Kongamano la Kitaifa la Kiongozi wa Dini kuombea Uchaguzi kufanyika 24/08/2020, mgeni rasmi atakuwa Rais Magufuli

Hao sio viongozi wa dini ni wajasiliamali wa dini. Wahuni na wala sadaka tu!

Ila Bora Lissu awajue wanafiki wote ili akiingia ikulu ajue amsikilize kiongozi yupi wa dini!

Hawa watu wamefanya hata watu wasiwe na hamu tena ya kwenda kanisani wala msikitini.
Well said. Nitakutafuta nikupe bando la mwezi mzima.
 
Kanisa katoliki hakuwepo askofu hata mmoja

Naona dini inatumika kisiasa

wiki iliyopita ilikuwa ni TAG, kisha baada ya hapo Taasisi za dini zikaitisha kongamano la kusifu utendaji wa serikali ya Magufuli na ghafla wiki moja baadae eti kuna kongamano lingine la kuombea uchaguzi kisha mualikwa ni Magufuli

Waache wafanye hii michezo yao ya kulifanyia propaganda jina tukufu la Mwenyezi Mungu waje waone mwisho wake! .

Mungu hadhihakiwi!
 
BAKWATA wanajengewa msikiti na ofisi kubwa na serikali, hivyo walijengewa ili watumike kwenye mazingira haya.

Shida ya waislamu siyo misikiti.

Wanayo misikiti mingi tu kila mahali.

BAKWATA ni tawi na nyenzo muhimu ya Dola ya kuwakeep incheck waislamu na bahati mbaya CCM ya Magufuli inaiabuse hii taasisi kwa kuitumia kisiasa kupitiliza!
 
Kuna watu wanamuangalia Mungu wanamuona kama mpambe wao tu hivi lkn wasubiri iko siku.

Watu wamejaa dhambi hadi wengine mikono ni damu tupu utafikiri muuza bucha halafu eti wanaandaa sijui takataka gani huko Dodoma. Useless kabisa.
 
johnthebaptist,

Masheikh wa bakwata, ccm na wale wanao jiita mastaa katika nchi hii wote ni sawa hawatofautiani hata kidogo.

Kama kongamano ni la viongozi wa dini, je magufuli anahusika vipi kuwa mgeni rasmi?

Sheikh mkuu wa DSM imekuaje akahitishe kongamano Dodoma?

Ina maana Dodoma hakuna sheikh wa mkoa?

Kama lengo ni kuombea uchaguzi kwa nini mgombea wa chama kimoja awe mgeni rasmi?

Huu ni unafiki wa wazi sana, na dhambi ya unafiki ni mbaya sana mbele ya m/mungu.
 
Naona dini inatumika kisiasa

wiki iliyopita ilikuwa ni TAG, kisha baada ya hapo Taasisi za dini zikaitisha kongamano la kusifu utendaji wa serikali ya Magufuli na ghafla wiki moja baadae eti kuna kongamano lingine la kuombea uchaguzi kisha mualikwa ni Magufuli

Waache wafanye hii michezo yao ya kulifanyia propaganda jina tukufu la Mwenyezi Mungu waje waone mwisho wake! .

Mungu hadhihakiwi!

Viongozi wote wanao hudhuria hiyo mikutano.... Wanaenda kuhakikiwa na malipo yao yatalipwa kwa kwaajiri ya kuwapigia kampeni....

Umesahau ktk orodha ya eskrow ht maaskofu walikuwa na mgao wao...
 
CCM maji ya shingo, kutoka Chama cha siasa chenye ushawishi hadi kuwa genge la wachumia tumbo wanao kodi wasanii na viongozi wa dini ili kulazimisha kukubalika. Hamtoboi na hao majeshi yenu ya kukodi mwaka huu. Watanzania hawataki ujinga.
 
Shehe wa mkoa wa Dsm alhad Mussa Salum ametangaza kuwepo kwa kongamano kubwa la viongozi wa dini jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea uchaguzi na kutoa mwelekeo kwa waumini kuhusu mazingatio wakati wa uchaguzi.

Kongamano hilo litafanyika katika uwanja wa Jamhuri na mgeni rasmi atakuwa Rais Magufuli.

Source: Star TV habari.

Maendeleo hayana vyama!
Kampeni zimepamba moto mwaka huu.
 
Halafu kumuhusisha mungu kwenye issue za kijnga jinga kama hizi tuache
 
Back
Top Bottom