Ni vigogo gani wanatengeneza jezi feki za Simba, Yanga na Taifa Stars? Kwanini dola inaogopa kuwachukulia hatua? Wanalipa kodi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
897
4,187
1698278770486.png

Nimeona viongozi wa vilabu vya mpira ndio wanahangaika na watu wanaotengeneza jezi feki. Najiuliza ni halali kisheria mtu kutengeneza jezi feki Tanzania?

Mbona kwenye bidhaa nyingine watu huchukuliwa hatua kali za kisheria? Au wanaotengeneza ndio vigogo wenye nchi? Tukiendelea hivi haiwezekani hawa viongozi wa vilabu wakashambuliwa na wananchi au wana mtandao wa biashara hizi zisizolipa hata kodi?

TRA na Polisi mpo wapi kwenye hujuma hizi za kiuchumi?

Pia soma: Kontena zaidi ya 2 ya Jezi feki zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2 zakamatwa
 
Kuna tatizo na nadhani Viongozi wa Serikali ''wanahusika'' kwa namna fulani.

Timu zetu zimefanya yale yanayofanywa na vilabu duniani kuepuka ' kupitisha mabakuli' Tumeona usajili unavyokuwa makini na Timu zinavyofanya vizuri Kimaaifa

Kuuza jezi FEKI ni kujumu Simba, Yanga na Taifa stars kwa ujumla. Huu ni wizi kama wizi mwingine

Nilitegemea kuanzia jana tungemsikia Waziri Ndumbaro , Waziri Masauni, IGP Wambura n.k. wakifuatilia jambo! kimyaa. Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) ni kinara wa kesi za mafao ya Wasanii, hivi hili la mpira halioni?

Hii ina maana moja, kwamba wanajua hawawezi kuthubutu au ni sehemu ya mpango huo.

Huu ni wizi unaofumbiwa macho ukiachiwa akina Ali Kamwe

Ali Kamwe na Ahmed wa Simba ulizeni katika vyombo vya habari ikiwa serikali imeruhusu wizi wa namna hii

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Nimeona viongozi wa vilabu vya mpira ndio wanaangaika na watu wanaotengeneza jezi feki. Najiuliza ni halali kisheria mtu kutengeneza jezi feki Tanzania? Mbona kwenye bidhaa nyingine watu uchukuliwa hatua kali za kisheria ? Au wanaotengeneza ndio vigogo wenye nchi? Tukiendelea hivi haiwezekani hawa viongozi wa vilabu wakashambuliwa na wananchi au wana mtandao wa biashara hizi zisizolipa hata kodi? TRA na Polisi mpo wapi kwenye hujuma hizi za kiuchumi?
Unatafuta matatizo, nakushauri kaa kimya. Utakuja kunishukuru
 
Nimeona viongozi wa vilabu vya mpira ndio wanaangaika na watu wanaotengeneza jezi feki. Najiuliza ni halali kisheria mtu kutengeneza jezi feki Tanzania? Mbona kwenye bidhaa nyingine watu uchukuliwa hatua kali za kisheria ? Au wanaotengeneza ndio vigogo wenye nchi? Tukiendelea hivi haiwezekani hawa viongozi wa vilabu wakashambuliwa na wananchi au wana mtandao wa biashara hizi zisizolipa hata kodi? TRA na Polisi mpo wapi kwenye hujuma hizi za kiuchumi?
Trust me hawatakaa wajulikane na hata kama wakijulikana hiyo kesi itaishia hewani mzigo utataifishwa ili ukapigwe mnada kwa ajili ya kuharibiwa.. Litachezwa dili lingine na haohao kisha mzigo utarudi sokoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni Serikali ya Tanzania buana!! Inasikitisha sana tumeona mengi yakifinywa hivihivi.

Kuna mjamaa alikutwa amevuta wire wa Bomba la mafuta hadi kwa nyumba isiyoishi watu huko Kigamboni na malori ndani kibao! Tukaaminishwa amepatikana na atashughulikiwa kisheria!!

Hadi leo haijawahi eleweka iliendaje.

Ni TZ pekee mwenge unakimbizwa kaa shetani!!!
 
Nimeona viongozi wa vilabu vya mpira ndio wanaangaika na watu wanaotengeneza jezi feki. Najiuliza ni halali kisheria mtu kutengeneza jezi feki Tanzania? Mbona kwenye bidhaa nyingine watu uchukuliwa hatua kali za kisheria ? Au wanaotengeneza ndio vigogo wenye nchi? Tukiendelea hivi haiwezekani hawa viongozi wa vilabu wakashambuliwa na wananchi au wana mtandao wa biashara hizi zisizolipa hata kodi? TRA na Polisi mpo wapi kwenye hujuma hizi za kiuchumi?
Vyomba vya ulinzi nchi hii havina maadili kabisa. Vyombo vya habari ni useless sijawahi kuona.
 
Mimi naona inawezekana ikawa pia ni dili la hawahawa wazabuni wa hizi timu kwasababu hizi original ni ghali na wananchi wengi hawamudu hivyo wakaona wajiongeze.

Inawezekana wakawa wanawacheka tu kina Kamwe. Cha muhimu tusubiri kauli ya wanausalama
 
Sio kweli. Mi ndio kazi zangu hizo. ila sio hao wazabun kama unavyosema Kuna mengi ndani yake. Kwa kifupi ni ngumu kudhibiti biashara feki kwa nchi zinazoibukia au zenye uchumi mdogo. Ni cartels business. Hata china kwenyewe hawawez sembuse sisi.
 
Nimeona viongozi wa vilabu vya mpira ndio wanahangaika na watu wanaotengeneza jezi feki. Najiuliza ni halali kisheria mtu kutengeneza jezi feki Tanzania?

Mbona kwenye bidhaa nyingine watu huchukuliwa hatua kali za kisheria? Au wanaotengeneza ndio vigogo wenye nchi? Tukiendelea hivi haiwezekani hawa viongozi wa vilabu wakashambuliwa na wananchi au wana mtandao wa biashara hizi zisizolipa hata kodi?

TRA na Polisi mpo wapi kwenye hujuma hizi za kiuchumi?

Pia soma: Kontena zaidi ya 2 ya Jezi feki zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2 zakamatwa
Nimeshangaa kumuona ali kamwe kwenda kukamata izo jezi fake akiwa na waandishi wa habari bila ya polisi na sitaki kuamini kuwa hawakupewa taarifa.

Hili suala inaonekana serikali hailitilii mkazo sijui kwanini? Au ndio wanatafuta hela za kampeni?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Sio kweli. Mi ndio kazi zangu hizo. ila sio hao wazabun kama unavyosema Kuna mengi ndani yake. Kwa kifupi ni ngumu kudhibiti biashara feki kwa nchi zinazoibukia au zenye uchumi mdogo. Ni cartels business. Hata china kwenyewe hawawez sembuse sisi.
Kazi zako kuchapisha jezi fake?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Trust me hawatakaa wajulikane na hata kama wakijulikana hiyo kesi itaishia hewani mzigo utataifishwa ili ukapigwe mnada kwa ajili ya kuharibiwa.. Litachezwa dili lingine na haohao kisha mzigo utarudi sokoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona unaongea lugha gongana. Kwanza umesema mzigo utataifishwa na kupigwa mnada, Kwa ajili ya kuharibiwa hapo hapo unasema itarudi sokoni. Sasa mnada ni kuuzwa tena.
 
Back
Top Bottom