Kosa kuu la tatu la UKAWA

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,779
1,304
CCM imepata mtelezo.Ikitaka kupitisha jambo lolote bungeni bila vikwazo vya upinzani inamuambia Tulia aongoze bunge. CCM sasa inaweza kuamua lini wapinzani wawepo bungeni na lini wasiwepo kwa kutumia msimamo wa UKAWA dhidi ya Tulia. Haya ni matokeo ya maamuzi ya hasira ya Mbowe. Yatagharimu UKAWA na nchi pia wakati mwingine.

Kuna makosa makuu matatu wanaUKAWA (wale wanaofikiri) tunayajutia sana.Kosa la kwanza ni kukubali Lowassa awe mgombea wetu wa urais.Kosa la pili ni kugomea uchaguzi wa Zanzibar.Na kosa la tatu ni hili la kumgomea Tulia.TUNGOJE.
 
Wabunge wengi wa CCM ni wasaliti wa Watanzania. Mfano siku ya Hajatulia Jipu alipozuia mjadala wa kufukuzwa wanafunzi wa UDOM hata baadhi ya Wabunge wa CCM waliwaunga mkono na mguu wabunge wa upinzani na wao kutoka Bungeni. Jioni wakarudia unafiki wao baada ya kutishwa na wakubwa wao kwamba atakayetoka anaweza kabisa kufukuzwa CCM na hapo ndiyo itakuwa mwisho wa ubunge wake na hakuna aliyethubutu kutoka.

Hivyo uwepo au kutokuwepo kwa Wabunge wa upinzani hausaidii chochote kwa hiki chama cha majipu kupitisha madudu yao, ila sasa kinachokosekana ni mijadala ya Wabunge wa upinzani kuichachafya Serikali kwenye madudu yao mbali mbali kwa mfano kupunguza bajeti ya CAG kwa 50%.

CCM imepata mtelezo.Ikitaka kupitisha jambo lolote bungeni bila vikwazo vya upinzani inamuambia Tulia aongoze bunge.

CCM sasa inaweza kuamua lini wapinzani wawepo bungeni na lini wasiwepo kwa kutumia msimamo wa UKAWA dhidi ya Tulia.

Haya ni matokeo ya maamuzi ya hasira ya Mbowe. Yatagharimu UKAWA na nchi pia wakati mwingine.

Kuna makosa makuu matatu wanaUKAWA (wale wanaofikiri) tunayajutia sana.Kosa la kwanza ni kukubali Lowassa awe mgombea wetu wa urais.Kosa la pili ni kugomea uchaguzi wa Zanzibar.Na kosa la tatu ni hili la kumgomea Tulia.TUNGOJE.
 
Pole sana mtoa Mada, maadamu nchi hii ni demokrasia na bando umenunua kwa pesa zako basi tunakuvumilia lililo muhimu ni kukuelimisha.

Suala la Lowasa.
Kwa wana CCM na wenye fikra duni Lowasa si lolote na hakustahiri kupewa nafasi UKAWA. Swali la kujiuliza kama sio Lowasa nani alistahili?
Kwa wenye kujua kufanya ulinganifu kwa kutumia "input output ratio" wanajua ni kwa kiasi gani ametoa mchango na hamasa kubwa katika uchaguzi uliopita.

Uchaguzi wa Zanzibar.
Haramu ni haramu. Huwezi kusema kitendo cha kuufuta uchaguzi wa Zanzibar kilikuwa haramu "then" Ukikubali kushiriki uchaguzi wa marudio. Kilicho muhimu ni historia imeandikwa "Kuna chama kimeamua kung'ang'ania madaraka pasipo ridhaa ya wananchi"
Kumsusia Dr.
Kumbuka sisi bunge letu linaendana na kanuni za mabunge ya jumuiya ya madola. Fuatilia ujue wengine huwa wa nafanyaje?
 
CCM imepata mtelezo.Ikitaka kupitisha jambo lolote bungeni bila vikwazo vya upinzani inamuambia Tulia aongoze bunge.

CCM sasa inaweza kuamua lini wapinzani wawepo bungeni na lini wasiwepo kwa kutumia msimamo wa UKAWA dhidi ya Tulia.

Haya ni matokeo ya maamuzi ya hasira ya Mbowe. Yatagharimu UKAWA na nchi pia wakati mwingine.

Kuna makosa makuu matatu wanaUKAWA (wale wanaofikiri) tunayajutia sana.Kosa la kwanza ni kukubali Lowassa awe mgombea wetu wa urais.Kosa la pili ni kugomea uchaguzi wa Zanzibar.Na kosa la tatu ni hili la kumgomea Tulia.TUNGOJE.
Kuna ombwe ya uongozi. Nadhani Mbowe sasa amefikia kikomo cha uwezo wake wam[pe Professor Baregu au professor Safari. Angekuwa Dr Slaa yupo haya tusingeyaona. Unajitoa Bungeni kwa sababu Mwenyekiti humpendi tukueleweje? Ndivyo walivyokutuma wapiga kura? Mheshimiwa Sugu, wewe ni Mnyakyusa na Tulia ni Mnyakyusa, angalia nexty time Wanyakyusa watakubwaga. Lakini la muhimu nadhani ni kwamba CHADEMA ni kampuni, mwenye hisa kubwa alikuwa Mbowe na Ndesamburo wakaziuza kwa Lowassa. Sasa hakuna mwenye ubavu wa kumtoa Mr Mbowe labda apate baraka za Lowassa. Lowassa naye hatathubutu kujitokeza waziwazi kwa sababu anadhani kuna siri kuwa yeye siyo mmiliki wa CHADEMA kumbe watu wanajua. KIna Mbatia na Zitto ndiyo wabunge huru waliobaki, bora wangejiangalia vizuri wakaamua mambo yao kwa maslahi ya waliowachagua siyo kwa kuburuzwa na Mbowe. Tusi[poteze muda, hili ni sikio la kufa.
 
I think aliyetoa post hakufanya upembuzi yakinifu wa madhanio yake.

Labda tumpe muda akafikiri upya tena................
 
Ukiona mwanaCCM anamsema Kiongozi wa upinzani vibaya ujue amewashika pabaya.Leo Esther Bulaya aliyekuwa Jembe kwa CCM amekuwa Umma
 
Wewe ni mfuasi wa Dr Slaa, ulisikia Lowassa ni liability ukaamini hivyo... na slaa angegombea Rais angekuwa Membe na angeshinda kwa kura milioni 10.......... i am sure of that. Lowasa na nyota, hata leo akianzisha amshamsha anaweza kubadilisha mitazamo ya wengi.... Dr Slaa Who??? yule aliyetukimbia kipindi angali tunamhitaji mno? yule aliyeona na nguvu sana zaidi ya chama??? Ni vibaya sana kichwa cha mwananume kutawaliwa na Delila
 
Asiyeona athari za wabunge kususa bunge basi upeo wake ni mdogo sana.
Hivi pamoja na matatizo yote yaliyopo bado hoja zote za serikali zipite kwa ndiooo kubwa kutoka kwa wabunge wa CCM wanainchi wanalionaje bunge?
 
Wewe ni mfuasi wa Dr Slaa, ulisikia Lowassa ni liability ukaamini hivyo... na slaa angegombea Rais angekuwa Membe na angeshinda kwa kura milioni 10.......... i am sure of that. Lowasa na nyota, hata leo akianzisha amshamsha anaweza kubadilisha mitazamo ya wengi.... Dr Slaa Who??? yule aliyetukimbia kipindi angali tunamhitaji mno? yule aliyeona na nguvu sana zaidi ya chama??? Ni vibaya sana kichwa cha mwananume kutawaliwa na Delila
Hahaha ...siku ukijua siasa za nchi hii ..utatamani kufuta comments zako ...zinachezwa sinema lakini sababu ya ushabiki wetu ...tunajitengenezea wenyewe conspiracy theory kujustify ushabiki wetu ....kama tungeacha akili zetu zifikiri vyema bila kuongozwa na ushabiki ....ungejua hii michezo alafu ungejikalia pembeni tu ...
 
Hivi Mbowe ana elimu gani? Kama huyo ndo engine ya wapinzani TZ basi safari ya wapinzani ni ndefu saaana! Hoja hupingwa kwa hoja, hivyo wapinzani kujinunisha na kuondoka bungeni utoto huo hadi lini? Ivi bunge pia linafanya majukumu sawa na Vyuo au shule kuwaelimisha baadhi ya wabunge...............? Ivi Wabunge wa namna hiyo ya mkuu wao wanahakika na wanachokifanya kweli au wanafuatanafuatana mikumbomikumbo tu?. Nionanvyo mimi, upinzani TZ unajihimbia kaburi.
 
Ndio kuna Uhuru Wa mawazo ndio unao kulinda mtoa mada , hayo sio makosa sema watqnzania wengi wamefugwa akili zao ndio sababu wana wahi kudanganyika nakuhakikishia miaka mitano itapia na hapatakuwa na viwanda Tanzania
 
Back
Top Bottom