Tetesi: Koko Beach nayo ishauzwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,155
Reaction score
831,828
Hizi kelele wanazopiga hawa vijana hapa ni sawa na kelele za chura ambazo haziwezi kumzuia tembo kunywa maji.

In fact kwasaasa kinauzwa kila kitu

Vikubwa vimeshauzwa vyote

Vya kati vimeshauzwa vyote sasa ni zamu ya vidogo

Wiki iliyopita tulishuhudia uuzwaji wa shule kule Kurasini DSM.

Kabla ya hapo kuna mashamba yenye mahindi yaliyokuwa yamemea vizuri sana kule Ngorongoro.. Kwa taharuki kubwa na kwa mshangao wa wengi yale mahindi yalifyekwa yote kwa amri na usimamizi wa DC

Mwaka jana stendi ya daladala ya simu 2000 iliuzwa. Wananchi walipinga kwa nguvu sana mpaka kufikia kuandamana lakini haikusaidia waliondoshwa kwa nguvu

Maeneo ya wazi karibia yote yalishauzwa, shule za serikali tumeshuhudia mbili zikiuzwa ndani ya mwaka mmoja

Masoko mengi yameuzwa lakini kelele hazikuwa nyingi kwakuwa ilitumika style ya kupiga kibiriti
Hawa vijana nawaonea huruma sana hasa hawa wanaoonekana wakiongea.

Tuwaombee sana sana!

Na si ajabu ndani ya mwezi ujao ukaambiwa COCO BEACH imewaka moto usiku! Maana ajali za moto maeneo kama hayo siku hizi ni kawaida sana

Your browser is not able to display this video.
 
Aisee niliwahi kujiuliza kwa nini sisi maeneo ya fukwe hatufanyi kama wenzetu ni maeneo ya wananchi majengo yanajengwa baada ya bara bara huko ufukweni watu wanaweza kufanya mazoezi umbali mrefu kwenye mchanga au vitofari..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…