Kuachana na mke wa ndoa (christian) ni kweli biblia imezuia?

Ndugu yangu mimi nimeisoma Biblia na kiasi nafahamu maandiko yanavyosema. Swala la kuoa au kuolewa sio jambo la mchezo hata kidogo. Kwetu sisi wanaume, unaweza ukaoa mwanamke halafu ukajuta sana baadae. Katika swala la ndoa Biblia imetupendelea sana wanaume kwa sababu, kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume ndio aliumbwa wa kwanza na BWANA MUNGU. Hivyo basi, mwanaume ndio kichwa katika familia; kwa maana nyingine, mwanaume ndio mkuu au mtawala katika ndoa. Ukisoma Mwanzo 3:16 "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." Hapa utaona wazi kabisa BWANA MUNGU alisema mke, atatawaliwa na mumewe.
Sasa baada ya utangulizi huo turudi kwenye hoja yako ya kwamba, je, kumuacha mke wa ndoa (christian) ni kweli Biblia imezuia? Mimi binafsi naweza kukujibu ya kuwa Biblia haijazuia kumuacha mkeo wa ndoa. Biblia imefafanua kwa uwazi kabisa sababu zinazokubalika kumuacha mkeo wa ndoa. Kabla Yesu hajazaliwa duniani, wana wa Israeli walipewa sheria na BWANA MUNGU kupitia kwa Musa. Sheria hii ilikuwa inawaelezekeza wana wa Israeli namna ya kuishi na mambo yote yakiwamo pia mambo ya ndoa. Ukisoma katika Kumbukumbu La Torati 22:13 mpaka 21, utaona kwamba mwanaume alipewa ruhusa kumuacha mkewe kama siku ya ndoa hakumkuta na bikira. Tena sio kumuacha tu, bali mwanamke huyu adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa.(Soma kifungu hicho kwenye Biblia utaelewa, hapa siwezi kukiandika maana ni kirefu mno.) Kuhusu talaka imeandikwa hivi, "Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake,(yaani asipopendezwa na huyo mwanamke) kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha,(talaka), akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake , ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, MUNGU wako, iwe urithi." Kumbukumbu La Torati 24:1 mpaka 4u Hivyo basi ndugu yangu kwa kifungu hicho utaona kwamba, mwanaume alipewa ruhusa kumwacha mkewe wa ndoa, pale alipojisikia kufanya hivyo.
Lakini, baada ya Yesu Kristo kuja duniani, aliulizwa swali kuhusu hili jambo la talaka, na Bwana Yesu, bila kuficha kitu, alilitolea jambo hili ufafanuzi zaidi. Ukisoma katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11, imeandikwa hivi; "Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba, mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha MUNGU, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa."
Hapa sasa utaona wazi kabisa Biblia haijakataza kumwacha mke, unaruhusiwa kumpatia mkeo hati ya talaka kama tu amefanya uasherati, yaani amefanya mapenzi nje ya ndoa yenu. Kwa mujibu wa maneno ya Bwana Yesu, huna ruhusa kumpatia mkeo talaka kama amefanya makosa mengine ambayo sio uasherati. Kama unaushahidi ya kuwa mkeo amefanya uasherati, basi, ruksa kumapatia hati ya talaka na kuoa mke mwingine. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitafsri kifungu hichi kimakosa kabisa. Kuna watu wanasema eti ukisha muacha mkeo huna ruhusa ya kuoa mke mwingine. Hilo sio kweli hata kidogo. Kama umesoma vizuri kifungi hicho, (Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11) utaona ya kwamba, kama umemuacha mkeo kwa sababu zako zingine, basi huna ruhusa kuoa mke mwingine, na yeye mkeo uliyemuacha, pia, hana ruhusa ya kuolewa na mtu mwingine, sababu kwa kufanya hivyo wote mtakuwa mnazini. Lakini, ikiwa mkeo ni muasherati, basi unayo ruhusa kumwacha na kuoa mke mwingine.
Hakika jambo la ndoa ni gumu sana, ndio maana hata wanafunzi wa Yesu waliposikia majibu yake, walisema kama mambo ya mke na mume yako hivyo, basi ni bora kukaa bila kuoa. Ni kweli kabisa, mambo ya mke na mume ni magumu sana kwani unaweza ukaoa leo mke ukiwa unampenda kabisa, lakini baada ya muda fulani kupita, ukajikuta hutamani hata kumuona, achalia mbali kulala naye kitanda kimoja! Hapo sasa huna ruhusa ya kumuacha kama hajafanya uasherati. Inawezekana kabisa mwanamke akawa kero katika matendo mengine, lakini kama hafanyi uasherati, ndugu yangu huo ni mzigo wako, inabidi uvumilie tu, hakuna jinsi nyingine. Ndio maana Bwana Yesu alisema pia kuwa jambo la kukaa bila kuoa, sio kila mtu anayeweza kukaa bila kuoa bali wale tu waliojaliwa. Yapo maandiko mengi sana yanayozungumzia jambo hili la ndoa. Nikisema niyaandike yote, hakika sitaweza kumaliza kuandika. Lakini naamini kwa vifungu hivyo nitakuwa nimeweza kujibu swali lako la msingi.
Hitimisho la haya yote ni kwamba Biblia haijakataza kumuacha mke wa ndoa. Biblia imetoa ruhusa kumuacha mke pale tu inapodhihirika ya kuwa mke husika ni muasherati. Kama mkeo ni muasherati, basi unaruhusiwa kabisa kwa mujibu wa Biblia kumpatia hati ya talaka. Nakutakia kila la kheri katika ndoa yako ndugu yangu.
Ukiwa na nafasi unaweza ukajisomea vifungu vifuatavyo kutoka kwenye Biblia;
1 Wakorintho 7:1 mpaka 40.
1 Wakorintho 13:1 mpaka 13.
Waefeso 5:22 mpaka 33.
Wakolosai 3:18 mpaka 21.
Marko Mtakatifu 10:1 mpaka 12.
Hizi mambo ndo huwafanya watu wajiue, imani, watu watanionaje, nitawaambiaje, nk vimekuwa vikiwatesa watu ile hari maumivu ya moyo unayapata wewe. Kama mtu unaona unateseka na hizo ndoa, just move out and anza kitu kipya even new faith km unaona hiyo inakuumiza.
 
Mimi sidhan kama dhambi ni kuachana tu, hivi ukilazimisha kuishi naye alafu mwisho wa siku ukawa unamuombea kifo ili iwe rahisi kupata sababu ya kondokana na hiyo adha si ndo dhambi zaidi. Ni bora tu kama unaona moyo wako unateseka, unakosa amani, furaha na mambo yako hayaendi. Bora uachane na hiyo ndoa bila kujali ishu za imani zinasemaje, sijui watu watanionaje sijui nini na nini..... Ila angalia tu sheria za ustawi wa jamii though nao wataangalia msimamo wako. Maisha ni mafupi sana, kama huyafurahii na chance yako ya kuishi ni ndogo sana, Fanya maamuzi kabla tatizo halijawa kubwa.
 
samahani
Biblia inakataza kuachana isipokuwa kwa dhambi ya uzinzi
Mkeo/mume akizini nje ya ndoa na ikathibitika hapo biblia inaruhusu kuachana
dada, kikawaida inatakiwa tuthibitishe vipi? ni nani anatakiwa athibitishe? nataka tu kujifunza
 
samahani

dada, kikawaida inatakiwa tuthibitishe vipi? ni nani anatakiwa athibitishe? nataka tu kujifunza

Uwakute live na uwepo na shahidi mmoja pamoja naye ambaye ataenda thibitisha kwa kuhani/padri/mchungaji
Ila technolojia ya sahivi naona rahisi video una chukua tu
 
Ili ndoa iwe ndoa lazima itimize vigezo..

Kigezo kikuu ni upendo wa mke na mume.

Kupigana ngumi kila siku na suluhu hamna hiyo sio ndoa..

Kuishi bila mawasiliano yyt hata salamu tu hakuna hiyo sio ndoa

Mmoja wenu kutojali familia hiyo sio ndoa.

Kutokubaliana kwa jambo lolote lile mnalopanga kama wanandoa hiyo sio ndoa

Kupigana mangumi kila mara mpaka kutiana vilema hamna ndoa hapo.

NDOA SI GEREZA. Watu wanatafsir maandiko vibaya.

Kama Mungu tu hakulazimishi kuabudu, sembuse swala ndoa.?

Kumbuka pamoja na mitume kuwa inspired na roho mtakatifu (kwa mujibu wa biblia) kuandika maandiko ya biblia Lakin pia target yao kibinadamu ilikuwa kufikisha ujumbe kwa jamii wanazoishi ndani yake na zinazowazunguka. Wasingeongelea jamii ambazo zingekuwepo karne ya 21.

Na ndo maana kuna mambo mengi yapo kwenye maandiko yameamriwa yafanywe leo hii wengi hawayafuati kwa sababu hayakidhi tamaduni tulizonazo leo na hayana madhara ya kiroho hata kidogo kama hukuyafuata.

Maandiko ni kiongozi lakini ROHO MTAKATIFU ni kiongozi mkuu.

Mungu alimuumbia mwanadamu utashi na akili kwa sababu alijua kuna mambo atahitajika atumie utashi na akili ili aishi vizuri.

Ukipigwa ngumi na mmeo kila siku mpaka unavunjika taya au unapewa stress na mkeo mpaka unapata kiharusi eti kisa "biblia imesema tusiachane", huo utakuwa ni upumbavu wako na utakufa kwa sababu ya upumbavu wako na Mungu hatolaumiwa kwa upumbavu wako.

NDOA SI GEREZA.

Mungu hakuruhusu ndoa ije kuwa mzigo mzito kwa mwanadamu.

Kuweni wapole kama hua na wajanja kama nyoka (kwa mujibu wa biblia)
 
this is very controversial, kuna maeneo mengine Bible inasema kuwa, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe, pia Mungu anachukia kuachana. lakini pia maeneo mengine yanasema kuwa, ukimwacha mme au mke usioe tena, ukiacha ukaoa tena utakuwa unazini. hivyo kuachana ruksa lakini hakikisha kuwa hautaoa tena, hautafanya mapenzi tena yaani utakuwa padri milele. however, this is subject to more research. soma kitabu hiki pengine kitakusaidia uielewa ndoa ili msiachane.
View attachment 98211
View attachment 98211
View attachment 98212View attachment 98212View attachment 98212View attachment 98212
" Alichokiunganisha Mungu" Kuna ndoa nyingi sana ambazo hazikuunganishwa na Mungu, mfano demu mmekutana baa kwenye ulabu ukiwa umelewa chakari ukamchukua kwako ukagonga mipango kumbe mimba ilikuwa inasubiri mlangoni kushika mara unaamisha bibi ndani mnaendelea kuishi baada ya miaka kadhaa mkaacha dhambi na kuamua kuingia kwenye ukristo kindakindaki, Swali je mke huyo ni halali kwako? Je mmeunganishwa na Mungu? Je ukimuacha ni dhambi?
 
Biblia Inakuitaji utoe talaka KWA DHAMBI YA UZINZI TUUU.
Bibilia inasema " Mke mwema hutoka kwa Bwana" Je wake wasio wema hutoka wapi? Je ni haki kuendelea kuishi na mke asie mwema na asitoka kwa bwana?
"Alicho kiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe" je Mungu anaweza kukuunganisha na mke asie mwema?
Kama mke sio mwema inamaana hajatoka kwa Mungu na pia inamaana hamjaunganishwa na Mungu?

Sifa pekee za mke mwema & mambo muhimu ya kuzingatia utafutapo mtu wa kuishi naye
 
fourtypercent, jaribu kuwaona viongozi wako wa dini hususan wa dhehebu lako wanaweza kukusaidia zaidi. Hizi imani ziko tofauti na hapa waweza kupewa majibu tofauti tofauti na tena ya kukuchanganya kulingana na imani ya kila mwana JF MMU au pengine unaweza usijibiwe kabisa!
hujatoa majibu coz na wengine tulitaka tujuwe so toa majibu kama alivyouliza kama hujuwi pia sema tu
 
Ili ndoa iwe ndoa lazima itimize vigezo..

Kigezo kikuu ni upendo wa mke na mume.

Kupigana ngumi kila siku na suluhu hamna hiyo sio ndoa..

Kuishi bila mawasiliano yyt hata salamu tu hakuna hiyo sio ndoa

Mmoja wenu kutojali familia hiyo sio ndoa.

Kutokubaliana kwa jambo lolote lile mnalopanga kama wanandoa hiyo sio ndoa

Kupigana mangumi kila mara mpaka kutiana vilema hamna ndoa hapo.

NDOA SI GEREZA. Watu wanatafsir maandiko vibaya.

Kama Mungu tu hakulazimishi kuabudu, sembuse swala ndoa.?

Kumbuka pamoja na mitume kuwa inspired na roho mtakatifu (kwa mujibu wa biblia) kuandika maandiko ya biblia Lakin pia target yao kibinadamu ilikuwa kufikisha ujumbe kwa jamii wanazoishi ndani yake na zinazowazunguka. Wasingeongelea jamii ambazo zingekuwepo karne ya 21.

Na ndo maana kuna mambo mengi yapo kwenye maandiko yameamriwa yafanywe leo hii wengi hawayafuati kwa sababu hayakidhi tamaduni tulizonazo leo na hayana madhara ya kiroho hata kidogo kama hukuyafuata.

Maandiko ni kiongozi lakini ROHO MTAKATIFU ni kiongozi mkuu.

Mungu alimuumbia mwanadamu utashi na akili kwa sababu alijua kuna mambo atahitajika atumie utashi na akili ili aishi vizuri.

Ukipigwa ngumi na mmeo kila siku mpaka unavunjika taya au unapewa stress na mkeo mpaka unapata kiharusi eti kisa "biblia imesema tusiachane", huo utakuwa ni upumbavu wako na utakufa kwa sababu ya upumbavu wako na Mungu hatolaumiwa kwa upumbavu wako.

NDOA SI GEREZA.

Mungu hakuruhusu ndoa ije kuwa mzigo mzito kwa mwanadamu.

Kuweni wapole kama hua na wajanja kama nyoka (kwa mujibu wa biblia)
Kama nimekuelewa vilivyo, unamaanisha kuna mambo zaidi ya uesherati ambayo yanafaa kabisa kuwa sababu ya watu kuachana,right?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom