Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,449
- 100,743
Hii ni kali ya miaka 50 ya uhuru... Al Shabaab na dowans wapi na wapi? Hawa manjagu wamepiga ramli ndio mganga akawapa huu usaniiKutokana na taarifa ya polisi, maandamano ya kupinga malipo ya Dowans hayawezi kufanyika kutokana na hofu ya Al Shabab.
Source ITV saa 2 usiku.
Nadhani kuna haja ya kuahirisha maazimisho ya miaka 50 ya uhuru, mechi ya simba na yanga na mikusanyiko mingine mingi itayojumuisha viongozi wa taifa na kimataifa kwa kuhofia Al Shabab!Intelijensia ya Jeshi letu hii. Acha nicheke miye!
Lakini kwanini intelijensia yetu inaonyesha kufanikiwa kwenye mambo ya MAANDAMANO tu, na si kwenye issu kama KILIMO KWANZA na uchumi?
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...
Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....
Hili tishio la dowans hajawahi kuliona hata kidogo?
Nadhani kuna haja ya kuahirisha maazimisho ya miaka 50 ya uhuru, mechi ya simba na yanga na mikusanyiko mingine mingi itayojumuisha viongozi wa taifa na kimataifa kwa kuhofia Al Shabab!
Kweli kabisa.Tufike mahali tuheshimu ushauri unaotolewa na vyombo vya usalama siyo kubeza kila tunachoambiwa. Yanayowapata wakenya hamyaoni?????
kwa mara ya kwanza ninakubaliana na Polisi ktk hili sababu kwa kipindi hiki ambacho hali ni tete hawa jamaa Al shabab wanaweza kutupiga ktk maandamano na kusababisha mass casualty,tukikumbuka uganda jinsi walivyoshambuliwa wakati wakiangalia world cup.Kifupi kwa kipindi hiki tujiepushe na mikusanyiko siyo ya lazima.
Tatizo hawa maitelijensia wetu wanafikiria kwa masaburi! Vitu vya muhimu kwa Taifa kwao havina umuhimu...
Kuna uhusiano gani wa kulipwa doainzi na Al Shabaab?!! Ifike muda watawawala wetu wawe wanafikiri kwa kutumia bongo zao badala ya kuendelea kutumia nyayo zao kufikiri!!!!! Shwine kabisa