Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Haya maandamano ni ya CDM kutaka kutuvurugia amani yetu ya Tz na si lingile lolote !
drunk-people-3-400x282.jpg
 
Kamanda Kova tunashindwa kuelewa kama kweli umezui maandamano kwa sababu ya tishio la vitendo vya kigaidi,
Hebu tujiulize jamani, hivi yale maandamano yasiyo rasmi ya pale barabara ya kongo kariakoo na haya ambayo yangefanyika leo yapi yanaweza kuwa na idadi kubwa ya raia?na je jumamosi mechi ya mpira kati ya simba na yanga itazuiliwa?
Nasikitika kwamba viongozi wetu wakati mwingine wanafanya maamuzi yatakayozua malalamiko bila sababu za msingi.
Ninawakumbusha kuwa wananchi wa nchi hii sasa hivi wengi ni waelewa wa mambo, hivyo wanapoenda kwenye public kusema kitu wawe wametafakari kwa makini nini wanachoenda kusema.
 
Mnajaribu kupinga kisichopingika, Dowans lazma ilipwe.
Acha ujinga we mzee!,kabla hawajalipwa waseme kwanza DOWANS ni nani.Samahnai kama kuna wanaojuwa,mimi sijui dowans ni nani.
 
Yaani Tanzania ni nchi ya kipekee kabisa. Mambo ya msingi yanazuiwa, yale yasiyo na msingi ndio mpeto kwenda mbele. Kwani hao Dowans si hao watanzania wenzetu? Alshabab hapa hawana uhusiano kabisa, aliogopa kurudia lile neno la sababu za ki intelijensia!
 
Ahaa jamani; kova anamtindio wa ubongo au mnajifanya hamjui? Huwa anaingia stoo ya silaha anachukua ma ak 47, marisasi anaita waandishi akidai wamekata majambazi,kumbe huwa geresha ili viongozi wamuone anafanya kazi, kova fixiii aibu!
 
Haya maandamano ni ya CDM kutaka kutuvurugia amani yetu ya Tz na si lingile lolote !

Kwa lugha kama hizi za kipuuzi inaonyesha wazi watanganyika tuna safari ndefu ya kujikomboa kifikra. Huyu hayuko peke yake wako wengi wenye mawazo pumba kama yeye. Mungu tuhurumie taifa hili
 
Maamuzi kama haya ndio chanzo ya viongozi kuzomewa hata na watoto wadogo mitaani.
 
Mnajaribu kupinga kisichopingika, Dowans lazma ilipwe.

Wewe kweli siyo JF material!!! Yaani unachangia bila hata kufikiria!!!!!

Kama wanapinga kisichopingika, na Downs lazima ilipwe, sasa serilkali imekata rufaa ya nini??? Kwa mchango wako najua hilo ni swali gumu sana kwako!! Nenda kawaconsult akina MS, GB, FF......!!!
 
Wakati mwingine nashikwa hasira sana mpaka natamani kutukana. Kwahiyo Nape akiamua kufanya mkutano leo atanyimwa? Au mnaogopa hayo maandamano yataunganisha na kumtoa Rais?

Nataman sana hiyo route ya maandamano ingekuwa Arusha, walaah Kova ungekuja hata wewe lakini watu wangeandamana na ukizingua ungeumia vile vile. Muda wa kuwabembeleza umeisha.

Leo mahakama Arusha mmezuia watu wasiingie, amri ya mahakama ya kufunga spika njee mmepuuza. Mnawataka nini wadanganyika?

Siku zenu si nyingi, Kova nakushauri anza kutafuta exile.
 
Kuna uhusiano gani wa kulipwa doainzi na Al Shabaab?!! Ifike muda watawawala wetu wawe wanafikiri kwa kutumia bongo zao badala ya kuendelea kutumia nyayo zao kufikiri!!!!! Shwine kabisa

Labda Dowan ni kampuni ya Alshabaab
 
hata mechi ya Simba na Yanga ni mkusanyiko kwahiyo nayo haina budi kuchezwa kesho, au ichezwe bila mashabiki
 
Kwa hiyo ni mpaka tunapotangaza maandamano juu ya uovu wa serikali ndiyo Al-Shabaab wanaingia nchini? Kova likitokea lolote lenye picha na sura ya Al-Shabaab unalo!!!!!!
 
Si jana tu bosi wake kasema kwamba wamejidhatiti kukabiliana na Al-shabab?!
Tatizo Kova anapenda sana kucheza na jukwaa; huyu mjomba toka yuko Mbeya alikua anapenda sana kucheza na media..sasa kwa vile anajua kila mTZ ana habari ya hayo maandamano anataka apate airtime kidogo hapo..
Kwa hilo na Mechi ya Simba na Yangu ifutwe maana pale kutakuwa na zaidi ya watu 60,000:hatari:
 
Kama hii itakuwa ndio sababu ya kuzuia maandamano na wananchi tukaacha kujitokeza kwa wingi basi watawala wetu watakuwa wamefanikiwa kuifanya TZ taifa la wajinga..Ni haki yetu kuandamana kupinga ufedhuli wa mafisadi kupitia dowans. leo mnatafuta sababu za ki**nge kutuzuia? kwa hiyo mtazuia pia sehemu zote ambazo huwa zina wingi wa watu kama kariakoo kwa siku ya jumamosi pamoja na mechi ya simba na yanga?.Kwa kweli inauma sana..kama watanzania tungekuwa na sauti ya umoja na kutokuwa waoga tungejitokeza kwa wingi sana kesho,mass inapokuwa kubwa mno kamwe hawatoweza kuzuia maana wakijaribu safari ya ukombozi huenda ikaanzia hapo mpaka ****** kung'oka maana hii ya Dowans inatuhusu wote sio cuf,sio chadema,hata wengi tu ndani ya ccm yenyewe wanakili ni uhuni na ufedhuli wa mafisadi...KWA NINI TUZUIWE KIPUUZI HIVI?
 
kama kufa kupo uwezi kukwepa al-shabib mnao siku nyingi na nchi yetu inafaidika na pesa haramu ndio maana viwanja vimepanda sana , tuna dola nyingi lakini hazina manufaa, hawa wat utawajua tu wanauza maused computer, fridge maredio na makapeti polisi ndio wanawapa vibali vya kufanya kazi ni vipi hawa watu hawahui hata lugha wanafanya biashara, lakini tuyaache tu na tuwakumbatie kama rage, kinana na base wazae na dada zetu tuchanganyane ingawaje wana roho tofauti hawanaga huruma
 
Back
Top Bottom