KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

Upo vizuri sana mkuu.. naoenda unavyo leta fact.
 
Nimekusoma kaka, lakini hebu tuangalie pale Mamlaka yetu hii ingejikita katika maboresho ya utendaji na kuachana na siasa..

Maono yangu mimi, kuna kuna sababu ndogo ndogo na huwa kuna sababu mzizi, ambao ukifanikiwa kuujua ukaung'oa basi ule mti wa tatizo utanyauka.

TRA wanajitahidi, lakini tunaangushwa na viongozi wetu.

KUMBUKA: Hao TRA kwa sasa wanacheza kulingana na mdundo wa wakuu wa serikali na sio kulingana na maelekezo ya taaluma zao au mahitaji ya soko.

TRA itengwe na siasa, ipewe nguvu ya kukemea pale inapoingiliwa na wanasiasa.
 
Well said..
 
Mkuu Mr zero brain naomba nikukunbushe bapa sio facebook
 
Hakuna anaependa kulipa kodi hata ingekua ndogo kiasi gani!! Hapa agenda kuu ni kwnn KRA wanakusanya zaidi ya TRA,Hata izo fedha zilizokusanywa hazijatolewa kwa dhati ni kwasababu ya sheria kanuni na taratibu za nchi.
Kwasababu Kenya uchumi wao ni mkubwa, kumbuka kodi inatozwa kutokana na % ya mapato ya nchi, mapato yakiwa makubwa hiyo % inakua ni pesa nyingi.

Muhimu ni kulinganisha ufanisi kati ya TRA na KRA, sio kiwango cha jumla ya fedha kilichokusanywa, hilo ni kosa.

Tujiulize KRA inakusanya % ngapi ya GDP ya Kenya, na TRA inakusanya % ngapi ya GDP ya Tanzania?
 
Nasema kila siku, TRA ni adui wa wafanya biashara.

Wafanyabiashara ni adui wa TRA.

Wakati wenzetu wanaona sifa kulipa kodi, sisi tunaona sifa kukwepa kodi.

Chanzo cha yote haya ni SIASA kuingizwa kwenye UKUSANYAJI na MATUMIZI YA MAPATO.
 
Asielewa kati yangu na yako ni nani sasa? Government domestic revenue unaita grants? We si takataka kabisa

Sasa mtu asiyeelewa domestic revenue na Grants unabishana nae nini si unapoteza muda wako
 
Nasema kila siku, TRA ni adui wa wafanya biashara.

Wafanyabiashara ni adui wa TRA.

Wakati wenzetu wanaona sifa kulipa kodi, sisi tunaona sifa kukwepa kodi.

Chanzo cha yote haya ni SIASA kuingizwa kwenye UKUSANYAJI na MATUMIZI YA MAPATO.
Siasa imeingizwaje kwenye mfumo wa kikodi?
 
Upo sahihi lakini hata hicho kiwango TRA inakusanya .. unakusanya kutoka base ndogo sana kwa sababu unatoza kodi kubwa.

Mfano

KRA: Capital Gain Tax ni 5%
TRA : Capital Gain Tax ni 10%

Ndio maana tunasema makusanyo ya TRA yamebeba risk kwa sababu yapo kisiasa.

Kama TRA watatoza kodi sahihi kwa wafanya biashara maana yake hatuwezi kufikia hata kiwango cha sasa hadi watakapo kuza base ya walipa kodi na kufikia walau 80% ya wanao stahili kulipa kodi.

Kuna maeneo mengi sana ambayo hayaja guswa na kama yakiguswa TRA inaweza kuwa na nafasi kubwa sana katika maendeleo ya nchi hii.
 
We unadhani hawalijui hili wanajua sana ila wamejawa na tamaa tu, kupenda kuwanyonya walipa kodi.

TRA amkeni amkeniiiiii
 
Kaka katika kitu kinachomuumiza kichwa Magufuli ni TRA na Wizara ya mambo ya ndani na BoT, wewe mwenyewe umemsikia mara kadhaa Magufuli akichanganyikiwa kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa TRA, katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 5. amebadilisha makamishina wakuu 5, wastani wa kamishna mkuu mmoja kila mwaka
, hii ni dalili kwamba hakuna utendaji mzuri TRA.

Kaka tatizo la TRA lipo kwa wetendaji kuwa na uwezo mdogo, kukosa ubunifu na kutokuwepo na uongozi imara, bado wafanyakazi wengi wa TRA ni mangi meza, sidhani Kama kuna siasa.
 
Shida kubwa ya TRA ni kwamba sio taasisi huru ambayo inajiendesha yenyewe bila kuingiliwa na wanasiasa . Nafasi ya bosi wa TRA ilifaa iwe inatangazwa watu wanaomba kuajiriwa kwa mkataba wa muda fulani huku wakija na mbinu za kuiboresha hii taasisi ili iende na waakati. Pale ambapo TRA inacheza mziki wa wanasiasa iwe Rais,Waziri, RC, DC au mbunge basi hiyo taasisi haiwezi kujiendesha kwa weledi.

Tutalia na kupiga kelele lakini wanasiasa (viongozi) Hawaii tayari kuichia TRA ijiendeshe yenyewe kwa sababu inatumika kama fimbo kuwachapia wasiowapenda,kupata cheap political milage nk. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi mirahaba na kodi za madini hukusanywa na TRA au huenda directly Hazina? maana hili gap la kuzidishwa mara tatu ni kubwa!
 
Kumbe JPM kwa miaka 5 ameongeza 4% kutoka pale tulipo achwa na JK, pamoja namajigambo bado makusanyo ya TRA yako chini yakiwango, kazi nimoja kwa CCM tenganisha siasa na uchumi wa nchi ndomtaweza kuona performance ya sector ya fedha
 
2019-2020
Zimejumuisha maduuli yote ya serikali kutoka maeneo kama national parks, wizara ya kilimo, wizara ya nishati na agencies nyingine za serikali ambayo mifumo yake kikodi haiintercept na TRA?

Ya Kenya ulioweka hapo ukasema imetuzidi mara 3 imejumuisha hayo yote, sasa na kuuliza na ya Tanzania imejumuisha? 🚮🚮🚮🚮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…