Rais Samia Kuongoza Marais wa Afrika katika Kongamano la Jukwaa la Mifúmo ya Chakula Afrika (AGRF)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Jukwaa la Mifúmo ya Chakula Afrika (AGRF) unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu ambapo marais zaidi ya 15 wamealikwa kushiriki.

Katika kongamano hilo linalofanyika kwa mara ya nchini, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo zaidi ya washiriki 3000 wanaojishughulisha katika mifumo ya chakula, wanatarajiwa kuhudhuria.
Akizungumzia kongamano hilo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alieleza hayo jijini hapa juzi wakati akifungua mkutano wa wadau wa mifugo na uvuvi pamoja na maandalizi va kushiriki katika kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba tano hadi nane mwaka

Kwa heshima ya kipekee naomba nimpongeze Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa mwenyeji wa kongamano hili muhimu litakalohudhuriwa na washiriki zaidi ya 3000 wanaojishughulisha na mifumo ya chakula," alibainisha.

Ulega alibainisha kuwa wizara yake imeadhimiria kuunga mkono mikakati ya pamoja kutekeleza dhana ya mabadiliko na kuchangia katika kutatua matatizo ya mifumo ya chakula Afrika.

"Sekta za mifugo na uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu za kiuchumi zinazochangia katika usalama wa chakula na lishe nchini. Kwa mwaka 2022/2023. Sekta ya Mifugo imekua kwa asilimia 5.0 huku ikichangia asilimia 6.7 kwenye Pato la Taifa," alisema.
Kwa upande wa Sekta ya Uvuvi, alisema imekua kwa asilimia 2.5 na kuchangia asilimia 1.8 katika Pato la Taifa.
Alisema kati ya asilimia 35 ya kaya za Watanzania wanaojishughulisha katika kilimo, wanafuga huku Watanzania milioni 4.5 wameaiiriwa katika shughuli mbalimbali za minyororo ya thamani ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji nchini.

Hata hivyo, alieleza kuwa licha ya mchango huo bado kuna mahitaji ya mazao ya mifugona uvuvi katika soko la ndani na nje ya nchi. Alizitaja changamoto hizo ni kukosekana kwa mitaji, uduni, uhaba wa pembejeo, uhaba wa malisho na vyakula ya mifugo, magonjwa ya mifugo, uhaba wa miundombinu wezeshi ikiwemo minada, masoko, mialo, malambo na nyanda za malisho.
 
Back
Top Bottom