Kongamano la Kitaifa la Kiongozi wa Dini kuombea Uchaguzi kufanyika 24/08/2020, mgeni rasmi atakuwa Rais Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,752
139,555
Shehe wa mkoa wa DSM Alhad Mussa Salum ametangaza kuwepo kwa kongamano kubwa la viongozi wa dini jijini Dodoma kwa ajili ya kuombea uchaguzi na kutoa mwelekeo kwa waumini kuhusu mazingatio wakati wa uchaguzi.

Kongamano hilo litafanyika katika uwanja wa Jamhuri na mgeni rasmi atakuwa Rais Magufuli.

Source: Star TV habari.

Maendeleo hayana vyama!
 
Maelekezo ya mchakato wa uchaguzi yashatolewa na Sheikh Ponda tayari. Hayo mengine yanatokea wapi?

Nyie masheikh kuowa nakushangaeni sana. Magu kwenye suala la uchaguzi ni mshiriki kama walivo washiriki wengine. Hamuwezi kumpa special treatment kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ni upendeleo.

Jee mtume Muhammad ndivo alivowafunza hivyo? Magu alitakiwa awe Mualikwa tu pamoja na watia nia kutoka vyama vyengine. Uislamu wenu una udhaifu mkubwa sana Wallahi! Kazi kujipendekeza kwa binadamu mwenzenu.
 
Acha sisi twende kwa maombi na yule msaliti wa nchi mwache aende na mabeberu

Asiyemsujudia rais ndio msaliti!? Chaguzi zote toka Magufuli kaingia madarakani tumeona zikitawaliwa na ushenzi, ukatili, unyama na uhayawani wa wazi. Dini zisitumike kufunika watu waovu. Hiyo ibada ni ya watu waovu wanaotaka kuhadaa umma kumbe ni mashetani waliojivika ngozi ya kondoo.

Ni nani hajui ushenzi uliofanyika kwenye chaguzi za marudio? Ni nani hajui uhayawani uliofanyika kwenye uchaguzi wa SM? Hayo maombi ya wanafiki mbona hayakufanyika wakati wapinzani wanafanyiwa dhuluma, na kupata vilema toka kwa vikundi vya ccm kwa uratibu wa jeshi la polisi?

Nchi yetu ina watu karibia 60m, inawezekana vipi wapiga kura wawe 29m? Hao wahuni waliondaa hayo maombi badala ya kuandaa maombi, kwanini hawajiulizi kuwa kila watanzania wawili mmoja kajiandikisha inawezekana vipi? Ni kweli nchi hii watu wenye miaka 18+ idadi yao ni sawa na walio chini ya miaka 18? Huyo Shehe wa Bakwata anatumika maana kajengewa msikiti na jiwe. Mungu hadhihakiwi na wahuni kwa kofia ya viongozi wa dini.
 
johnthebaptist,

Maombi gani ya kuombea uchaguzi na mnamwalika mgombea mmoja Kama mgeni rasmi, Hawa wachumia tumbo wa dini waache kumpigia Jiwe kampeni juzi tu wametoka kukutana wakamwalika waziri mkuu
 
Naona dini inatumika kisiasa

wiki iliyopita ilikuwa ni TAG, kisha baada ya hapo Taasisi za dini zikaitisha kongamano la kusifu utendaji wa serikali ya Magufuli na ghafla wiki moja baadae eti kuna kongamano lingine la kuombea uchaguzi kisha mualikwa ni Magufuli

Waache wafanye hii michezo yao ya kulifanyia propaganda jina tukufu la Mwenyezi Mungu waje waone mwisho wake! .

Mungu hadhihakiwi!
 
Amri ya Mungu inasema usiue. Kupeleka watu wamuue mwenzio kwa sababu ana mawazo tofauti na wewe ni dhambi kubwa sana. Mtu mwenye roho ya shetani kiasi hicho anastahili kuombewa. Ndio maana viongozi wa dini wameamua kumwombea.
Acha sisi twende kwa maombi na yule msaliti wa nchi mwache aende na mabeberu
 
Mastermind wa hii michezo yote ya kufanya siasa kupitia dini ni BAKWATA kupitia Alhadi.

Hawa BAKWATA wanawadjalilisha sana waislamu mbele ya jamii nzima ya Watanzania.

Wanatumika vibaya!
 
Naona dini inatumika kisiasa

wiki iliyopita ilikuwa ni TAG, kisha baada ya hapo Taasisi za dini zikaitisha kongamano la kusifu utendaji wa serikali ya Magufuli na ghafla wiki moja baadae eti kuna kongamano lingine la kuombea uchaguzi kisha mualikwa ni Magufuli

Waache wafanye hii michezo yao ya kulifanyia propaganda jina tukufu la Mwenyezi Mungu waje waone mwisho wake! .

Mungu hadhihakiwi!

Halafu viongozi wa dini wanaitisha kuombea amani nchi, huku tume ina idadi ya wapiga kura ya kubumba. Watanzania tunakaribia 60m. Inawezekana vipi 29m wawe wamejiandikisha kupiga kura? Ni kweli kila watanzania wawili mmoja kajiandikisha kupiga kura?

Ni kweli nusu ya watanzania wanamiaka 18+, huku walio chini ya miaka 18 ni sawa kabisa na walio juu? Kwa akili ya kawaida tu hili linawezekana? Katika mazingira ambayo tume wana idadi ya wapiga kura ya kubumba wataweza kutangaza matokeo ya kweli?
 
Mastermind wa hii michezo yote ya kufanya siasa kupitia dini ni BAKWATA kupitia Alhadi.

Hawa BAKWATA wanawadjalilisha sana waislamu mbele ya jamii nzima ya Watanzania.

Wanatumika vibaya!

BAKWATA wanajengewa msikiti na ofisi kubwa na serikali, hivyo walijengewa ili watumike kwenye mazingira haya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom