na mkeo mpaka unapata kiharusi eti kisa "biblia imesema tusiachane", huo utakuwa ni upumbavu wako na utakufa kwa sababu ya upumbavu wako na Mungu hatolaumiwa kwa upumbavu wako.

NDOA SI GEREZA.

Mungu hakuruhusu ndoa ije kuwa mzigo mzito kwa mwanadamu.

Kuweni wapole kama hua na wajanja kama nyoka (kwa mujibu wa biblia)
Yoote yanaangukia kwenye upendo. Ukianza na huo basi kila kitu kinakaa kwenye mstari.

Sometimes tunakuwa ving'ang'anizi.. Unataka tuuuu unasahau its two way traffic. Umpende akupende.. Na sio vingine.

Halafu ukishakuta sio.. Mnang'ang'ana kuonekana mmo.. Na ndio uharibifu unapozidi kuwa mkubwa. There is no coming back safely from that kind of marriages.
 
Ukifuatilia wanandoa wanaochomana visu na kuuana au kutiana vilema upendo wa mke na mme uliisha miaka mingi sana iliyopita.. Walikuw wakiishi kwa kuviziana. Hapo mtu anakwambia eti hao watu waendelee kuishi pamoja.

Mme kila siku anamtishia bastola mkewe, mke anamtishia mmewe kisu lakini mtu anakwambia kwa sababu walioana kanisani wanatakiwa wasiachane. Kesho utasikia mtu kafumuliwa ubongo na bastola au mtu kachomwa kisu utumbo wote nje.

Uhalali wa ndoa ni upendo na si suała la mwanamke na mwanaume kufungia ndoa kanisani. Kama ndoa haina upendo hao watu waachane mara moja kabla madhara hayajatokea
 
Hii kuishi kwa kuwa mnawaogopa nanii na nanii ni mambo hatari. Too bad sumu yake inatambaa taratibu na watoto mnawagawa majirani wanagawanywa ...marafiki yaani kung'ng'ana ni htr mno.
 
Ndugu yangu mimi nimeisoma Biblia na kiasi nafahamu maandiko yanavyosema. Swala la kuoa au kuolewa sio jambo la mchezo hata kidogo. Kwetu sisi wanaume, unaweza ukaoa mwanamke halafu ukajuta sana baadae. Katika swala la ndoa Biblia imetupendelea sana wanaume kwa sababu, kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume ndio aliumbwa wa kwanza na BWANA MUNGU. Hivyo basi, mwanaume ndio kichwa katika familia; kwa maana nyingine, mwanaume ndio mkuu au mtawala katika ndoa. Ukisoma Mwanzo 3:16 "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." Hapa utaona wazi kabisa BWANA MUNGU alisema mke, atatawaliwa na mumewe.
Sasa baada ya utangulizi huo turudi kwenye hoja yako ya kwamba, je, kumuacha mke wa ndoa (christian) ni kweli Biblia imezuia? Mimi binafsi naweza kukujibu ya kuwa Biblia haijazuia kumuacha mkeo wa ndoa. Biblia imefafanua kwa uwazi kabisa sababu zinazokubalika kumuacha mkeo wa ndoa. Kabla Yesu hajazaliwa duniani, wana wa Israeli walipewa sheria na BWANA MUNGU kupitia kwa Musa. Sheria hii ilikuwa inawaelezekeza wana wa Israeli namna ya kuishi na mambo yote yakiwamo pia mambo ya ndoa. Ukisoma katika Kumbukumbu La Torati 22:13 mpaka 21, utaona kwamba mwanaume alipewa ruhusa kumuacha mkewe kama siku ya ndoa hakumkuta na bikira. Tena sio kumuacha tu, bali mwanamke huyu adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa.(Soma kifungu hicho kwenye Biblia utaelewa, hapa siwezi kukiandika maana ni kirefu mno.) Kuhusu talaka imeandikwa hivi, "Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake,(yaani asipopendezwa na huyo mwanamke) kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha,(talaka), akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake , ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, MUNGU wako, iwe urithi." Kumbukumbu La Torati 24:1 mpaka 4u Hivyo basi ndugu yangu kwa kifungu hicho utaona kwamba, mwanaume alipewa ruhusa kumwacha mkewe wa ndoa, pale alipojisikia kufanya hivyo.
Lakini, baada ya Yesu Kristo kuja duniani, aliulizwa swali kuhusu hili jambo la talaka, na Bwana Yesu, bila kuficha kitu, alilitolea jambo hili ufafanuzi zaidi. Ukisoma katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11, imeandikwa hivi; "Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba, mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha MUNGU, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa."
Hapa sasa utaona wazi kabisa Biblia haijakataza kumwacha mke, unaruhusiwa kumpatia mkeo hati ya talaka kama tu amefanya uasherati, yaani amefanya mapenzi nje ya ndoa yenu. Kwa mujibu wa maneno ya Bwana Yesu, huna ruhusa kumpatia mkeo talaka kama amefanya makosa mengine ambayo sio uasherati. Kama unaushahidi ya kuwa mkeo amefanya uasherati, basi, ruksa kumapatia hati ya talaka na kuoa mke mwingine. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitafsri kifungu hichi kimakosa kabisa. Kuna watu wanasema eti ukisha muacha mkeo huna ruhusa ya kuoa mke mwingine. Hilo sio kweli hata kidogo. Kama umesoma vizuri kifungi hicho, (Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11) utaona ya kwamba, kama umemuacha mkeo kwa sababu zako zingine, basi huna ruhusa kuoa mke mwingine, na yeye mkeo uliyemuacha, pia, hana ruhusa ya kuolewa na mtu mwingine, sababu kwa kufanya hivyo wote mtakuwa mnazini. Lakini, ikiwa mkeo ni muasherati, basi unayo ruhusa kumwacha na kuoa mke mwingine.
Hakika jambo la ndoa ni gumu sana, ndio maana hata wanafunzi wa Yesu waliposikia majibu yake, walisema kama mambo ya mke na mume yako hivyo, basi ni bora kukaa bila kuoa. Ni kweli kabisa, mambo ya mke na mume ni magumu sana kwani unaweza ukaoa leo mke ukiwa unampenda kabisa, lakini baada ya muda fulani kupita, ukajikuta hutamani hata kumuona, achalia mbali kulala naye kitanda kimoja! Hapo sasa huna ruhusa ya kumuacha kama hajafanya uasherati. Inawezekana kabisa mwanamke akawa kero katika matendo mengine, lakini kama hafanyi uasherati, ndugu yangu huo ni mzigo wako, inabidi uvumilie tu, hakuna jinsi nyingine. Ndio maana Bwana Yesu alisema pia kuwa jambo la kukaa bila kuoa, sio kila mtu anayeweza kukaa bila kuoa bali wale tu waliojaliwa. Yapo maandiko mengi sana yanayozungumzia jambo hili la ndoa. Nikisema niyaandike yote, hakika sitaweza kumaliza kuandika. Lakini naamini kwa vifungu hivyo nitakuwa nimeweza kujibu swali lako la msingi.
Hitimisho la haya yote ni kwamba Biblia haijakataza kumuacha mke wa ndoa. Biblia imetoa ruhusa kumuacha mke pale tu inapodhihirika ya kuwa mke husika ni muasherati. Kama mkeo ni muasherati, basi unaruhusiwa kabisa kwa mujibu wa Biblia kumpatia hati ya talaka. Nakutakia kila la kheri katika ndoa yako ndugu yangu.
Ukiwa na nafasi unaweza ukajisomea vifungu vifuatavyo kutoka kwenye Biblia;
1 Wakorintho 7:1 mpaka 40.
1 Wakorintho 13:1 mpaka 13.
Waefeso 5:22 mpaka 33.
Wakolosai 3:18 mpaka 21.
Marko Mtakatifu 10:1 mpaka 12.
.
Umejitahidi sana mkuu ila kuna mambo fulani umeyasoma ndivyo sivyo. Mfano wa hiyo matayo 19:3 Bwana Yesu aliposema "haimpasi mwanamme kumwacha mkewe na kuoa mwingine kwa sababu yoyote ila kwa habari ya uasherati, na yule aliyeachwa(kwa sababu ya uasherati), akiolewa azini, na huyo (mwanaume) atakae muoa azini.
Sasa sentesi hii ya Bwana Yesu ni kama unaweza kuisoma hivi:- Mwanamume atamwacha mkewe na kuoa mwingine ikiwa kutakuwa na uasherati kwa huyo mke.
Mlango wa ndoa kwa huyo mwanamke haujafunguliwa kuolewa ila umefunguka kwa huyo mtu mume kuoa, maana kama ungefunguka kwa huyo mtu mke, basi isingelikua tena uzinzi dhidi ya yule aliyemwacha kwa huyo mpya atakaye mwoa.
Maana yake hapo ni kwamba kitakachoruhusu mwanamke aliyeachika kwa sababu ya uasherati ni kifo cha yule aliyemwacha. Pia kuna mkanganyo kwa watu katika ufafanuzi wa maana au ujuzi juu ya neno "uasherati" na "uzinzi"
Inavyofahamika uzinzi ni kwa wanandoa walioruhusika tayari kuishi pamoja kingono. Na hakuna kuachana kwa sababu ya uzinzi.
Uasherati ni mahusiano ya kingono kwa watu ambao hawajaruhusika kuishi pamoja na kuwa na mahusiano kingono. Hapa ndio kuna kuachana kwa sababu ya uasherati. Mwanamume anayo ruhusa ya kumwacha mke aliyemposa na kuoa mwingine ikiwa tu atapata ushahidi wa mke aliyemposa kufanya ngono na mwanaume mwingine baada ya kumposa.
 
Kama mwanamke kazin unaruhusiwa kumuacha na je kama mwanaume kazin ww. Huruhusiwi kumuacha? mbona din imemkandamiza sana mwanamke? Kwa ukandamizaji huu kila mwanamke asingependa kuwa mwanamke maana hakuna mtu anayependa kukandamizwa
 
Biblia Inakuitaji utoe talaka KWA DHAMBI YA UZINZI TUUU.

Nimekuelewa . NI UZINZI TU . Kuna kesi inaendelea mwanamke alikodi watu wa kwenda kumuua mumewe pamoja na mtoto wake mkubwa aliyezaa na mwanamke mwingine kabla ya ndoa yao ya kikristo na mumewe ili aweze kurithi mali . Wale Jamaa walichukua pesa lakini kwa huruma yao wakamtonya jamaa na kumpa ushahidii . HAPA MUMEWE HARUHUSIWI KUMWACHA . Asubiri dhambi ya UZINZI , ambayo ni ngumu sana kudhibitisha .
 
Hapo Mkuu ,uchaguzi niwako , ukimwacha nisawa ..maana hata Bible inahesabu km dhambi kitendo chakuua.
 
Nimekuelewa . NI UZINZI TU . Kuna kesi inaendelea mwanamke alikodi watu wa kwenda kumuua mumewe pamoja na mtoto wake mkubwa aliyezaa na mwanamke mwingine kabla ya ndoa yao ya kikristo na mumewe ili aweze kurithi mali . Wale Jamaa walichukua pesa lakini kwa huruma yao wakamtonya jamaa na kumpa ushahidii . HAPA MUMEWE HARUHUSIWI KUMWACHA . Asubiri dhambi ya UZINZI , ambayo ni ngumu sana kudhibitisha .
.
Ni andiko lipi katika injili linasema kuna kuachana kwa sababu ya uzinzi? Hakuna!
Ndio maana mkisharuhusika kuishi maisha ya ndoa ndani ya ukristo hakuna talaka. Kitakachowaachanisha ni kifo.
Hata hivyo mnaweza kuishi maisha ya kujitenga kila mtu kivyake lakini haimaanishi ni divorce, na ukichepuka tu unazini kinyume na mwenzi wako. Na hivyo unastahili hukumu.
 
Kama mwanamke kazin unaruhusiwa kumuacha na je kama mwanaume kazin ww. Huruhusiwi kumuacha? mbona din imemkandamiza sana mwanamke? Kwa ukandamizaji huu kila mwanamke asingependa kuwa mwanamke maana hakuna mtu anayependa kukandamizwa
Ni wapi Biblia imesema mwanaume "akizini" mke wake hana ruhusa ya kumwacha? NENO la MUNGU halina upendeleo wala "ukandamizaji". MUNGU ni mwenye haki na kamwe hamuonei kiumbe yeyeto yule. Kama mumeo amezini na wewe unataka kumwacha, unayo ruhusa kuomba akupe talaka. Lakini kumbuka kwamba BWANA YESU alisema mtu akikukosea na kukuomba msamaha; msamehe, hata kama akikosa sabini mara saba na kuomba msamaha basi wewe msamehe. Ukimsamehe mwenzako na wewe BABA MUNGU atakusamehe makosa yako na utafanyika kuwa "mwana wa MUNGU" na kuurithi UFALME WA MBINGUNI ambao umekaribia kuja. MUNGU wetu ni upendo, na upendo hauhesabu makosa, bali huvumilia katika yote.
 
.
Umejitahidi sana mkuu ila kuna mambo fulani umeyasoma ndivyo sivyo. Mfano wa hiyo matayo 19:3 Bwana Yesu aliposema "haimpasi mwanamme kumwacha mkewe na kuoa mwingine kwa sababu yoyote ila kwa habari ya uasherati, na yule aliyeachwa(kwa sababu ya uasherati), akiolewa azini, na huyo (mwanaume) atakae muoa azini.
Sasa sentesi hii ya Bwana Yesu ni kama unaweza kuisoma hivi:- Mwanamume atamwacha mkewe na kuoa mwingine ikiwa kutakuwa na uasherati kwa huyo mke.
Mlango wa ndoa kwa huyo mwanamke haujafunguliwa kuolewa ila umefunguka kwa huyo mtu mume kuoa, maana kama ungefunguka kwa huyo mtu mke, basi isingelikua tena uzinzi dhidi ya yule aliyemwacha kwa huyo mpya atakaye mwoa.
Maana yake hapo ni kwamba kitakachoruhusu mwanamke aliyeachika kwa sababu ya uasherati ni kifo cha yule aliyemwacha. Pia kuna mkanganyo kwa watu katika ufafanuzi wa maana au ujuzi juu ya neno "uasherati" na "uzinzi"
Inavyofahamika uzinzi ni kwa wanandoa walioruhusika tayari kuishi pamoja kingono. Na hakuna kuachana kwa sababu ya uzinzi.
Uasherati ni mahusiano ya kingono kwa watu ambao hawajaruhusika kuishi pamoja na kuwa na mahusiano kingono. Hapa ndio kuna kuachana kwa sababu ya uasherati. Mwanamume anayo ruhusa ya kumwacha mke aliyemposa na kuoa mwingine ikiwa tu atapata ushahidi wa mke aliyemposa kufanya ngono na mwanaume mwingine baada ya kumposa.
Tatizo ni watu kutafsri kila kitu kwenye Biblia. Siyo kila NENO lililoandikwa kwenye Biblia ni mafumbo. Maandiko mengine yako wazi kabisa wala huna haja ya kutafsiri. Soma vizuri huo mstari na utaona. YESU alisema mtu hana ruhusa kumwacha mkewe "ISIPOKUWA TU KWA HABARI YA UASHERATI". Sasa hapo unatafsiri kitu gani tena. Mfano umeambiwa "USIIBE", hapo utataka kutafsiri hilo neno "usiibe"? Talaka imeruhusiwa, na sababu ya kutoa talaka ni moja tu; UASHERATI basi. Hata Mtume Paulo alisema kama mkeo hana imani ya YESU KRISTO na wewe unaamini, na kama hataki kuamini kama wewe na akitaka kuondoka sababu ya tofauti ya imani basi unaruhusa ya kumwacha aondoke zake. Soma 1 WAKORONTHO 7:15. Lakini mtu yoyote yule ambaye ni MKRISTO anapaswa kujali sana "msamaha". Kama mkeo au mumeo amekukosea hata kama kwa kufanya uasherati au uzinzi, mnatakiwa kusameheana makosa yenu. Huo ndiyo upendo wa KWELI, upendo ni kusameheana kama ambavyo BABA MUNGU anavyotusamehe sisi makosa yetu kila siku.
 
Kwani viongozi wako wa dini hauwaamini wanachokufundisha? Kama hauwaamini ni nani mwingine utamuamini?. NB: Utakapo enda kupewa mafundisho na viongozi wako usiende ukiwa tayari na majibu au interests zako kichwani! Kwa mfano mimi ni mu islamu,baada ya kuona nyama ya nguruwe huwa imenona muda wote na watu wengi huwa wanaila,naweza kwenda kwa sheikh wangu na kuanza kumsumbua kwamba ni wapi aya kwenye quran inayokataza kula kitimoto! Thats insane!.
That's reasonable thinking.
Mtu asiehoji ni kama mfu.
 
Ndugu yangu mimi nimeisoma Biblia na kiasi nafahamu maandiko yanavyosema. Swala la kuoa au kuolewa sio jambo la mchezo hata kidogo. Kwetu sisi wanaume, unaweza ukaoa mwanamke halafu ukajuta sana baadae. Katika swala la ndoa Biblia imetupendelea sana wanaume kwa sababu, kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume ndio aliumbwa wa kwanza na BWANA MUNGU. Hivyo basi, mwanaume ndio kichwa katika familia; kwa maana nyingine, mwanaume ndio mkuu au mtawala katika ndoa. Ukisoma Mwanzo 3:16 "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." Hapa utaona wazi kabisa BWANA MUNGU alisema mke, atatawaliwa na mumewe.
Sasa baada ya utangulizi huo turudi kwenye hoja yako ya kwamba, je, kumuacha mke wa ndoa (christian) ni kweli Biblia imezuia? Mimi binafsi naweza kukujibu ya kuwa Biblia haijazuia kumuacha mkeo wa ndoa. Biblia imefafanua kwa uwazi kabisa sababu zinazokubalika kumuacha mkeo wa ndoa. Kabla Yesu hajazaliwa duniani, wana wa Israeli walipewa sheria na BWANA MUNGU kupitia kwa Musa. Sheria hii ilikuwa inawaelezekeza wana wa Israeli namna ya kuishi na mambo yote yakiwamo pia mambo ya ndoa. Ukisoma katika Kumbukumbu La Torati 22:13 mpaka 21, utaona kwamba mwanaume alipewa ruhusa kumuacha mkewe kama siku ya ndoa hakumkuta na bikira. Tena sio kumuacha tu, bali mwanamke huyu adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa.(Soma kifungu hicho kwenye Biblia utaelewa, hapa siwezi kukiandika maana ni kirefu mno.) Kuhusu talaka imeandikwa hivi, "Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake,(yaani asipopendezwa na huyo mwanamke) kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha,(talaka), akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake , ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, MUNGU wako, iwe urithi." Kumbukumbu La Torati 24:1 mpaka 4u Hivyo basi ndugu yangu kwa kifungu hicho utaona kwamba, mwanaume alipewa ruhusa kumwacha mkewe wa ndoa, pale alipojisikia kufanya hivyo.
Lakini, baada ya Yesu Kristo kuja duniani, aliulizwa swali kuhusu hili jambo la talaka, na Bwana Yesu, bila kuficha kitu, alilitolea jambo hili ufafanuzi zaidi. Ukisoma katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11, imeandikwa hivi; "Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba, mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha MUNGU, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa."
Hapa sasa utaona wazi kabisa Biblia haijakataza kumwacha mke, unaruhusiwa kumpatia mkeo hati ya talaka kama tu amefanya uasherati, yaani amefanya mapenzi nje ya ndoa yenu. Kwa mujibu wa maneno ya Bwana Yesu, huna ruhusa kumpatia mkeo talaka kama amefanya makosa mengine ambayo sio uasherati. Kama unaushahidi ya kuwa mkeo amefanya uasherati, basi, ruksa kumapatia hati ya talaka na kuoa mke mwingine. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitafsri kifungu hichi kimakosa kabisa. Kuna watu wanasema eti ukisha muacha mkeo huna ruhusa ya kuoa mke mwingine. Hilo sio kweli hata kidogo. Kama umesoma vizuri kifungi hicho, (Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11) utaona ya kwamba, kama umemuacha mkeo kwa sababu zako zingine, basi huna ruhusa kuoa mke mwingine, na yeye mkeo uliyemuacha, pia, hana ruhusa ya kuolewa na mtu mwingine, sababu kwa kufanya hivyo wote mtakuwa mnazini. Lakini, ikiwa mkeo ni muasherati, basi unayo ruhusa kumwacha na kuoa mke mwingine.
Hakika jambo la ndoa ni gumu sana, ndio maana hata wanafunzi wa Yesu waliposikia majibu yake, walisema kama mambo ya mke na mume yako hivyo, basi ni bora kukaa bila kuoa. Ni kweli kabisa, mambo ya mke na mume ni magumu sana kwani unaweza ukaoa leo mke ukiwa unampenda kabisa, lakini baada ya muda fulani kupita, ukajikuta hutamani hata kumuona, achalia mbali kulala naye kitanda kimoja! Hapo sasa huna ruhusa ya kumuacha kama hajafanya uasherati. Inawezekana kabisa mwanamke akawa kero katika matendo mengine, lakini kama hafanyi uasherati, ndugu yangu huo ni mzigo wako, inabidi uvumilie tu, hakuna jinsi nyingine. Ndio maana Bwana Yesu alisema pia kuwa jambo la kukaa bila kuoa, sio kila mtu anayeweza kukaa bila kuoa bali wale tu waliojaliwa. Yapo maandiko mengi sana yanayozungumzia jambo hili la ndoa. Nikisema niyaandike yote, hakika sitaweza kumaliza kuandika. Lakini naamini kwa vifungu hivyo nitakuwa nimeweza kujibu swali lako la msingi.
Hitimisho la haya yote ni kwamba Biblia haijakataza kumuacha mke wa ndoa. Biblia imetoa ruhusa kumuacha mke pale tu inapodhihirika ya kuwa mke husika ni muasherati. Kama mkeo ni muasherati, basi unaruhusiwa kabisa kwa mujibu wa Biblia kumpatia hati ya talaka. Nakutakia kila la kheri katika ndoa yako ndugu yangu.
Ukiwa na nafasi unaweza ukajisomea vifungu vifuatavyo kutoka kwenye Biblia;
1 Wakorintho 7:1 mpaka 40.
1 Wakorintho 13:1 mpaka 13.
Waefeso 5:22 mpaka 33.
Wakolosai 3:18 mpaka 21.
Marko Mtakatifu 10:1 mpaka 12.

kama ni marks nakupa 100%
 
Kwanza ukumbuke Yesu aliulizwa kama suala la kuoa ni lazima?

Yesu alijibu kuwa siyo lazima kuoa, ni ruksa kukaa bila kuoa lakini akasisitiza kuwa, kama unahisi huwezi kukaa bila kuoa basi ni heri uoe ili kuepuka kutenda dhambi kwa sababu hata ukimtizama mwanamke ambaye si mkeo kwa matamanio basi unakuwa umezini.

Kuhusu talaka mkuu, Biblia inasisitiza kuwa Mungu anachukia talaka na Yesu mwenyewe anasisitiza kuwa kilichounganishwa na Mungu (ndoa takatifu) basi binadamu asikitenganishe.

Aidha, mume anaruhusiwa kumuacha mkewe kama tu mkewe amefanya uasherati (kufanya mapenzi nje ya ndoa).. Hata hivyo Biblia inasisitiza kuwa na uhakika kuwa mkeo ni muasherati.

Pia, suala la talaka siyo la lazima hata kama mkeo ni muasherati unaweza kumsamehe na ndoa ikaendelea kwa kuwa Biblia inasisitiza msamaha kwa kuwa hata wewe hujakamilika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom