Kongamano la miaka 62 ya uhuru ya iliyokuwa Tanganyika SUA

Djob Nkondo

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
232
181
Baada ya kumaliza kula michembe na maziwa nimekaa zangu kwenye duka la Muha nikaona mdahalo unaoendelea muda huu kupitia TBC 1 ambapo wadau mbalimbali wanajadili masuala mbalimbali hususani uendeleshwaji wa kilimo kwa kileo wanaita uchumi wa blue.

Kwa uelewa wangu mdogo nimeona na kujifunza kua hakuna au kuna uchache au kutokuwepo kabisa kwa watu wanaojihusisha na kilimo. Kwa kutolea mfano tu kuna kijiji nilikua naishi ambapo nachelea kusema pembejeo zinazoitwa za ruzuku (mbolea) bei inayouzwa hakuna mwanakijiji hata mmoja kijijini kwetu aliyeweza kununua. Familia nyingi kijiji nilipokua zina endeshwa kwa mitaji ya kuuza nyanya, maembe na msaada kutoka kwa ndugu walioko mjini mbolea ya ruzuku mfuko mmoja 75,000 TZS, Mbegu ya kisasa ya mahindi Kilo Mbili hapa kijijini inauzwa 15,000 TZS.

Kijiji nilipo hakuna afsa ugani, mtendaji wa kijiji ambaye hana taaluma ya kilimo ndo anakaimu nafasi ya afsa ugani. Mabilioni yalowekezwa yangeelekezwa kwenye kuajiri mafsa kilimo na ugawaji wa pembejeo kungekua na matokeo chanya kuliko siasa ninazoziona zikiendelea runingani. Ngoja nirudi zangu shamba nisubiri uchumi wa buluuu.
 
Back
Top Bottom