Kosa kuu la tatu la UKAWA

Kosa kuu la tatu la UKAWA

Endeleni lakini watanzania siyo wajinga mnafanya maigizo mingi wanawangalia tu


Kajifunze kwanza Kiswahili ndiyo urudie Siasa, wenzako hao akina Mbowe wameshamaliza huko wewe hata Lugha haujui lkn uko hapa kupiga domo, Siasa haiweki chakula mezani, haya rudi darasani!
 
Wafunzi walio dahiliwa kwenye uongozi Wa kikwete hawana sifa basi asiwafukuze kwa stahili hiyo wadailiwe upya nawaambiwe vigezo vipi wamevikosa
 
Ndugu hata wakibaki na wakaamua hakuna lolote kujadiliwa ispokua lile wanalotaka, watatolewa na poliCCM kwa hujawahi kushuhudia?
 
CCM imepata mtelezo.Ikitaka kupitisha jambo lolote bungeni bila vikwazo vya upinzani inamuambia Tulia aongoze bunge.

CCM sasa inaweza kuamua lini wapinzani wawepo bungeni na lini wasiwepo kwa kutumia msimamo wa UKAWA dhidi ya Tulia.

Haya ni matokeo ya maamuzi ya hasira ya Mbowe. Yatagharimu UKAWA na nchi pia wakati mwingine.

Kuna makosa makuu matatu wanaUKAWA (wale wanaofikiri) tunayajutia sana.Kosa la kwanza ni kukubali Lowassa awe mgombea wetu wa urais.Kosa la pili ni kugomea uchaguzi wa Zanzibar.Na kosa la tatu ni hili la kumgomea Tulia.TUNGOJE.

No, si kweli mkuu na sikubaliani na wewe kwa 100%!

CCM ina wabunge zaidi ya 250 na UKAWA/UPINZANI ni si zaidi 120!!

Kwa tofauti hiyo ya idadi hata kama hawa wangekuwa wanahudhuria kila kikao wakati wote na CCM wakataka kupitisha jambo lolote wangeshindwaje?

Ninakubaliana na wewe ktk moja tu, kuwa sasa wanaweza kupitisha chochote pasipo upinzani mkubwa.

Hata hivyo, hii hata haina maana yoyote kwa sbb kama jambo lililopitishwa ni baya basi litabaki kuwa baya tu na litawaathiri wananchi wote na kama ni kupingwa basi litapingwa tu huku nje!!

Rejea bunge la katiba. Pamoja na kuachiwa na kuipitisha "katiba pendekezwa" kwa mbwembwe za kila dizaini, iko wapi? Je, haikugeuka kuwa kitanzi cha kwao wenyewe? Samwel Sitta yuko wapi?

Uliona ugumu wa uchaguzi wa mwaka jana?

Hii watacheka kwa muda na kudhani wamewaweza, lakini ukweli ni kuwa hiki ni kitanzi chao cha hapo badae...waingereza wanasema ita back fire!

Ni vyema sana mkashindana kwa hoja humo humo na mkawashinda kuliko kujengewa dhana ya kutoaminiwa na upande mmoja kwa sbb za upendeleo, ukiukaji wa taratibu na ubabe tu usio na kichwa wala miguu!!

Una habari kuwa ujinga huu tayari unafungamanishwa na Rais Magufuli na serikali kwa ujumla? Unajua madhara yake? Utazuia watu kutoamini haya?

Mkubwa siasa haziko bungeni tu. Uwanja wa siasa na harakati za kisiasa zina eneo pana sana. Tena huku nje ndiko siasa hasa zinakofanyika!!

Unakumbuka sakata la Buzwagi mwaka 2006/7 dhidi ya Zitto KABWE? Wakamwadhibu Zitto Kabwe kutohudhuria vikao kadhaa, wakachekelea sana na kudhani wamemuua kisiasa yeye binafsi na CHADEMA ili kuficha uchafu wa CCM na serikali yao chini ya zulia!

Matokeo yake unayakumbuka? Ili back fire kwa CCM na kuiporomosha serikali kwa kishindo kikuu na leo Zitto huyo politically stronger than ever hata akienda kugombea jimboni Chato kesho na Magufuli, anachaguliwa tu!!

Na unafuatilia lakini jinsi huyu mama anavyopondwa na kuitwa majina ya kila aina kwa sbb ya hiki anachokifanya anapokuwa amekalia kiti cha spika?

Trust me. Hata wale wenye akili walioko humo humo CCM na serikalini, wanaoona mbali, hawaungi mkono ujinga huu unaofanywa na huyu mama aliyepachikwa hapo!!
 
CCM imepata mtelezo.Ikitaka kupitisha jambo lolote bungeni bila vikwazo vya upinzani inamuambia Tulia aongoze bunge.

CCM sasa inaweza kuamua lini wapinzani wawepo bungeni na lini wasiwepo kwa kutumia msimamo wa UKAWA dhidi ya Tulia.

Haya ni matokeo ya maamuzi ya hasira ya Mbowe. Yatagharimu UKAWA na nchi pia wakati mwingine.

Kuna makosa makuu matatu wanaUKAWA (wale wanaofikiri) tunayajutia sana.Kosa la kwanza ni kukubali Lowassa awe mgombea wetu wa urais.Kosa la pili ni kugomea uchaguzi wa Zanzibar.Na kosa la tatu ni hili la kumgomea Tulia.TUNGOJE.


Watapingana nao wataweza? Mtu kaletwa na rais kwa jambo moja la kuilinda serikali unataka mbowe afanyaje? Kwa nn asikasirike pale ambapo mambo yahusuyo taifa yanapigwa chini wanatanguliza uchama? Idadi ya wabunge wa CCM bungeni ipoje wakiwepo au wakitoka akid inapungua? Vipi ile ripot ya lema walikuwepo bungeni je waliweza kuizuia isihaririwe na serikali? Unataka ukawa wafanyaje? Ujio wa lowasa umeongeza kura upande wa ukawa au umepunguza? Kama zimeongezeka kuna kosa hapo?
 
Endeleni lakini watanzania siyo wajinga mnafanya maigizo mingi wanawangalia tu

Hiyo hoja ya 'watanzania siyo wajinga' imezungumzwa sana na namna ya ukweli...Hata hivyo inaonekana ni kauli inayowafaa CCM zaidi kwani ni kweli 'watanzania siyo wajinga' kukubaliana na mawazo hasi ya UKAWA.
 
Siku zote ukiwa na kiongozi anayetazama mwisho mahali aliposimama ndiyo madhara yake maana kama mbowe ndiyo kila kitu ukawa mtapotezwa sana.
1464806241219.jpg
 
Mbowe is a disgrace to the opposition. Hivi huyu jamaa ana mandate ya kuwa mwenyekiti wa CDM kwa miaka mingapi? He's got to step down now!!
Hakuna anayeweza kumtoa mpaka aamue yeye mwenyewe
 
Wewe ni mfuasi wa Dr Slaa, ulisikia Lowassa ni liability ukaamini hivyo... na slaa angegombea Rais angekuwa Membe na angeshinda kwa kura milioni 10.......... i am sure of that. Lowasa na nyota, hata leo akianzisha amshamsha anaweza kubadilisha mitazamo ya wengi.... Dr Slaa Who??? yule aliyetukimbia kipindi angali tunamhitaji mno? yule aliyeona na nguvu sana zaidi ya chama??? Ni vibaya sana kichwa cha mwananume kutawaliwa na Delila
Ni kweli namkubali dokta Sla.
Huyu Lowassa sio tu kwamba hakuleta faida yoyote kwenye uchaguzi bali ametupotezea vita yetu kuu ya ufisadi.
Leo ona Lusinde anavyotudhalilisha bungeni na hatuna hoja ya kujibu.
 
Ukiona mwanaCCM anamsema Kiongozi wa upinzani vibaya ujue amewashika pabaya.Leo Esther Bulaya aliyekuwa Jembe kwa CCM amekuwa Umma

Alikuwa kiti maalum CCM amekuwa jembe huko aliko mwenzie lembeli wafuasi wa EL
 
Wakisusa sisi twala. Tulia atawanyoosha sana kipindi hiki.
 
mawazo ya mbowe hayaruhusiwi kupingwa, shauri yako utaitwa msaliti!!
 
Alikuwa kiti maalum CCM amekuwa jembe huko aliko mwenzie lembeli wafuasi wa EL

Lakini ndiyo CCM wanamponda kwelikweli sasa hivi,Angalia posts zao ndipo utajua kwa nini sasa hivi ni UMMA kwa CCM na si JEMBE tena
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni kweli namkubali dokta Sla.
Huyu Lowassa sio tu kwamba hakuleta faida yoyote kwenye uchaguzi bali ametupotezea vita yetu kuu ya ufisadi.
Leo ona Lusinde anavyotudhalilisha bungeni na hatuna hoja ya kujibu.
Kama unaogopa vita ya maneno ya Lusinde basi wewe ni Kwisha.... Yule ni specialist wa majungu wa CCM.
 
Kwani Magufuli si Dr? Pamoja na kuwa Dr mbona sukari imempiga mueleka mkubwa sana. Pamoja na kuwa Dr mbona hana sera zaidi ya sera za kukurupuka na udikteta? Unaweza ukawa umesoma madarasa yote lakini kama huna sifa ya kuongoza watu basi kamwe hutafanikiwa na yule ambaye ana elimu ya chini kuliko wewe ambaye ana kipaji cha kuongoza watu akafanikiwa. Unadhani Mbowe angekuwa hakubaliki, CUF ya Maalim Seif na NCCR ya Mbatia ingemkubali na kuungana na CHADEMA ili kuunda UKAWA na kumpa yeye uenyekiti wa UKAWA? Tafakari kwa kina kabla ya kukurupuka.

Hivi Mbowe ana elimu gani? Kama huyo ndo engine ya wapinzani TZ basi safari ya wapinzani ni ndefu saaana! Hoja hupingwa kwa hoja, hivyo wapinzani kujinunisha na kuondoka bungeni utoto huo hadi lini? Ivi bunge pia linafanya majukumu sawa na Vyuo au shule kuwaelimisha baadhi ya wabunge...............? Ivi Wabunge wa namna hiyo ya mkuu wao wanahakika na wanachokifanya kweli au wanafuatanafuatana mikumbomikumbo tu?. Nionanvyo mimi, upinzani TZ unajihimbia kaburi.
 
Lakini ndiyo CCM wanamponda kwelikweli sasa hivi,Angalia posts zao ndipo utajua kwa nini sasa hivi ni UMMA kwa CCM na si JEMBE tena

Yaani amesilimu juzi leo kawa mchungaji? Ndio wenzie wanamshangaa vipi huyu wa jana kawapita aliowakuta
 
Avatar uliyoweka na kitu ulichoandika kina-tudhalilisha sisi academician. Please try to change it or change your mindset and the way u used to think.
 
Back
Top Bottom