Kuachana na mke wa ndoa (christian) ni kweli biblia imezuia?

fourtypercent

Member
Jun 4, 2011
53
20
Kwa muelewa wa maandiko matakatifu(biblia) anijuze, je, ni kweli biblia imezuia waliofunga ndoa kanisani wasiachane?, kama inawezekana anipe na reference za maandiko. ahsanteni.....
 
Kwa muelewa wa maandiko matakatifu(biblia) anijuze, je, ni kweli biblia imezuia waliofunga ndoa kanisani wasiachane?, kama inawezekana anipe na reference za maandiko. ahsanteni.....
fourtypercent, jaribu kuwaona viongozi wako wa dini hususan wa dhehebu lako wanaweza kukusaidia zaidi. Hizi imani ziko tofauti na hapa waweza kupewa majibu tofauti tofauti na tena ya kukuchanganya kulingana na imani ya kila mwana JF MMU au pengine unaweza usijibiwe kabisa!
 
Kwani viongozi wako wa dini hauwaamini wanachokufundisha? Kama hauwaamini ni nani mwingine utamuamini?. NB: Utakapo enda kupewa mafundisho na viongozi wako usiende ukiwa tayari na majibu au interests zako kichwani! Kwa mfano mimi ni mu islamu,baada ya kuona nyama ya nguruwe huwa imenona muda wote na watu wengi huwa wanaila,naweza kwenda kwa sheikh wangu na kuanza kumsumbua kwamba ni wapi aya kwenye quran inayokataza kula kitimoto! Thats insane!.
 
this is very controversial, kuna maeneo mengine Bible inasema kuwa, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe, pia Mungu anachukia kuachana. lakini pia maeneo mengine yanasema kuwa, ukimwacha mme au mke usioe tena, ukiacha ukaoa tena utakuwa unazini. hivyo kuachana ruksa lakini hakikisha kuwa hautaoa tena, hautafanya mapenzi tena yaani utakuwa padri milele. however, this is subject to more research. soma kitabu hiki pengine kitakusaidia uielewa ndoa ili msiachane.
View attachment 98211
View attachment 98211
View attachment 98212View attachment 98212View attachment 98212View attachment 98212
 
ukipatia kuoa utasema nilikuwa nimekawilia wapi na ukikosea kuoa utaikumbuka mithari ya Suleimani inayosema,nibora kukaa pembe ya dari kuliko kukaa ktk chumba kipana na mwanamke mchokozi, ni PM kwa msaada zaidi
 
Ndugu yangu mimi nimeisoma Biblia na kiasi nafahamu maandiko yanavyosema. Swala la kuoa au kuolewa sio jambo la mchezo hata kidogo. Kwetu sisi wanaume, unaweza ukaoa mwanamke halafu ukajuta sana baadae.

Katika swala la ndoa Biblia imetupendelea sana wanaume kwa sababu, kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume ndio aliumbwa wa kwanza na BWANA MUNGU.

Hivyo basi, mwanaume ndio kichwa katika familia; kwa maana nyingine, mwanaume ndio mkuu au mtawala katika ndoa. Ukisoma Mwanzo 3:16 "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." Hapa utaona wazi kabisa BWANA MUNGU alisema mke, atatawaliwa na mumewe.

Sasa baada ya utangulizi huo turudi kwenye hoja yako ya kwamba, je, kumuacha mke wa ndoa (christian) ni kweli Biblia imezuia? Mimi binafsi naweza kukujibu ya kuwa Biblia haijazuia kumuacha mkeo wa ndoa. Biblia imefafanua kwa uwazi kabisa sababu zinazokubalika kumuacha mkeo wa ndoa. Kabla Yesu hajazaliwa duniani, wana wa Israeli walipewa sheria na BWANA MUNGU kupitia kwa Musa. Sheria hii ilikuwa inawaelezekeza wana wa Israeli namna ya kuishi na mambo yote yakiwamo pia mambo ya ndoa.

Ukisoma katika Kumbukumbu La Torati 22:13 mpaka 21, utaona kwamba mwanaume alipewa ruhusa kumuacha mkewe kama siku ya ndoa hakumkuta na bikira. Tena sio kumuacha tu, bali mwanamke huyu adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa.(Soma kifungu hicho kwenye Biblia utaelewa, hapa siwezi kukiandika maana ni kirefu mno.)

Kuhusu talaka imeandikwa hivi, "Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake,(yaani asipopendezwa na huyo mwanamke) kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha,(talaka), akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake , ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, MUNGU wako, iwe urithi." Kumbukumbu La Torati 24:1 mpaka 4u

Hivyo basi ndugu yangu kwa kifungu hicho utaona kwamba, mwanaume alipewa ruhusa kumwacha mkewe wa ndoa, pale alipojisikia kufanya hivyo. Lakini, baada ya Yesu Kristo kuja duniani, aliulizwa swali kuhusu hili jambo la talaka, na Bwana Yesu, bila kuficha kitu, alilitolea jambo hili ufafanuzi zaidi.

Ukisoma katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11, imeandikwa hivi; "Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba, mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha MUNGU, mwanadamu asiwatenganishe.

Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa."

Hapa sasa utaona wazi kabisa Biblia haijakataza kumwacha mke, unaruhusiwa kumpatia mkeo hati ya talaka kama tu amefanya uasherati, yaani amefanya mapenzi nje ya ndoa yenu. Kwa mujibu wa maneno ya Bwana Yesu, huna ruhusa kumpatia mkeo talaka kama amefanya makosa mengine ambayo sio uasherati. Kama una ushahidi ya kuwa mkeo amefanya uasherati, basi, ruksa kumpatia hati ya talaka na kuoa mke mwingine.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitafsri kifungu hichi kimakosa kabisa. Kuna watu wanasema eti ukishamuacha mkeo huna ruhusa ya kuoa mke mwingine. Hilo sio kweli hata kidogo. Kama umesoma vizuri kifungi hicho, (Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11) utaona ya kwamba, kama umemuacha mkeo kwa sababu zako zingine, basi huna ruhusa kuoa mke mwingine, na yeye mkeo uliyemuacha, pia, hana ruhusa ya kuolewa na mtu mwingine, sababu kwa kufanya hivyo wote mtakuwa mnazini. Lakini, ikiwa mkeo ni muasherati, basi unayo ruhusa kumwacha na kuoa mke mwingine.

Hakika jambo la ndoa ni gumu sana, ndio maana hata wanafunzi wa Yesu waliposikia majibu yake, walisema kama mambo ya mke na mume yako hivyo, basi ni bora kukaa bila kuoa. Ni kweli kabisa, mambo ya mke na mume ni magumu sana kwani unaweza ukaoa leo mke ukiwa unampenda kabisa, lakini baada ya muda fulani kupita, ukajikuta hutamani hata kumuona, achalia mbali kulala naye kitanda kimoja! Hapo sasa huna ruhusa ya kumuacha kama hajafanya uasherati.

Inawezekana kabisa mwanamke akawa kero katika matendo mengine, lakini kama hafanyi uasherati, ndugu yangu huo ni mzigo wako, inabidi uvumilie tu, hakuna jinsi nyingine. Ndio maana Bwana Yesu alisema pia kuwa jambo la kukaa bila kuoa, sio kila mtu anayeweza kukaa bila kuoa bali wale tu waliojaliwa. Yapo maandiko mengi sana yanayozungumzia jambo hili la ndoa. Nikisema niyaandike yote, hakika sitaweza kumaliza kuandika. Lakini naamini kwa vifungu hivyo nitakuwa nimeweza kujibu swali lako la msingi.

Hitimisho la haya yote ni kwamba Biblia haijakataza kumuacha mke wa ndoa. Biblia imetoa ruhusa kumuacha mke pale tu inapodhihirika ya kuwa mke husika ni muasherati. Kama mkeo ni muasherati, basi unaruhusiwa kabisa kwa mujibu wa Biblia kumpatia hati ya talaka.

Nakutakia kila la kheri katika ndoa yako ndugu yangu. Ukiwa na nafasi unaweza ukajisomea vifungu vifuatavyo kutoka kwenye Biblia;
1 Wakorintho 7:1 mpaka 40.
1 Wakorintho 13:1 mpaka 13.
Waefeso 5:22 mpaka 33.
Wakolosai 3:18 mpaka 21.
Marko Mtakatifu 10:1 mpaka 12.
 
Ndugu yangu mimi nimeisoma Biblia na kiasi nafahamu maandiko yanavyosema. Swala la kuoa au kuolewa sio jambo la mchezo hata kidogo. Kwetu sisi wanaume, unaweza ukaoa mwanamke halafu ukajuta sana baadae. Katika swala la ndoa Biblia imetupendelea sana wanaume kwa sababu, kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume ndio aliumbwa wa kwanza na BWANA MUNGU. Hivyo basi, mwanaume ndio kichwa katika familia; kwa maana nyingine, mwanaume ndio mkuu au mtawala katika ndoa. Ukisoma Mwanzo 3:16 "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." Hapa utaona wazi kabisa BWANA MUNGU alisema mke, atatawaliwa na mumewe.
Sasa baada ya utangulizi huo turudi kwenye hoja yako ya kwamba, je, kumuacha mke wa ndoa (christian) ni kweli Biblia imezuia? Mimi binafsi naweza kukujibu ya kuwa Biblia haijazuia kumuacha mkeo wa ndoa. Biblia imefafanua kwa uwazi kabisa sababu zinazokubalika kumuacha mkeo wa ndoa. Kabla Yesu hajazaliwa duniani, wana wa Israeli walipewa sheria na BWANA MUNGU kupitia kwa Musa. Sheria hii ilikuwa inawaelezekeza wana wa Israeli namna ya kuishi na mambo yote yakiwamo pia mambo ya ndoa. Ukisoma katika Kumbukumbu La Torati 22:13 mpaka 21, utaona kwamba mwanaume alipewa ruhusa kumuacha mkewe kama siku ya ndoa hakumkuta na bikira. Tena sio kumuacha tu, bali mwanamke huyu adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa.(Soma kifungu hicho kwenye Biblia utaelewa, hapa siwezi kukiandika maana ni kirefu mno.) Kuhusu talaka imeandikwa hivi, "Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake,(yaani asipopendezwa na huyo mwanamke) kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha,(talaka), akamtilie mkononi mwake na kumtoa katika nyumba yake. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake , ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine. Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe; yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za BWANA; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo BWANA, MUNGU wako, iwe urithi." Kumbukumbu La Torati 24:1 mpaka 4u Hivyo basi ndugu yangu kwa kifungu hicho utaona kwamba, mwanaume alipewa ruhusa kumwacha mkewe wa ndoa, pale alipojisikia kufanya hivyo.
Lakini, baada ya Yesu Kristo kuja duniani, aliulizwa swali kuhusu hili jambo la talaka, na Bwana Yesu, bila kuficha kitu, alilitolea jambo hili ufafanuzi zaidi. Ukisoma katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11, imeandikwa hivi; "Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba, mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha MUNGU, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa."
Hapa sasa utaona wazi kabisa Biblia haijakataza kumwacha mke, unaruhusiwa kumpatia mkeo hati ya talaka kama tu amefanya uasherati, yaani amefanya mapenzi nje ya ndoa yenu. Kwa mujibu wa maneno ya Bwana Yesu, huna ruhusa kumpatia mkeo talaka kama amefanya makosa mengine ambayo sio uasherati. Kama unaushahidi ya kuwa mkeo amefanya uasherati, basi, ruksa kumapatia hati ya talaka na kuoa mke mwingine. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitafsri kifungu hichi kimakosa kabisa. Kuna watu wanasema eti ukisha muacha mkeo huna ruhusa ya kuoa mke mwingine. Hilo sio kweli hata kidogo. Kama umesoma vizuri kifungi hicho, (Mathayo Mtakatifu 19:3 mpaka 11) utaona ya kwamba, kama umemuacha mkeo kwa sababu zako zingine, basi huna ruhusa kuoa mke mwingine, na yeye mkeo uliyemuacha, pia, hana ruhusa ya kuolewa na mtu mwingine, sababu kwa kufanya hivyo wote mtakuwa mnazini. Lakini, ikiwa mkeo ni muasherati, basi unayo ruhusa kumwacha na kuoa mke mwingine.
Hakika jambo la ndoa ni gumu sana, ndio maana hata wanafunzi wa Yesu waliposikia majibu yake, walisema kama mambo ya mke na mume yako hivyo, basi ni bora kukaa bila kuoa. Ni kweli kabisa, mambo ya mke na mume ni magumu sana kwani unaweza ukaoa leo mke ukiwa unampenda kabisa, lakini baada ya muda fulani kupita, ukajikuta hutamani hata kumuona, achalia mbali kulala naye kitanda kimoja! Hapo sasa huna ruhusa ya kumuacha kama hajafanya uasherati. Inawezekana kabisa mwanamke akawa kero katika matendo mengine, lakini kama hafanyi uasherati, ndugu yangu huo ni mzigo wako, inabidi uvumilie tu, hakuna jinsi nyingine. Ndio maana Bwana Yesu alisema pia kuwa jambo la kukaa bila kuoa, sio kila mtu anayeweza kukaa bila kuoa bali wale tu waliojaliwa. Yapo maandiko mengi sana yanayozungumzia jambo hili la ndoa. Nikisema niyaandike yote, hakika sitaweza kumaliza kuandika. Lakini naamini kwa vifungu hivyo nitakuwa nimeweza kujibu swali lako la msingi.
Hitimisho la haya yote ni kwamba Biblia haijakataza kumuacha mke wa ndoa. Biblia imetoa ruhusa kumuacha mke pale tu inapodhihirika ya kuwa mke husika ni muasherati. Kama mkeo ni muasherati, basi unaruhusiwa kabisa kwa mujibu wa Biblia kumpatia hati ya talaka. Nakutakia kila la kheri katika ndoa yako ndugu yangu.
Ukiwa na nafasi unaweza ukajisomea vifungu vifuatavyo kutoka kwenye Biblia;
1 Wakorintho 7:1 mpaka 40.
1 Wakorintho 13:1 mpaka 13.
Waefeso 5:22 mpaka 33.
Wakolosai 3:18 mpaka 21.
Marko Mtakatifu 10:1 mpaka 12.

Heshima yako Mkuu.. Chinekee, kumbe we have Pastors here.. Ntakupm kwa ushauri wa kiroho.. Ukinikubalia unijibu pls pls.. Am serious..
 
Heshima na wewe mkuu....Lakini kwanini unipime? au na wewe ni Mfarisayo? Kama unao ushauri wa kiroho mimi sioni kwanini nikatae kujadili. Nakukaribisha tujadili hoja ndugu yangu.
 
Asante sana sana......... na je mwanamke akimuacha mumewe kwa uasherati? je aweza kuolewa? au niulize kiupana zaidi, kuna sehemu yeyote ya bible imeruhusu mwanamke kumuacha mumewe?
 
Asante sana sana......... na je mwanamke akimuacha mumewe kwa uasherati? je aweza kuolewa? au niulize kiupana zaidi, kuna sehemu yeyote ya bible imeruhusu mwanamke kumuacha mumewe?
Ukisoma vizuri kwenye Biblia utaona kuwa jambo la mwanamke kumuacha mumewe halijazungumziwa. Lakini kwa kutumia busara, kama mume ni muasherati, basi mke anayohaki ya kudai talaka kutoka kwa mumewe. Tukumbuke kuwa anayetoa talaka kwa mujibu wa Biblia ni mume. Bwana Yesu alifafanua wazi kabisa kuwa ni uasherati tu pekee utakowezesha ndoa kuvunjika. Hivyo, basi kama mume ni muasherati, mke anayoruhusu kudai talaka na kuachana naye na akaolewa na mtu mwingine. Lakini, Kwa Wakristo, msamaha na kusameheana vimesisitizwa katika Biblia, soma Mathayo Mtakatifu 6:14,15. Pia waweza soma Mathayo Mtakatifu 7:1,2. Kama mume amekukosea au mke amekukosea kwa kufanya uasherati, ukiwa kama Mkristo unaweza kumsamehe mwenza wako wa ndoa. Ndoa ni sehemu moja kubwa sana ya upendo. Basi kama upendo wa kweli upo tafakari maneno haya, "Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu nuingue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo, huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; upendo hauhesabu mabaya; upendo haufurahii udhalimu; bali hufurahi pamoja na kweli; upendo huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; upendo hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote;" Soma 1Wakorintho 13:1 mpaka 8.
 
Back
Top Bottom